Kijo Bisimba, Ananilea Nkya, Lissu na Fatma Karume taasisi mlizoongoza zinakufa mkiangalia?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
330
1,000
Kwa Nini mtu aondoke madarakani taasisi inyong'onyee? TAMWa, TLS na taasisi nyingine zinazitetea haki Tanzania zinakufa taratibu kwa kukosa watu wanaoweza kuyaona matatizo ya wananchi kwa upana nakuyatatua.

Kama taasisi hizi za haki za binadamu zimebaki kulipana mishahara nakukaa ofisini bila kutekeleza majukumu yake kwanini wafadhili wasisitishe misaada dhidi yao kwa sababu wanatumia fedha hizo kinyume na malengo?

Wakina Kijobi Simba, Nkya na Karume waliwezaje kutetea wananchi adharani mara tu uvunjifu wa haki unapotendeka? Kwanini viongozi wa Sasa wanashindwa? Mawakili wanaonewa TLS wapo kimya, wananchi wananyanyashwa Wapo kimya, wanasubiri siku wanyanyaswe wao viongozi?
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
4,398
2,000
Hizo taasisi hazifi, na hazitakufa kamwe, siku zote giza haliwezi kuishinda nuru, hao TLS ndio wamekubali kutumika, kinachotokea sasa kwa hizo taasisi nyingine ni kukosa uwanja mpana wa kutekeleza majukumu yao kutokana na aina ya uongozi uliopo nchini.

Nchi inaongozwa kibabe, hizo taasisi za kutetea haki za binadamu zinaitwa "mawakala wa mabeberu" wakati kimsingi wanatimiza majukumu yao kwa kukemea vitendo vya unyanyasaji wanavyofanyiwa raia wa nchi hii.

Kwa serikali iliyopo sasa kuwa mzalendo kwa taifa ni kufumbia macho kila uonevu ataofanyiwa raia wa nchi hii, na kutofuata sheria; ukinyanyuka ukemee unaonekana adui wa taifa, watakutengenezea majina yote ya kipropaganda ili kuhalalisha uhuni wao, na kuwadanganya wajinga wasioijua hali halisi.
 
Magema Jr

JF-Expert Member
Apr 22, 2020
1,299
2,000
Mbona Wanachapa kazi kama kawaida??🤔
Au unataka wapige selfie kila matukio ili ujue bado wapo?
 
kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
7,270
2,000
Kwa Nini mtu aondoke madarakani taasisi inyong'onyee? TAMWa, TLS na taasisi nyingine zinazitetea haki Tanzania zinakufa taratibu kwa kukosa watu wanaoweza kuyaona matatizo ya wananchi kwa upana nakuyatatua.

Kama taasisi hizi za haki za binadamu zimebaki kulipana mishahara nakukaa ofisini bila kutekeleza majukumu yake kwanini wafadhili wasisitishe misaada dhidi yao kwa sababu wanatumia fedha hizo kinyume na malengo? Wakina Kijobi Simba, Nkya na Karume waliwezaje kutetea wananchi adharani mara tu uvunjifu wa haki unapotendeka? Kwanini viongoz wa Sasa wanashindwa? Mawakili wanaonewa TLS wapo kimya, wananchi wananyanyashwa Wapo kimya, wanasubiri siku wanyanyaswe wao viongozi?
Wala taasisi hizo hazijanyong'onyea ila zimepata viongozi wanaojua wajibu wao badala ya kuzitumia taasisi hizo kwa malengo yao binafsi ya kisiasa.

Kwa mfano taasisi kamaTLS ni chama cha kitaaluma kwa wanasheria siasa za vyama sio kazi yake. Lakini kibaraka wa ubeberu tundu lissu alipofanikiwa kua kiongozi tofauti na miaka mingine TLS ikawa kama tawi la chadema kama ilivyo bawacha na bavicha.

Alipokuja kibaraka mwingine wa mabeberu fatma karume mambo yakawa vilevile.

TLS sasa inaelekea imerejea kwenye majukumu yake.
 
Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
330
1,000
Soma taarifa za taasisi hizo za utendaji utagundua

Angalia vilio vya wananchi wanaoonewa ambao hawana wakusemea au kuwakumbusha watawala wamekosea.

Kukemea uovu si ubeberu ni wajibu wa kiongozi

Uvunjifu wa haki za binadamu haujawahi kushughulikiwa kwa watatetezi kukaa ofisi wanapaswa kupanua wigo na kukemea adharani.

Kila kizi na misingi yake, ukimya wa taasisi hizi unaifanya jamii ione hakuna wakuwatetea
 
Shambaboy jogoli

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
1,066
2,000
Kwa Nini mtu aondoke madarakani taasisi inyong'onyee? TAMWa, TLS na taasisi nyingine zinazitetea haki Tanzania zinakufa taratibu kwa kukosa watu wanaoweza kuyaona matatizo ya wananchi kwa upana nakuyatatua.

Kama taasisi hizi za haki za binadamu zimebaki kulipana mishahara nakukaa ofisini bila kutekeleza majukumu yake kwanini wafadhili wasisitishe misaada dhidi yao kwa sababu wanatumia fedha hizo kinyume na malengo? Wakina Kijobi Simba, Nkya na Karume waliwezaje kutetea wananchi adharani mara tu uvunjifu wa haki unapotendeka? Kwanini viongoz wa Sasa wanashindwa? Mawakili wanaonewa TLS wapo kimya, wananchi wananyanyashwa Wapo kimya, wanasubiri siku wanyanyaswe wao viongozi?
Tatizo wabakia uanaharakati wa chadema badala ya kutetea haki za wananchi! Wenyewe wanachojua, haki ni lissu kuwa raisi
 
Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
7,313
2,000
Hizo taasisi zimeshafanywa kuwa kama vyama vya wafanyakazi katika nchi hii ambavyo vinaongozwa aidha na makada wa ccm au vibaraka wao.
 
Statesman

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
23,643
2,000
TLS sio NGO ya maswala ya human rights, ile ni professional Organization.

Lisu anamchango mkubwa Sana wa Kuiharibu TLS.

Baada ya yeye Lisu kuigeuza kijiwe chake Sasa ipo juu ya mawe, huyo mtu kaharibu Chama cha mawakili.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
39,329
2,000
Wala taasisi hizo hazijanyong'onyea ila zimepata viongozi wanaojua wajibu wao badala ya kuzitumia taasisi hizo kwa malengo yao binafsi ya kisiasa.
Kwa mfano taasisi kamaTLS ni chama cha kitaaluma kwa wanasheria siasa za vyama sio kazi yake. Lakini kibaraka wa ubeberu tundu lissu alipofanikiwa kua kiongozi tofauti na miaka mingine TLS ikawa kama tawi la chadema kama ilivyo bawacha na bavicha. Alipokuja kibaraka mwingine wa mabeberu fatma karume mambo yakawa vilevile.
TLS sasa inaelekea imerejea kwenye majukumu yake.

Majukumu ya TLS ni kufumbia macho udhalimu wa serikali kwa mahasimu wake? Unapoona TLS inafanya kazi ili kutoiudhi serikali na sio kutekeleza majukumu yake, basi ujue hapo hakuna taasisi, bali kuna kundi la majoga yanayokula pesa ya wafadhili bure.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
39,329
2,000
Wanafanya kazi vizuri sana ila hawafanyi kwa makelele kama hao uliowataja

Hawafanyi kazi kwa makelele, huku viongozi wa serikali hata wakizindua mradi wa shilingi milioni tano wanaenda na wanahabari ili kuonyesha wanafanya kazi? Juzi DC kudhalilisha watu wazima kwa kuwachapa hata bila kuwapeleka mahakamani, huku taasisi ya wanasheria wanafanya kazi nzuri sana wamejifungia ofisini wanashuhudia kiongozi wa umma akichukua sheria mkononi! Shubamiit.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom