kikao cha mwaka cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kinaendelea huko New York,Viongozi wa Nchi za kiafrika wanena! Tz sijui nani katuwakilisha?

mkuu unajua insu kubwa sio kikao husika bali kuna vikao vingine vingi vidogo dogo kati ya maraisi kwa maraisi vinaendelea! kuhusu mahusiano hasa ya kibiashara.ni katika huo mkutano rais anakuwa na uwezo wa kukutana na maraisi wenzake wengi kwa kutumia muda mchache na rasilimali kidogo
Pia kila kiongozi anastaili yake ya kiutawala, cha msingi taifa lisonge mbele
 
Tunae balozi wa kudumu UN atosha
Hicho kikao ni cha kawaida tu cha mwaka,hakuna issue crucial kwetu au kwa nchi rafiki,muacheni balozi atuwakilishe,ingekua enzi za JK mngsema ameenda kutalii
 
Viongozi wa Afrika kwenye vikao vya UN GENERAL ASSEMBLY ni kama vile wale ndugu maskini katika familia wamekutana kwenye kikao cha familia na ndugu zao walio matajiri.
 
Sababu za mkuu kutokusafiri ni simpo sana kuzijuwa. ..mnajuwa vile vimondo vya kiunoni, alivyovielezea yule mchungaji fulani, baadae akaletewa kashikashi hevi? Yeah! Vile vimondo na vibweka kiunoni deili kwenye viwanja vya mtoni hata uwe vvvvp lazima upite kwenye xray kwa sababu za kiulinzi. Mkuu hawezi tia mguu kwa wazungu. Never. Viwanja kwa kiafrika wanaachiana tu kwa sababu lao ni moja.
 
Heti Afrika itatue matatizo yake yenyewe vichekesho kama hivi vinapatika Afrika kwa mfano nani amkemee Museveni au Kagame
 
Sisi tumewakilishwa na huyo jirani yetu mwembamba mrefu kwamba mambo yetu ya Afrika( kama vile kuuawana, kutekana, maiti kwenye viroba, kubambikiana kesi) tuyamalize wenyewe. Amesahau kuwa kulikuwa na vikosi vya Umoja wa Taifa nchini kwake wakati hali tete chini ya Juvenal. Kama hatutaki watukosoe basi tusiwaombe misaada kabisa! Wakitupa Bil 200 tunatangaza nchi nzima vyombo vyote, wakitukosoa tunalalamika. Waafrika akili hatuna!
Sema wewe akili huna, usinijumuishe mimi mkuu
 
Kwani leo si anazindua daraja letu la juu pale bgrn tulilojengewa kwa msaada wa Japan. Sasa angekwenda UN nani angelizindua?
 
Kiswahili hakiruhusiwi?
umesahau alivyohutubia kwa kiswahili addis ababa, hakumpa nafasi mkalimani ya kutafsiri kwa kuwa alijua hana cha kuwaambia waafrika zaidi ya "tumejenga fly over, standard gauge, tumenunua ndege kwa cash"
 
Back
Top Bottom