kIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI LUDEWA CHAVUNJIKA

Jun 9, 2011
16
7
Madiwani wa Halmadhauri ya wilaya ya Ludewa mkoa mpya wa Njombe (Iringa) leo wamegoma kuendelea na kikao cha tathimini ya robo mwaka juu ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika Halmashauri hiyo baada ya wakuu wa Idara kushindwa kutekeleza maagizo mbali mbali ambayo waliagiza katika vikao vilivyopita .

Katika kikao hicho kilichoongozwa na mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Matei Kongo kilikuwa kikifanyika ktk ukumbi wa HALMASHAURI hiyo kuanza majira ya saa 8 za mchana baada ya kumalizika kwa semina ya mkurabita.

Madiwani hao zaidi ya 25 wote walipiga Kura za ndiyo kuafiki kusitishwa kwa kikao hicho ili kupisha wakuu wa Idara kutekeleza maagizo yaliyotolewa siku za mwanzo bila kutekelezwa.
 

Mbugi

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,489
256
Madiwani wamekuja juu kwani wanajua kichapo watakachopata kutoka kwa wananchi 2015 wakati watendaji wao wakiendelea kupeta kwa kwenda mbele
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom