Kikao cha kuunda TANU nyumbani kwa Hamza Kibwana Mwapachu - Nansio, Ukerewe 1953

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,909
30,253
KIKAO CHA KUUNDA TANU NYUMBANI KWA HAMZA KIBWANA MWAPACHU NANSIO, UKEREWE 1953
Ilikuwa miezi ya mwanzo ya mwaka wa 1953 kabla ya kufika April, 1953.

Abdul Sykes Act. President na Secretary wa TAA akifuatana na Ali Mwinyi Tambwe Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) walikwenda Nansio, Ukerewe nyumbani kwa Hamza Mwapachu.

Abdul Sykes alikuwa anataka kupata kauli ya mwiisho ya Hamza Mwapachu kuhusu Julius Nyerere kuingizwa katika uongozi wa juu wa TAA kwenye uchaguzi wa viongozi wa TAA uliokuwa ufanyike mwezi April.

Uchaguzi ulifanyika kama walivyokubaliana watu hawa watatu na TAA ikawa chini ya uongozi wa Julius Kambarage Nyerere kama ilivyo hapo chini:

J.K. Nyerere, President; Abdulwahid Sykes, Vice-President; J.P. Kasella Bantu, General Secretary; Alexander M. Tobias, Waziri Dossa Aziz, Joint Minuting Secretary; John Rupia, Treasurer, Ally K. Sykes Assistant Treasurer.

Committee members: Dr. Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo, Patrick Aoko.

(Tanganyika Standard 19 June 1953)
Angalia na sikiliza historia hii hapo chini:

Huu uchaguzi ,Nyerere alimshinda Abdul Sykes...... Abdul sijui kwa nini aliamua kushindana na Nyerere, bora angejitoa tu, hakutumia busara.
 
Hii familia ya Sykes kama wangesoma wangekuwa mbali Sana

..hiyo sio familia ya walalahoi.

..ni watu waliofanikiwa ktk biashara na siasa / utawala.

..kuna Ally Sykes ambaye alikuwa mfanyabiashara na tajiri mkubwa hapa Dsm.

..pia alikuwepo Abbas Sykes ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Jimbo la Mashariki[kabla mikoa haijaundwa], na baadae balozi wa Tz ktk nchi mbalimbali.

..Ukiacha hao wazee waasisi wa Tanu, kuna Kleist Sykes ambaye aliwahi kuwa meya wa jiji la Dsm kati ya mwaka 2000 mpaka 2005.
 
Huu uchaguzi ,Nyerere alimshinda Abdul Sykes...... Abdul sijui kwa nini aliamua kushindana na Nyerere, bora angejitoa tu, hakutumia busara.
Vito...
Dots katika kanuni za uandishi unaandika tatu tu...

Nimefurahi kuwa katika yote niliyoeleza katika historia hii ulichokiona kikubwa kwako ni kuuliza kwa nini Abdul hakujitoa katika uchaguzi ule.

Hili swali lishaulizwa hapa mara kadhaa na nimelijibu.
Ulikuwa unaijua historia hii?

Historia ya African Association (AA) 1929 hadi kufikia TANU 1954 ina uhusiano mkubwa sana na ukoo wa Sykes kama waasisi na wafadhili wake.

Abdul angejitoa uchaguzi ule dhidi ya Nyerere wanachama wangehisi kachukia na kasusa na hii ingevuruga murua wa TAA na pengine kukiridusha chama nyuma sana.

Abdul alikuwa anaungwa mkono na wanachama wengi kutoka 1950 alipoingia katika uongozi na Dr. Vedasto Kyaruzi.

Kujitoa katika uongozi katika kipindi kile cha uchaguzi isingekuwa kitu cha busara.
Nyerere pale anaingia katika uchaguzi hakuwa anajulikana Dar es Salaam.

Judith Listowel kakielez kisa hiki vizuri sana katika kitabu chake, ''The Making of Tanganyika, '' (1965).

Sikiliza maneno ya Hamza Mwapachu kwa Abdul Sykes kuhusu uchaguzi uliokuwa mbele yao na umuhimu kwa kuunda TANU katika uchaguzi ujao wa 1954.

Kwa nini umeshughulishwa na kujitoa kwa Abdul na siyo imekuwaje historia ya TANU imeandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni Abdul Sykes na Hamza Mwapachu hawakutajwa katika kitabu hicho?

Au huamini kuwa haya niliyoeleza ndiyo historia ya kweli ya TANU?
Hivyo vitabu hapo chini kuhusu historia ya TANU vinatoka kwenye chanzo kimoja.

Kitabu cha Abubakar Ulotu kimenakiliwa kutoka mswada uliokuwa katika maktaba ya TANU ulioandikwa na Dr. Wilbard Klerruu 1962/63.

Kitabu Chuo Cha Kivukoni hakiko tofauti sana na kitabu cha Ulotu.

Vitabu vyote hivi viwili vinatokana na mradi wa TANU wa kuandika historia yake ambao mwandishi mkuu alikuwa Abdul Sykes akisaidiwa na Dr. Kleruu lakini kwa bahati mbaya Abdul akajitoa katika kazi hii.

Dr. Klerruu akakamilisha mswada lakini haukukuchapwa.
Kitabu cha Abubakar Ulotu inaaminika unatokana na mswada huu.

Screenshot_20220510-075746_Facebook.jpg
 
Hii familia ya Sykes kama wangesoma wangekuwa mbali Sana
Msa...
Wamesoma vizuri.

ikutoshe tu kuwa Abdul angeingia Makerere kama si kutiwa jeshini kwenda kupigana Burma katika WWII.

Baada ya vita Abdul alipata ''admission,'' Princeton University, Marekani lakini hakwenda.

Abbas Sykes alipelekwa na baba yake King's College Budo, Uganda elimu ya msingi na alisoma darasa moja na Kabaka Edward Mutesa.

Sidhani kama kuna mtoto Tanganyika katika miaka ile ya 1930s aliyesoma King's College Budo achilia kutolewa nchini kwenda kusomeshwa nje.
 
Abdul Sykes alikuwa mkorofi korofi sana, labda kwa sababu alikuwa bondia, hata uongozi wa TAA aliuchukua kwa kumfanyia vurugu baba yake, nadhani ndio maana Nyerere aliwaweka kando hii familia.
Vito...
Hapa hatuzungumzi kuwekwa kando mtu yeyote tunazungumza suala la kuwa na historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ambayo si ya kweli.
 
Vito...
Dots katika kanuni za uandishi unaandika tatu tu...

Nimefurahi kuwa katika yote niliyoeleza katika historia hii ulichokiona kikubwa kwako ni kuuliza kwa nini Abdul hakujitoa katika uchaguzi ule.

Hili swali lishaulizwa hapa mara kadhaa na nimelijibu.
Ulikuwa unaijua historia hii?

Historia ya African Association (AA) 1929 hadi kufikia TANU 1954 ina uhusiano mkubwa sana na ukoo wa Sykes kama waasisi na wafadhili wake.

Abdul angejitoa uchaguzi ule dhidi ya Nyerere wanachama wangehisi kachukia na kasusa na hii ingevuruga murua wa TAA na pengine kukiridusha chama nyuma sana.

Abdul alikuwa anaungwa mkono na wanachama wengi kutoka 1950 alipoingia katika uongozi na Dr. Vedasto Kyaruzi.

Kujitoa katika uongozi katika kipindi kile cha uchaguzi isingekuwa kitu cha busara.
Nyerere pale anaingia katika uchaguzi hakuwa anajulikana Dar es Salaam.

Judith Listowel kakielez kisa hiki vizuri sana katika kitabu chake, ''The Making of Tanganyika, '' (1965).

Sikiliza maneno ya Hamza Mwapachu kwa Abdul Sykes kuhusu uchaguzi uliokuwa mbele yao na umuhimu kwa kuunda TANU katika uchaguzi ujao wa 1954.

Kwa nini umeshughulishwa na kujitoa kwa Abdul na siyo imekuwaje historia ya TANU imeandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni Abdul Sykes na Hamza Mwapachu hawakutajwa katika kitabu hicho?

Au huamini kuwa haya niliyoeleza ndiyo historia ya kweli ya TANU?
Hivyo vitabu hapo chini kuhusu historia ya TANU vinatoka kwenye chanzo kimoja.

Kitabu cha Abubakar Ulotu kimenakiliwa kutoka mswada uliokuwa katika maktaba ya TANU ulioandikwa na Dr. Wilbard Klerruu 1962/63.

Kitabu Chuo Cha Kivukoni hakiko tofauti sana na kitabu cha Ulotu.

Vitabu vyote hivi viwili vinatokana na mradi wa TANU wa kuandika historia yake ambao mwandishi mkuu alikuwa Abdul Sykes akisaidiwa na Dr. Kleruu lakini kwa bahati mbaya Abdul akajitoa katika kazi hii.

Dr. Klerruu akakamilisha mswada lakini haukukuchapwa.
Kitabu cha Abubakar Ulotu inaaminika unatokana na mswada huu.

View attachment 2218707
Nimekuelewa, TAA haikuwa chama cha siasa, bali ulikuwa ni muungano wa wafanyakazi, na waafrika kutetea haki zao kwa serikali,...Nyerere alipoingia madarakani, aliibadili TAA kutoka chama cha wanaharakati wa kiafrika ,mpaka kuwa chama cha siasa cha kupigania Uhuru. Historia ya TANU inaanzia pale Nyerere alipoingia madarakani...Nyerere ndio aliekuwa mpangaji wa mipango yote ya chama.....Wengine walikuwa wasindikizaji tu
 
KIKAO CHA KUUNDA TANU NYUMBANI KWA HAMZA KIBWANA MWAPACHU NANSIO, UKEREWE 1953
Ilikuwa miezi ya mwanzo ya mwaka wa 1953 kabla ya kufika April, 1953.

Abdul Sykes Act. President na Secretary wa TAA akifuatana na Ali Mwinyi Tambwe Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) walikwenda Nansio, Ukerewe nyumbani kwa Hamza Mwapachu.

Abdul Sykes alikuwa anataka kupata kauli ya mwiisho ya Hamza Mwapachu kuhusu Julius Nyerere kuingizwa katika uongozi wa juu wa TAA kwenye uchaguzi wa viongozi wa TAA uliokuwa ufanyike mwezi April.

Uchaguzi ulifanyika kama walivyokubaliana watu hawa watatu na TAA ikawa chini ya uongozi wa Julius Kambarage Nyerere kama ilivyo hapo chini:

J.K. Nyerere, President; Abdulwahid Sykes, Vice-President; J.P. Kasella Bantu, General Secretary; Alexander M. Tobias, Waziri Dossa Aziz, Joint Minuting Secretary; John Rupia, Treasurer, Ally K. Sykes Assistant Treasurer.

Committee members: Dr. Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo, Patrick Aoko.

(Tanganyika Standard 19 June 1953)
Angalia na sikiliza historia hii hapo chini:

Je Dully Sykes ana undugu na Abdul Sykes?
 
Nimekuelewa, TAA haikuwa chama cha siasa, bali ulikuwa ni muungano wa wafanyakazi, na waafrika kutetea haki zao kwa serikali,...Nyerere alipoingia madarakani, aliibadili TAA kutoka chama cha wanaharakati wa kiafrika ,mpaka kuwa chama cha siasa cha kupigania Uhuru. Historia ya TANU inaanzia pale Nyerere alipoingia madarakani...Nyerere ndio aliekuwa mpangaji wa mipango yote ya chama.....Wengine walikuwa wasindikizaji tu
Vito...
Bahati mbaya wewe hujui historia ya Nyerere wala historia ya TAA na TANU.

Bora ungeniuliza maswali ya mtu asiyejua sasa kapata mtu anaejua anataka na yeye ajue ili atoke kwenye ujinga.

Umekuwa kama Chuo Cha CCM Kivukoni walioandika historia ya TANU.

Hayo maneno uliyoandika umeyatoa wapi?

Umeona rejea ya viongozi wa TAA niliyoweka kutoka Tanganyika Standard la 19th June, 1953.

Kwa nini huniulizi maswali yenye faida na wewe uwe mjuzi?

Kwa nini huniulizi wapi nimepata nyaraka kama ile?

Badala yake unakuja na vichekesho kuwa Nyerere kafanya hivi Nyerere kafanya vile.

Sasa nikikuletea ushahidi kuwa hayo yalifanyika toka 1950 na Nyerere alikuwa hajafika TAA HQ New Street utasemaje?

Mimi nimenufaika sana kwa kukubali ujinga nikajifunza kwa wenye kujua.
 
lete katiba ya TAA na katiba ya TANU tuzilinganishe kama zina maudhui sawa.
 
Huu uchaguzi ,Nyerere alimshinda Abdul Sykes...... Abdul sijui kwa nini aliamua kushindana na Nyerere, bora angejitoa tu, hakutumia busara.
Naona mzee Saidi anajitahidi sana kutaka kuiandika upya history kwa kupotosha. Anataka kuonesha kwamba Nyerere hakupata uongozi kwa uwezo wake bali kwa kupewa kama hisani na wazee wa kiislam.
 
Back
Top Bottom