Kikao cha kukutana na Kikwete Pretoria, chaahairishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikao cha kukutana na Kikwete Pretoria, chaahairishwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by AirTanzania, Jul 18, 2011.

 1. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Kulitakiwa kuwa na Kikao Cha Mh Kikwete kukutana na Watanzania waishio South Africa. Mkutano ulitakiwa kufanyika Sheraton Hotel, Pretoria saa 12 za Jioni. Nimesikitika sana kuhairishwa huo mkutano, ilikuwa nafasi yangu ya kuuliza maswali yalio moyoni mwangu kuhusu Taifa.
   
 2. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Vipi air Tanzania imebakia na ndege ngapi? Ilo swali naomba uniulizea kikao kikifanyika!
   
 3. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,157
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Naomba mkianza kikao kama kuna uwezekano muulize atajiuzuru lini kama hana mpango huu basi muulize atakatisha na kuacha safari za nje lini, kama hana mpango pia basi mwambie akirudi tz apumzike angalau hata siku mbili tu tujue uwepo wake
   
 4. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Inasemekana kuwa amechelewa kuingia, wengine wanasema kuwa ameenda kwenye Birthday Party ya Mendela ya kutimiza 93. Mpaka sasa hivi sina habari ya uhakika.
  Kwa wanohesabu Safari zake watuambie hi ni No. ngapi? Kabla ua Kurudi na kwenda Mtwara kwenye Sikukuu ya Mashujaa 25 July 2011
   
 5. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  JK mwanzoni ndiyo alikuwa anawataka Watanzania wa nje siyo sasa Nchi iko taabani.Anaweza kuongea na ma CCM wenzake wa UK lakini si zaidi ya hapo maana watu wana masawali mazito na yeye ni mwepesi hajibu swali hutoa hadithi .
   
 6. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Hilo lilikuwa mojawapo ya Maswali yangu, Subiria utapata Jibu pindi nitakapo muuliza
   
 7. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #7
  Jul 18, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Jitahidi sana kutumia muda huo wa kuhairishwa kwa huo mkutano kwako wewe kujipanga vema na maswali yako kwa huyo mheshimiwa na utupe marejeo juu ya zoezi zima huko bondeni.

   
 8. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #8
  Jul 18, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kama mkifanya nae kikao naomba umuulize safari zake zinatija gani kwa taifa huku maliasili za nchi zikiuzwa hovyo.leo bungeni mbunge kasema uranium inachimbwa huko tunduru na wamarekaji huku kukiwa hakuna sheria wa amri iliyopitishwa katika nchi hii juu ya uchimbaji wa uranium.
   
 9. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #9
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Mi naona amekimbia Swali ndio maana ameingia Mitini, Eti kachelewa Ndege ghaaaa, Ndege gani? Wakati anaishi humo kwenye Ndege, wala haiingii akilini kwamba amechelewa ndege. Haya ndio aliyoyasema Pinda kuwa Watanzania wana excuses na kutoa sababu nyingi, sasa hapa sijui tuyaingize maneno ya Pinda kuwa pia ni excuses ya Kikwete kuingia Mitini kwa kusema amechelewa ndege
   
 10. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #10
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Uwezo Tunao, Nilikuwa na Maswali zaidi ya 10 kwa jinsi nilivyoshikwa na hasira kuona nchi ipo giza yeye wala hajali
   
 11. Prof Gamba

  Prof Gamba JF-Expert Member

  #11
  Jul 18, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 390
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Nasikia ni safari yake ya 346 tangu aanze urais mwaka 2005, ni karibia mwaka mmoja sasa toka awe rais anakuwa safarini, hii ni balaa.
   
 12. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #12
  Jul 18, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hii itakuwa mara ya 14 au 15 kama si kosei, tangu achaguliwe october 2011. Hajawahi kwenda kushukuru wapiga kura hata mkoa mmoja.
   
 13. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #13
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  RAIS YUKO KWENYE PARTY BIRTHDAY MANDELA MUDA HUU Namwona hapa anagonga cheers ,mama salma naona anatabasamu na mandela hapa na amempiga busu .ooh my God hajui huku ngeleja leo kaenda chooni mara ya 39
   
 14. data

  data JF-Expert Member

  #14
  Jul 18, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,795
  Likes Received: 6,573
  Trophy Points: 280
  uliza utajibiwa hapa.. juu ya nin .. umeme au?.. kma ni hilo taifa lipo gizan
   
 15. data

  data JF-Expert Member

  #15
  Jul 18, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,795
  Likes Received: 6,573
  Trophy Points: 280
  aisee..............
   
 16. data

  data JF-Expert Member

  #16
  Jul 18, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,795
  Likes Received: 6,573
  Trophy Points: 280
  rais wangu kapendeza... anaonekana TBC.. saiv
   
 17. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #17
  Jul 18, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  KASHFA YA RAIS KIKWETE KUWAACHA SOLEMBA WATANZANIA HOTELINI SHERATON AFRIKA KUSINI, MRATIBU WA SAFARI ZA RAIS AJIUZULU MARA MOJA!!!!!!!!!!

  Kama ni kweli Rais Kikwete kashindwa kukutana na sehemu ya waajiri wake (Watanzania Muishio Bondeni) na kuwapeni ufafanuzi wa kina juu ya safari yake Afrika Kusini pamoja na yale yanayojiri huku nyumbani kwa madai kwamba ANACHELEWA NDEGE basi ni
  SHARTI MPANGA RATIBA WA SAFARI ZA RAIS pamoja na programmes zake Ughaibuni AKAJIUZULU MARA MOJA.

  Rais Kikwete hafanyii Mtanzania yeyote HISANI kwa kukutana nao na kumhoji maswali yaliomo moyoni bali ni WAJIBU WAKE KIKATIBA kwetu kutoa taarifa ya kina pindi awatembeleapo huko ng'ambo na mara tu anaporejea hapa nyumbani pia ni sharti atupe mchanganuo wa kila safari aliyoifanya nje ya nchi bila kubembelezwa.

  Wajibu huo kwake ni kutokana na ukweli kwamba tunagharamia kila kitu katika safari zake kwa kutumia KODI ZETU.

  Hivyo, katika hili, kitendo cha Rais kuwaacha SOLEMBA Watanzania kwenye baraza za hoteli ya kifahari Afrika Kusini (Sheraton Hotel) eti kwa madai kwamba anachelewa ndege; lazima mtu awajibishwa mara moja kwenye ikulu yetu Dar es Salaam na Balozi wetu nchini humo atuambie alisaidia vipi kuhakikisha kwamba Watanzania wenzetu hawaonekani kama WADOEAJI hotelini hapo na kudhalilika kiasi hicho.


   
 18. WILLY GAMBA

  WILLY GAMBA JF-Expert Member

  #18
  Jul 18, 2011
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 210
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Aliyeweza kumshawishi {aliye mtapeli} JK asije kwenye mkutano ni genius kwa kuziokoa pesa za kukodi Sheratoni anastahili nishani ya taifa..
   
 19. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #19
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Mbaya zaidi Kuna watu wameenda na kuambiwa kuwa hakuna Mkutano, watu wameacha shughuli zao na bure
   
 20. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #20
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hebu tusaidie kumuuliza umeme wa megawati utatufikia lini nchini?? Kila siku tunasikia hesabu za megawati umeme hatuuoni. Pia utusaidie kumuuliza kwanini shilingi yetu sasa hivi inaenda kama jahazi halina nahodha? Mwisho kabisa atuambie lini atapunguza safari zake na kukaa nchini kushughulikia matatizo ya nchini kwake?
   
Loading...