Kikao cha kamati ya Bunge ya maendeleo na jamii na wadau wa sanaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikao cha kamati ya Bunge ya maendeleo na jamii na wadau wa sanaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msanii, Oct 26, 2011.

 1. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Wakuu,
  Leo wadau wa sanaa tyumestukizwa kwa kuitwa kwenye kikao baina ya Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii na Wadau wa sanaa nchini....
  Mwenyeji wetu ni Naibu Waziri wa Utamaduni, Habari na Michezo...

  Venue ni BASATA (Baraza la Sanaa la Taifa)

  Kikao ndo kimeanza....`

  Mada kuu ni masuala yanayohusu HAKIMILIKI NA HAKISHIRIKI...
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Wakuu, kwa kuwa sisi wadau tutashiriki moja kwa moja,
  nakaribisha maswali ama maoni ambayo tunaweza kuyatoa kwa hii kamati...

  Mimi nimejikita na masuala ya hakimiliki na hakishiriki, kuna makombora ya ufisadi ndani ya COSOTA....

  Wajumbe wa Kamati ya Bunge wamebadilisha ratiba kwamba wadau TUFUNGUKE kwanza ndipo watendaji wa serikali wajieleze mwishoni...
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mwenyekiti; Jenista Mhagama ndo anafungua kikao rasmi,
  anaelezea jukumu na maeneo ambayo Kamati yake inayagusa. Na kusudio lao la kikao cha leo...
   
 4. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  .... wasanii wanajua vipaumbele vya tasnia yao,
  ..... Wabunge wasingeweza kupokea maoni kwa ukamilifu iwapo hakungekuwa na mawasiliano ya moja kwa moja kutoka kwa wadau wenyewe...
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  ...tunataka kusikia wadau wanasema nini kuhusu maendeleo ya sanaa hasa namna inavyoweza kuinua pato la nchi...
   
 6. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  ...kuna matatizo...
  ..katika suala la hakimiliki na hakishiriki kuna tatizo ambalo tumeliona awali na tungetaka kusikia wadau wanasemaje ktk hilo suala...

  yote tutakayozungumza hapa ni kwajili ya faida ya Taifa letu
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Leo ndo tumegundua kwamba wasanii wanaweza kuitikia wito hata kwa muda mfupi maana taarifa ya kikao hiki imewajia ghafla lakini tumefarijika na kujitokeza kwenu hapa...
   
 8. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  ...Nimefungua kikao rasmi...
  Ninawakaribisha Waheshimiwa Wabunge kujitambulisha kabla hatujaendelea....
   
 9. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  hao wajumbe knye msururu wako wangapi allowance zao zikoje output na input vinashabiana? isijekuwa wanatafuta tu posho
   
 10. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  1. Jenister Mhagama - Peramiho- Mwenyekiti wa kamati na Bunge
  2. Mch Asunta Mshama- Nkenge
  3. Hamadi Ali Hamadi - Magogoni Unguja
  4. Livingston Lusinde - Mtera
  5. Asha m. Omari - Pemba
  6. Ramadhani Salehe
  7. Salum Baruiani - Dodoma
  8. Agnes Ndololo Kigoma
  9. Rebeka Mngodo - Aryusha
  10. J. Mbilinyi Mbeya mjini
  11. Kapten Komba- Mbinga
  12. Moza Abeid - Dodoma -maalum
  13. Hosiana John- Katibu wa kamati
  14. Tabu Omari - Usalama - Bunge

  Wabunge 5 wana udhuru....
   
 11. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Katibu mtendaji wa Basata, anafunguka sasa...
   
 12. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Anaitwa Gonche Materego..
  ....Nimefurahishwa sana kwa ujio huu mkubwa wa leo. Kwetu ni mafanikio na way forward
   
 13. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  BASATA ni matokeo ya kuunganishwa kwa mabaraza mawili hapo mwaka 19841. Baraza la sanaa za ufundi na Baraza la sanaa za Muziki
   
 14. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Wapo wa kutosha ukiangalia orodha hapo juu.Ila kuna mmoja hakusikika vyema alipokuwa anajitambulisha... ntaleta jina bdae kidogo
   
 15. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #15
  Oct 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  ...Baraza huandaa na kuratibu mafunzo ya sanaa ili kuboresha uzalishaji wa sanaa bora zaidi kwa masoko ya ndani na nje..
   
 16. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #16
  Oct 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  ...pamoja na kufanya hayo, lakini pia tunaandaa kanuni na sheria ndogo za kusimamia masuala ya sanaa nchini..
   
 17. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  ...Kumekuwa na mtazamo hasi kwamba sanaa ni kitu kisicho na umuhimu, na wasanii ni kama wanafanya kazi ya mzaha lakini tunajitahidi kuondoa mtazamo huo kwa kuwaelimisha wadau wa sanaa na wasanii kujitambua, kuthamini na kuboresha mtazamo chanya wa sanaa yetu nchini hususani kutafuta masoko ndani na nje...
   
 18. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #18
  Oct 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  ..Eneo lingine napenda kuongelea kitisho cha uharamia wa kazi za sanaa nchini...
   
 19. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #19
  Oct 26, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Nashukuru kwa taarifa hii, mimi pia ni mdau muhimu katika sanaa na nayajua mengi kuhusiana na Cosota
  na linapokuja suala la Cosota huwa nachoka kabisa kwa kuwa binafsi wala sielewi wanafanya nini kwa kuwa
  hadi sasa kuna mkanganyiko mkubwa ndani ya Cosota yenyewe na taasisisi zingine za serikali. Ieleweke kuwa
  Cosota ni mali ya wanachama na wala si taasisi ya Serikali. Na Mtendaji wa Cosota (Yustus Mkinga) alikuwa
  mwajiriwa wa mkataba maalum na alipewa kipindi cha miezi sita tu ili kuthibitishwa, lakini tangu aingie madarakani
  katikati ya 2007 alipaswa kupewa uthibitisho na bodi ya Cosota lakini kwa kutokuwepo bodi amekuwa akitumia
  nafasi hii kukwepa kuhojiwa na kutathminiwa na Bodi iliyomweka.

  Cosota hiyohiyo inayotakiwa kulinda haki za wasanii iko chini ya watendaji wa wizara tofauti na ya wasanii,
  mbaya zaidi watendaji wake hawana utaalamu wala uzoefu katika tasnia ya sanaa. Nadhani sasa ni muda muafaka
  wa mamlaka hii inayolinda haki za wasanii na kazi zao iwe chini ya BASATA ambayo ndiyo inayolea wasanii na
  wadau wa sanaa.

  Ili kuifanya Cosota iwajibike na kumaliza tatizo la wizi wa kazi za sanaa wasanii wanapaswa watambue ukweli
  uliopo kuhusu Cosota, kwani tatizo la wizi wa kazi za sanaa lina sura nyingi na lilishafanyiwa kazi kuanzia
  mwaka 2001 na National Anti Piracy Committee, taratibu (regulations) za kutekeleza hili zilishapitishwa tangu
  mwaka 2006 na aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara wakati huo, Nazir Karamagi.

  Lakini tangu Karamagi aidhinishe taratibu hizo, kumekuwepo tatizo la serikali kutotoa fungu la fedha la kuwezesha
  utekelezaji wa kazi hiyo, na jambo hilo halijatekelezwa hadi leo. Waziri aliyefuatia (Mary Nagu) baada ya Karamagi
  akakalia uamuzi wa kuchagua Mwenyekiti wa Bodi ya Cosota kwa sababu fulanifulani.

  Waziri huyo ndiye chanzo cha yote kwani aliamua kutoikubali bodi iliyochaguliwa na wadau katika mkutano wa
  mwisho uliofanyika mwanzoni mwa 2007, na wala hakuiruhusu bodi iliyopita kuendelea mpaka utatuzi upatikane
  na aliamua kukaa kimya ili achomeke watu wake katika bodi nzima ingawa ana uwezo kisheria kuteua wajumbe
  watatu anaowataka kuwepo kwenye bodi yenye jumla ya wajumbe 15.

  Siku chache kabla ya Bunge la Bajeti la mwaka huo, waziri akapeleka majina ili yachapishwe kwenye gazeti la Serikali.
  Cha kushangaza majina hayo yalikuwa tofauti na yale ambayo wanachama wa Cosota walichagua katika Mkutano
  wao Mkuu, aliingiza chaguo lake ambalo haliwakilishi wadau kamili wa Cosota kwa kufuata uchangiaji wao katika Cosota.

  Tangu wakati huo Bodi ya Cosota haijawahi kukukutana na haijulikani hatima yake ni nini, ambapo pamoja na kazi
  nyingine uhakiki wa bajeti na mahesabu ya taasisi hupitishwa na bodi kwanza ndipo huenda serikalini kwa hatua
  nyinginezo, kutokana na kutokuwepo bodi ambayo ndiyo muajiri wa 'staff' wa cosota kwa mujibu wa sheria
  inayoiunda ikiwa ni pamoja na Mtendaji, imepelekea mtendaji aliyepo kufanya usaili na uajiri kwa matakwa yake binafsi.  Kwa kweli hii ni hatari sana kwa sanaa yetu...
   
 20. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #20
  Oct 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  ..hatua mbalimbali zimechukuliwa ikiwemo
  1. kuboresha sheria zilizopo zinazohusu masuala hayo.
  2. kutoa elimu kwa wadau waweze kuheshimu na kutekeleza sheria hii.
  3. Kusimamia kwa ukamilifu kuhusu sanaa za JADI ambazo kwa mujibu wa sheria BASATA ndiye msimamizi mkuu
   
Loading...