Kikao cha Dkt. John Magufuli, Tundu Lissu, Dkt. Hussein Mwinyi na Maalim Seif Sharif Hamad ni muhimu kabla ya utangazaji matokeo

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Oct 7, 2020
1,382
1,246
WanaJF,Salaam!

Ninapendekeza kifanyike kikao cha haraka kitakachowakutanisha wagombea wenye nguvu kwa upande wa Zanzibar na Tanganyika ikiwezekana hata wasiokuwa na nguvu wahusishwe.

Kikao hicho kiwe na uwezo wa kuwajenga kisaikolojia, kuwaangaliza na kuwataka kuheshimu katiba ya nchi, utashi wa wapigakura, na utayari wa kukubali matokeo ya uchaguzi. Aidha, kikao hicho kwa kiasi kikubwa kinaweza kuratibiwa na uongozi wa Kanisa la Waadiventista Wasabato kwa kuwa huwa hawana upande wowote - lakini pia balozi zetu na asasi za kiraia zaweza kushirikishwa.

Kwa mtazamo wangu sioni haja kabisa ya mabomu kutumika katika uchaguzi na utangazaji matokeo, sioni haja ya risasi kutumika, sioni haja ya tume kusafisha wagombea kwa dodoki, sioni haja ya maandamano, wala sioni haja ya wagombea kuhasimiana. Naona haja ya mgombea kukiri kushindwa na kupongeza aliyeshinda kihalali.

Tanzania ni moja na hatuwezi kupata Tanzania nyingine ikiwa itavurugika, Zanzibar ni moja na hatuwezi kupata nyingine ikiwa itavurugika.

Nawatakia uchaguzi mwema 2020
Msakila Mussa Kabende
Mwanaccm
Kigoma - Tanzania
25 Oktoba, 2020
 
"Kwa mtazamo wangu sioni haja kabisa ya mabomu kutumika katika uchaguzi na utangazaji matokeo, sioni haja ya risasi kutumika, sioni haja ya tume kusafisha wagombea kwa dodoki, sioni haja ya maandamano, wala sioni haja ya wagombea kuhasimiana. Naona haja ya mgombea kukiri kushindwa na kupongeza aliyeshinda kihalali".

CCM na Magufuli bila mabomu, wizi,ubabe,vifo na dhuluma haiwezi kushinda uchaguzi.
 
Mkuu Msakila, naelewa hofu yako! Labda una watoto wadogo kama mimi, labda Una umri wa kuwa settled, Una kazi yako, umewekeza, kama mimi! Kama ndivyo, madhara yakitokea, Sisi ni wahanga zaidi! Hata Mimi namuomba Mungu, kama amani ikishindikana, basi utulivu uendelee, tukeep status quo!

Tatizo ni kwamba kila ukombozi, kuna damu huwa inamwagika, na inaonekana saa ya ukombozi imekaribia! Mungu atuvushe tu, lakini kuna watakaopoteza ili wengine wapate ukombozi, hope si Wewe wala mimi!
 
Wanadhani watabaki madarakani kwa njia haramu za kutumia mtutu wa bunduki. Wasipotia akili kichwani kwa ajili ya maslahi makubwa ya Taifa basi Nchi itawaka moto. Watu wamechoka huwa na udhalimu wa kutisha.
 
Nimesoma bandiko la Pascal Mayalla na nimetazama kibwagizo cha wanaccm leo kwenye mkutano wa Dr. Mwinyi uliohudhuriwa na Rais mstaafu Dr. Kikwete.

Kibwagizo chao kulikuwa hivi:- "Mapinduzi tutayalinda. Watakaonuna na wanune potelea pwete"

Nikagundua kuwa CCM haiwazi na haiamini katika kuondoka madarakani hata kama itashindwa.
 
Nyie ndio mnakosa Hekima
Ni ukosefu huo wa Busara unaliangamiza hili Bara la Afrika.Kuna shida gani hawa watu wote wana wafuasi wengi tu wakikaa wakajadili viziri maisha baada ya uchaguzi??
Mtu anayekuambia asiposhinda patachimbika huyo hata wafuasi wake wenye busara ni wachache mno, asilimia kubwa ni wahuni tu. Huyo akae mbali kabisa hatutaki kumuona. Tena usitukumbushe tukaanza kumuimbia nyimbo tulizomwimbia Oscar Kambona (Mungu amrehemu) miaka ile.
 
Nimesoma bandiko la Pascal Mayalla na nimetazama kibwagizo cha wanaccm leo kwenye mkutano wa Dr. Mwinyi uliohudhuriwa na rais mstaafu Dr. Kikwete.

Kibwagizo chao kulikuwa hivi:- "Mapinduzi tutayalimda. Watakaonuna na wanune potelea pwete"

Nikagundua kuwa ccm haiwazi, na haiamini ktk kuondoka madarakani hata kama itashindwa.
Mpaka huku mtaani yani hawaamini ila ndio watajua nini maana sapulaizi saiz
 
Mpaka huku mtaani yani hawaamini ila ndio watajua nini maana sapulaizi saiz.
 
hakuna busara hapo.Mtu anayekuambia asiposhinda patachimbika huyo hata wafuasi wake wenye busara ni wachache mno,asilimia kubwa ni wahuni tu.Huyo akae mbali kabisa hatutaki kumuona.Tena usitukumbushe tukaanza kumwimbia nyimbo tulizomwimbia Oscar kambona (Mungu amrehemu)miaka ile.

Wahuni sio Watanzania? Wewe unaetukana na hao unaita wahuni mna tofauti gani?
 
Nyie ndio mnakosa Hekima
Ni ukosefu huo wa Busara unaliangamiza hili Bara la Afrika.Kuna shida gani hawa watu wote wana wafuasi wengi tu wakikaa wakajadili viziri maisha baada ya uchaguzi??
Wawakamate kwanza wasiojulikana
 
Nimesoma bandiko la Pascal Mayalla na nimetazama kibwagizo cha wanaccm leo kwenye mkutano wa Dr. Mwinyi uliohudhuriwa na rais mstaafu Dr. Kikwete.

Kibwagizo chao kulikuwa hivi:- "Mapinduzi tutayalimda. Watakaonuna na wanune potelea pwete"

Nikagundua kuwa ccm haiwazi, na haiamini ktk kuondoka madarakani hata kama itashindwa.
CCM kamwe haiwezi kushindwa Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!.
P.
 
Kikao kingekuwa na maana kama wagombea wangekuwa wanajua kuheshimu wenzao, yaani wakawa wanagombea kwa sera tu. Iwapo una mgombea ambaye sera yake ni kumtukana na kumshambulia matusi ya hovyo mgombea mwenzake unategemea wakutane kweli?
 
Mpaka huku mtaani yani hawaamini ila ndio watajua nini maana sapulaizi saiz
Mitaa gani?
Nashindwa kutoa takwimu za ukubalika wa wagombea wa Urais kwa JMT sababu sina kibali lakini tayari uelekeo wa nani anashinda uko wazi sana.

Himizeni kikao kufanyike kwa kuwa tunajenga nchi moja
 
Back
Top Bottom