Kijiwe cha mlalahoi: Serikali yapoteza mabilioni kwa ufisadi wa CHANJO FEKI ZA MIFUGO

IsangulaKG

JF-Expert Member
Oct 14, 2010
706
386
Nikiwa katika majukumu yangu ya ujenzi wa Taifa,nikapitia katika kijiwe fulani cha walalahoi. Baada ya kuwasabahi, waungwana ambao awali walionyesha kustushwa na ujio wangu, wakaitikia salamu kama ilivyo ada kwa watanzania. Baada ya kujiaminisha kuwa uwepo wangu mahali pale ni wa kheri si shari, wakaendelea na maongezi yao.

"Nakwambia Serikali yetu imeoza sana, Kitengo cha chanjo za mifugo kimetengeneza maelfu ya chanjo feki...jambo la ajabu ni kwamba virutubisho chanjo viliagizwa kutoka kubwa kumbe vilikuwa vimekaribia muda wa ku-expire" alisema mmoja wa wasemaji aliyeonekana mwongeaji sana.

"Japo la ajabu ni kwamba virutubisho vilipokelewa kuanzia bandarini mpaka TBS wakavipitisha...hivi kweli hawakujua kuwa muda wake umekaribia kuisha au ni miradi ya wakubwa? alihoji mwingine.

"Pengine wataalamu wetu ni feki, ina maana hawakufanya majaribio kabla hawajaanza massive production?" akarukia mwingine

"Yaani nchi hii bwana, virutubisho feki, wataalamu feki, TBS feki...mabilioni ya fedha yamepotea na hakuna aliyewajibishwa" akasema mwingine aliyeonekana kuwa na uchungu sana na kodi anayokatwa kwenye mshahara wake


Kwa ufupi ni kwamba majaribio yalifanyika, virutubisho vikaagizwa Cuba lakini inasemekana vilikuwa vimeisha muda wake au havikuwa na contents sahihi, vikapokelewa na kupitishwa bandarini na wataalamu wa TBS na kitengo cha chanjo kikatengene maelfu ya chanjo ambazo hazifanyi kazi. Haijajulikana kama chanjo hizo zilishaingizwa sokoni na kama zilikuwa 'dead' au 'live' . Kwani kama zilikuwa 'live' zaweza kusababisha madhara makubwa sana kwa mifugo.

Hata hivyo, kwa kuwa mimi si mwandishi wa habari na si mtalaamu wa investigative journalism, sikwenda mbele kufuatilia habari hii katika idara ya mifugo, kitengo cha chanjo za mifugo.
 
Kuna thread niliileta humu may mwaka huu kuhusu hasara niliopata baada ya kuchanja kuku na bado wakafa wote
 
Bahati mbaya habari muhimu kama hizi zitapotezewa kama vile si muhimu
 
Kuna thread niliileta humu may mwaka huu kuhusu hasara niliopata baada ya kuchanja kuku na bado wakafa wote
kuna jamaa alikuwa na kuku 3,000 Layers Mesh, amechanja chanjo zote 4 za mwanzo- ikiwemo hii muhimu sana ya Newcastle (mdondo)

Kuku wale kama mnavyojua wanalishwa miezi 5 ( wiki kama 20) kabla hawajaanza production (kutaga) - ambapo wa hesabu za haraka haraka jamaa alitumia kama 30mil na ushee tangu kuwanunua hadi kuwatunza. kifaranga kimoja ni 2,500

Sasa wiki ya 18 kuku walianza kufa mfululuzo - hadi sasa jamaa kabaki na kuku 100 tu. Upelelezi unasema ni Chanjo ya Newcastle (Mdondo) hakufanya; lakini jamaa alichanja - Familia iko msibani sababu hela alikopa.

CHANJO za mifugo inaweza kuwa janga la taifa lingine.
 
Tayari hili ni janga, inasemekana kiasi kikubwa sana cha chanjo kilikuwa kimeingizwa sokoni
Kuku wale kama mnavyojua wanalishwa miezi 5 ( wiki kama 20) kabla hawajaanza production (kutaga) - ambapo wa hesabu za haraka haraka jamaa alitumia kama 30mil na ushee tangu kuwanunua hadi kuwatunza. kifaranga kimoja ni 2,500Sasa wiki ya 18 kuku walianza kufa mfululuzo - hadi sasa jamaa kabaki na kuku 100 tu. Upelelezi unasema ni Chanjo ya Newcastle (Mdondo) hakufanya; lakini jamaa alichanja - Familia iko msibani sababu hela alikopa.CHANJO za mifugo inaweza kuwa janga la taifa lingine.
 
Back
Top Bottom