nguvumali
JF-Expert Member
- Sep 3, 2009
- 4,923
- 1,325
Leo nikiwa ndani daladala kutoka Mwenge kwenda posta mpya , nikakutana na mabishano kati ya vijana watatu kuhusu chapisho la kijitabu cha Orodha ya Mafisadi Tanzania /The list of Shoddy Degree and Diploma Holders. First Edition...kilichoandikwa na ndugu Kainerugamba Msemakweli.
Baada ya kufika mjini yapata saa mbili hivi ikabidi nikatafuta hako kachapisho na mimi nipate nakala yake maana mjadala wavijana wale uliniacha kinywa wazi.
Sasa pale Posta mpya ilinigharimu zaidi ya saa moja kuweza kukipata kwenye meza ya muuza gazeti maana kila ninapopita naambiwa kimeisha...
Binafsi nimekisoma chote, kinakurasa 39 zenye maelezo ya kina juu ya elimu ya kutia shaka ya ndugu Kamala, Mary Nagu, Lukuvi, Makongoro Mahanga, Diallo, NCHIMBI, n.k
Jamaa amejitahidi kumla jongoo, maana hakuuma maneno.