kikao cha mwaka cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kinaendelea huko New York,Viongozi wa Nchi za kiafrika wanena! Tz sijui nani katuwakilisha?

Econometrician

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
15,785
28,429
Hotuba za viongozi wa dunia katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa zimeingia siku yake ya pili mjini New York, ambako marais wa Afrika tayari wameshahutubia kikao hicho cha kila mwaka cha Umoja wa Mataifa.
1537976699603.png

Rais wa Kongo Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambaye alizungumza hapo jana alilihakikishia baraza hilo kuwa uchaguzi utafanyika nchini mwake mwaka huu, huku Rais Paul Kagame wa Rwanda, ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, akielezea umuhimu wa Waafrika kutatua mizozo ya Afrika wenyewe.

Rais Kabila amezikosoa vikali nchi zinazoingilia kati masuala ya ndani ya Kongo na kusema ni kinyume na misingi ya kimataifa. Huku akihakikisha kwamba taratibu ya uchaguzi nchini mwake haziwezi tena kupotoshwa. "Nimehakikisha kwamba uchaguzi uliotarajiwa Desemba mwaka huu utafanyika."

Kuingiliwa masuala ya ndani ya nchi
1537976767047.png


Rais huyo wa DRC aliendelea kusema "Hatuwezi kujenga Umoja wa Mataifa ikiwa kutakuwepo na moja wapo ya serikali inayoingilia kati maswala ya ndani ya nchi zingine. Ni mshangao kuona Umoja wa Mataifa umeendelea kuachia hali hiyo ikiendelea na kujipumbaza. Na ndio sababu msimamo wa nchi yangu ni ule wakukataa uingiliaji kati wa maswala ya ndani ya Kongo." alisema rais Kabila

Kwenye hotuba yake Rais Kabila aliomba kuondolewa kwa wanajeshi wa Umoja Mataifa amabao amesema kazi yao haijawaridhisha Wakongomani. Miaka 20 baada ya kuletwa Kongo kikosi hicho kinaonyesha udhaifu na mafanikio yake kuhusu operesheni za kijeshi. Na kusema serikali yake imeelezea kwa mara nyingine tena lazima ya kuondolewa kwa wanajeshi hao.

Wakati Congo ikilaumiwa na mas ya kutetea haki za binadamu,lakini rais Kabila amesema kwamba deokrasia ya nchi yake ni mfano wa kuigwa.

Kwenye sekta ya kiusalama rais kabila amelani ashambulizi ya mara kwa mara ya makundi ya wapiganaji aliyoyaita kuwa mashambulizi ya kigaidi,mfano wa huko Beni alisema.

Kwa upande wake rais wa Rwanda Paul kagame ambae alikuwa rais wa mwanzo wa Afrika kuhutubia alitioa wito wa kujenga amani na usalama barani Afrika. Huku akilezea kwamba matatizo ya Afrika lazima yatatuliwe na Waafrika wenyewe. Ameyatolea mfano makundi ya kigaidi huko Afrika Magharibi na eneo la Sahel.

Marais wengine akiwemo Cyril Ramaphosa ametoa wito wa kufanyika mageuzi katika Umoja wa Mataifa huku akiomba viti viwili vya kudumu kwenye Baraza la Usaama la Umoja wa Mataifa mahususi kwa Bara la Afrika. Mikutano mingine kadhaa kuhusu maendeleo na kupambana na rushwa barani afrika imetarajiwa sambaba na kikao hiki cha umoja wa mataifa.
 
Sisi tumewakilishwa na huyo jirani yetu mwembamba mrefu kwamba mambo yetu ya Afrika( kama vile kuuawana, kutekana, maiti kwenye viroba, kubambikiana kesi) tuyamalize wenyewe. Amesahau kuwa kulikuwa na vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini kwake wakati hali tete chini ya Juvenal. Kama hatutaki watukosoe basi tusiwaombe misaada kabisa! Wakitupa Bil 200 tunatangaza nchi nzima vyombo vyote, wakitukosoa tunalalamika. Waafrika ni shida
 
Role model wetu ( ambaye tunasema ni smartest Afrika Mashariki)mbona yeye anaenda kutwa kwa Wazungu huku sisi tunasema havina maana hivyo vikao ni soga tu. Ni kweli havina uzito kwa Taifa letu?
 
Nakubaliana na wewe,sasa kwa mtindo unaoendelea umoja wa mataifa ndilo kusudio la awali?,la kuanzishwa kwake?
mkuu unajua insu kubwa sio kikao husika bali kuna vikao vingine vingi vidogo dogo kati ya maraisi kwa maraisi vinaendelea! kuhusu mahusiano hasa ya kibiashara.ni katika huo mkutano rais anakuwa na uwezo wa kukutana na maraisi wenzake wengi kwa kutumia muda mchache na rasilimali kidogo
 
mkuu unajua insu kubwa sio kikao husika bali kuna vikao vingine vingi vidogo dogo kati ya maraisi kwa maraisi vinaendelea! kuhusu mahusiano hasa ya kibiashara.ni katika huo mkutano rais anakuwa na uwezo wa kukutana na maraisi wenzake wengi kwa kutumia muda mchache na rasilimali kidogo
Napinga mkuu,fursa hazitafutwi kwenye kikao hicho,nchi kama nchi tuna representatives wa kutosha,labda kupiga selfie tu
 
Back
Top Bottom