Kikao cha CCM zanzibar ilikuwa hapatoshi

GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,432
3,011
Kikao kilicho fanyika zanzibar hapo kisiwandui, kwa habari tulizo zipata ni kwamba hali ya wanaccm haikuwa nzuri, agenda ilikuwa hasa ni kufikishwa kwa ujumbe kutoka kwa Magufuli.

Katika kikao hicho kilihudhuriwa na Rais wa Zanzibar Mohamed Shein na Samia Suluhu makamu wa rais wa Jamhuri ya muungano, baada ya kuongea yote ambayo ccm ipo katika utelezaji wa chama hicho, Samia Suluhu alitumbua jipu na kuwambia wanaccm kuwa ana ujumbe tena wa maandishi kutoka kwa Rais Magufuli kuwa alie shinda katika uchaguzi lazima atangazwe, hapo ndipo ilipo tokea mtafaruku, wako ccm walio tamka kuwa lazima atafutwe Jecha atangaze siku ya uchaguzi.

Wengine kutoka katika vikao wakiwa wamenuna, na wengine kuwaita waandishi wa habari na kutoa kauli ya kujitaarisha na uchaguzi.

Shein mwenyewe hakutamka kwamba siku ya uchaguzi itatangazwa, zaidi ya mahafidhina wa Zanzibar.

Tunasubiri na muda sio mrefu kutangazwa kwa mshindi wa uchaguzi
 
Last edited by a moderator:
Kikao kilicho fanyika zanzibar hapo kisiwandui, kwa habari tulizo zipata ni kwamba hali ya wanaccm haikuwa nzuri, agenda ilikuwa hasa ni kufikishwa kwa ujumbe kutoka kwa Magufuli.

Katika kikao hicho kilihudhuriwa alie kuwa Rais wa Zanzibar Mohamed Shein na Samia Suluhu makamu wa rais wa Jamhuri ya muungano, baada ya kuongea yote ambayo ccm ipo katika utelezaji wa chama hicho, Samia Suluhu alitumbua jipu na kuwambia wanaccm kuwa ana ujumbe tena wa maandishi kutoka kwa Rais Magufuli kuwa alie shinda katika uchaguzi lazima atangazwe, hapo ndipo ilipo tokea mtafaruku, wako ccm walio tamka kuwa lazima atafutwe Jecha atangaze siku ya uchaguzi.

Wengine kutoka katika vikao wakiwa wamenuna, na wengine kuwaita waandishi wa habari na kutoa kauli ya kujitaarisha na uchaguzi.

Shein mwenyewe hakutamka kwamba siku ya uchaguzi itatangazwa, zaidi ya mahafidhina wa Zanzibar.

Tunasubiri na muda sio mrefu kutangazwa kwa mshindi wa uchaguzi

"Aliyekuwa raisi wa Zanzibar, Dr Shein..." Very clever!
 
Zenji,,,waliambiwa na JK wafanye kampen za kitanda kwa kitanda shuka kwa shuka inaonekana hawakutekeleza
 
Kuna wana ccm ambao ni ma hardliners hasa kutoka unguja ndo kikwazo, btw nani aliye mwamuru Jecha kubatilisha sehemu ya uchaguzi ule?, siamini kama ali jiamulia yeye mwenyewe......
 
Nilijua tu ule mkutano na waandishi wa habari ulikuwa kama haukuwa na baraka za viongozi wakuu.
"tunakubaliana na mazungumzo yanayoendelea lakini wakati huo tunawataka wanaCCM wajiandae na uchaguzi wa marudio." statement kama hii haikuniingia akilini.
 
Umeona mkuu, ni wanafiki sana na uhafidhuna
 
Back
Top Bottom