Kijitabu Cha Orodha ya mafisadi wa Elimu Tanzania chagombewa sokoni


nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined
Sep 3, 2009
Messages
4,891
Likes
198
Points
160
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined Sep 3, 2009
4,891 198 160
Leo nikiwa ndani daladala kutoka Mwenge kwenda posta mpya , nikakutana na mabishano kati ya vijana watatu kuhusu chapisho la kijitabu cha Orodha ya Mafisadi Tanzania /The list of Shoddy Degree and Diploma Holders. First Edition...kilichoandikwa na ndugu Kainerugamba Msemakweli.

Baada ya kufika mjini yapata saa mbili hivi ikabidi nikatafuta hako kachapisho na mimi nipate nakala yake maana mjadala wavijana wale uliniacha kinywa wazi.

Sasa pale Posta mpya ilinigharimu zaidi ya saa moja kuweza kukipata kwenye meza ya muuza gazeti maana kila ninapopita naambiwa kimeisha...

Binafsi nimekisoma chote, kinakurasa 39 zenye maelezo ya kina juu ya elimu ya kutia shaka ya ndugu Kamala, Mary Nagu, Lukuvi, Makongoro Mahanga, Diallo, NCHIMBI, n.k

Jamaa amejitahidi kumla jongoo, maana hakuuma maneno.
 
C

ChiefmTz

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2008
Messages
2,715
Likes
495
Points
180
C

ChiefmTz

JF-Expert Member
Joined Apr 15, 2008
2,715 495 180
Kwa nini usituwekee na sisi tukakisoma hapa jamvini?
 
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined
Sep 3, 2009
Messages
4,891
Likes
198
Points
160
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined Sep 3, 2009
4,891 198 160
ChiefmTzKwa nini usituwekee na sisi tukakisoma hapa jamvini?
okey labda nikifikaa kwenye scanner, maana amewatolea uvivu hao kina Mahanga , sasa kwasababu mwanzoni walimtishia kwenda kwa mahakama sasa wapate nakala halisi ya maelezo kupitia chapisho hili kisha wakamsue Msemakweli kama jeuri ipo
 
Soulbrother

Soulbrother

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2009
Messages
408
Likes
4
Points
35
Soulbrother

Soulbrother

JF-Expert Member
Joined Apr 14, 2009
408 4 35
Vitu kama hivi mkuu unaweka hpa tuwafahamu wazee wenyewe
 
Sikonge

Sikonge

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2008
Messages
11,550
Likes
650
Points
280
Sikonge

Sikonge

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2008
11,550 650 280
na Edward Kinabo (Tanzania Daima)

MWANASHERIA na mwanaharakati wa kupambana na rushwa nchini, Kainerugamba Msemakweli, ameandika kitabu kinachotaja na kuelezea kwa undani orodha ya majina kumi ya mawaziri, wakuu wa mikoa na wabunge, wanaodaiwa kughushi vyeti vya taaluma zao.

Msemakweli akizungumza na Tanzania Daima jana jijini Dar es Salaam, alisema kitabu hicho kinachoitwa “Orodha ya Mafisadi wa Elimu”, kitazinduliwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam ili kutoa fursa kwa umma wa Watanzania na vyombo vya dola kuwajua vizuri viongozi walioghushi vyeti na kuwachukulia hatua zinazostahili.

“Nimeandika kitabu kinachowataja kwa majina na kuwaelezea kwa kina mafisadi wa elimu, ili umma wa Watanzania wazidi kuwafahamu na kushirikiana pamoja katika kuvishinikiza vyombo vya dola kuwachukulia hatua zinazostahili. Kitabu hiki kitazinduliwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam,” alisema Msemakweli.

Alisema kuandikwa kwa kitabu hicho ni mwendelezo wa jitihada zake za kuhakikisha mafisadi wa elimu wanajulikana na kuchukuliwa hatua, hasa baada ya kuwa ameshafanya jitihada nyingine za kuiwasilisha orodha hiyo kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Samuel Sitta na kuitambulisha kwa vyombo vya habari mwezi mmoja uliopita.

Miongoni mwa vigogo waliotajwa katika kitabu hicho, ni wale waliowahi kutajwa kusoma katika vyuo vya elimu ya juu nje ya nchi, ambavyo havitambuliki.

Kitabu hicho ambacho Tanzania Daima kimeiona nakala yake, kimewataja kwa majina vigogo hao na jinsi walivyolidanganya Bunge kwa kupeleka vyeti vya uongo na hatimaye kupata vyeo.

Kabla ya kufikia hatua ya kuandika kitabu hicho, Msemakweli alishamuandikia barua Spika wa Bunge, Sitta, miezi michache iliyopita, akibainisha orodha ya wabunge aliodai kuwa wameghushi vyeti vyao vya shahada na stashahada, na hivyo kuwa wamelidanganya Bunge na kukiuka kiapo chao cha utumishi na uaminifu kwa taasisi hiyo nyeti nchini.

Mwanasheria huyo alisema alimkabidhi Spika Sitta barua mbili zenye orodha ya vigogo hao, moja akiikabidhi Septemba 15 na nyingine Oktoba 16, mwaka huu, zote zikiwa na mihuri ya ofisi ya Bunge.

Aliendelea kutamba kuwa, ana ushahidi wa kutosha kuhusu madai hayo na kumtaka kiongozi yeyote atakayedai kuwa amekashifiwa kwenda mahakamani.

Kwa mujibu wa mwanaharakati huyo, viongozi walioghushi vyeti vya elimu yao, wanapaswa kuchukuliwa hatua ili kurejesha taifa katika maadili yanayotakiwa.

Alitaja adhabu ambazo watuhumiwa hao wanaweza kupata kama wanatiwa hatiani kuwa, ni pamoja na kuhukumiwa kifungo kisichozidi miezi sita au kulipa faini ya sh 1,500,000 au vyote kwa pamoja.

“Kutokana na uchunguzi wa kisayansi nilioufanya, imebainika pasipo shaka kuwa, waheshimiwa wabunge waliotajwa hapo chini, mwaka 2006, walikukabidhi taarifa za uongo na za kughushi kuhusu taaluma zao, kitendo ambacho ni ufisadi wa elimu.

“Kwa mujibu wa utafiti huu ambao nakala wewe unazo, unaonyesha kuwa wabunge hao wana shahada au digrii ambazo hawajawahi kuzisomea wakati wowote katika maisha yao yote na mahali popote duniani, hivyo wamelidanganya Bunge lako, kitendo ambacho ni kinyume na maadili ya ubunge,” ilisema barua hiyo iliyokabidhiwa kwa Sitta.

Aidha, akizungumza na vyombo vya habari wakati huo, alifafanua kuwa mbunge yeyote aliyewasilisha taarifa za uongo juu ya taaluma yake kwa Bunge, amekwenda kinyume na taratibu za Bunge na ibara ya 68 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyofanyiwa mabadiliko, kwani wameapa kuwa waaminifu, kulinda na kuhifadhi katiba na sheria nyinginezo.

Katika kitabu hicho, wametajwa mawaziri watatu, akiwemo waziri mmoja mwanamke kutoka mikoa ya Kanda ya Kaskazini, manaibu waziri watatu wa wizara nyeti nchini, ambao wana hadhi ya udaktari na waziri mmoja anayeongoza wizara muhimu sana nchini. Pia yumo mkuu wa mkoa mmoja ambaye ni mbunge wa jimbo moja kutoka mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Wamo pia wabunge watatu machachari wenye hadhi ya udaktari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Kaskazini.

Mwanasheria huyo ambaye alidai kuwa ushahidi wa kitabu chake hicho unatokana na utafiti aliosema wa kisayansi, alioufanya kwa zaidi ya mwaka mmoja, alisema taifa limeendelea kwenda kombo na kuanguka kimaadili kutokana na kuwa na viongozi wasio waadilifu.

Katika siku za hivi karibu, kumekuwa na mjadala wa kuhoji viwango vya elimu vya baadhi ya watendaji wa serikali, ambapo baadhi yao wamefika hatua ya kulazimishwa waitwe kwa hadhi ya viwango vyao vya elimu wakati hawana sifa hizo.
 
Fidel80

Fidel80

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2008
Messages
21,970
Likes
140
Points
145
Fidel80

Fidel80

JF-Expert Member
Joined May 3, 2008
21,970 140 145
Hata mm natafuta copy yake hiyo kimekuwa gumzo sana mitaani
 
H

Hofstede

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2007
Messages
3,584
Likes
41
Points
0
H

Hofstede

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2007
3,584 41 0
okey labda nikifikaa kwenye scanner, maana amewatolea uvivu hao kina Mahanga , sasa kwasababu mwanzoni walimtishia kwenda kwa mahakama sasa wapate nakala halisi ya maelezo kupitia chapisho hili kisha wakamsue Msemakweli kama jeuri ipo
Unapofanya hivyo zingatia na sheria za haki miliki pia. Kwa nini usimtafute Mwandishi kwanza upate ridhaa yake nafikiri anaweza kukupa hata summary yake kwenye soft copy.
 
Mponjoli

Mponjoli

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Messages
667
Likes
15
Points
35
Mponjoli

Mponjoli

JF-Expert Member
Joined Feb 29, 2008
667 15 35
Unapofanya hivyo zingatia na sheria za haki miliki pia. Kwa nini usimtafute Mwandishi kwanza upate ridhaa yake nafikiri anaweza kukupa hata summary yake kwenye soft copy.

Jamaa alitaka afanye ufisadi! Huu wote ni ufisadi,unatumia jasho lamtu bila ridhaa yake,kisa wana JF wapate.

Muacheni muungwana auze hata kidogo basi duh!
 
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
45,903
Likes
32,639
Points
280
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
45,903 32,639 280
mkuu tuwekee ukipata mda ..
 
Sikonge

Sikonge

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2008
Messages
11,550
Likes
650
Points
280
Sikonge

Sikonge

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2008
11,550 650 280
Sijui kama Mzee Mwanakijiji ataandika chake kwa Kiswahili juu ya USANII wa Tanzania. Hapa nikiwa na maana ya WASANII wote na zaidi iwekwe juu ya MSANII namba moja moja hadi tano wa Tanzania (the big five).

Hamna jhaja ya kuandika mengi maana kitakosa maana. Ikiwezekana hata wawe watatu tu au wawili. Waandishi anzeni kazi na sisi tutanunua. Inaweza kuwa ahadi HEWA za viongozi mwaka 2005, kushindwa kutimiza majukumu na takatala nyingine kibao. Uzembe na kutokufuatilia kazi. Vielelezo vipo kibao kama picha ya Gavana, hopsital ya watoto Temeke, shule za msingi nk.......
 
Fidel80

Fidel80

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2008
Messages
21,970
Likes
140
Points
145
Fidel80

Fidel80

JF-Expert Member
Joined May 3, 2008
21,970 140 145
Jamaa alitaka afanye ufisadi! Huu wote ni ufisadi,unatumia jasho lamtu bila ridhaa yake,kisa wana JF wapate.

Muacheni muungwana auze hata kidogo basi duh!
Hahahaha sasa waliopo mbali tutawasaidiaje jamani waliopo Iraq, Brazil kwani wao hawataki kukisoma?
 
Kiranga

Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
43,029
Likes
18,077
Points
280
Kiranga

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
43,029 18,077 280
As long as I hate these "fake degrees"

Hivi Tanzania tuna body inayo accredit vyuo kwamba hivi ni vya kweli na hivi ni fake?

Unless tuna kitu kama hicho, au mtu kanunua degree na hajaingia darasani, itakuwa vigumu kusema "hiki chuo fake"
 
RayB

RayB

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2009
Messages
2,754
Likes
93
Points
145
RayB

RayB

JF-Expert Member
Joined Nov 27, 2009
2,754 93 145


okey labda nikifikaa kwenye scanner, maana amewatolea uvivu hao kina Mahanga , sasa kwasababu mwanzoni walimtishia kwenda kwa mahakama sasa wapate nakala halisi ya maelezo kupitia chapisho hili kisha wakamsue Msemakweli kama jeuri ipo
Mzee hata mimi ningetamani sana kukipata online kwani itakuwa kazi kukisoma kwa sasa lakini wasiwasi wangu ni kuwa tutaua nguvu ya huyu jamaa manake katumia fedha ati na kazi yake inaonekana kuwa nzuri. andaa muhtasari tuletee mzee
 
Sikonge

Sikonge

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2008
Messages
11,550
Likes
650
Points
280
Sikonge

Sikonge

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2008
11,550 650 280
As long as I hate these "fake degrees"

Hivi Tanzania tuna body inayo accredit vyuo kwamba hivi ni vya kweli na hivi ni fake?

Unless tuna kitu kama hicho, au mtu kanunua degree na hajaingia darasani, itakuwa vigumu kusema "hiki chuo fake"
Kuna chombo kama hicho ingawa sifahamu uwezo wao kwani wako chini ya wizara. Namfahamu dada yake mmoja Mwakalinga ambaye anafanya kazi hiyo. Ila kwa kuwa wako chini ya wizara, tayari uwezo wao ni mdogo kwani hawawezi kumlima waziri wao au Waziri Mkuu.

Ilitakiwa hiki chombo kijitenge.
 
T

TANURU

Senior Member
Joined
Jan 13, 2010
Messages
162
Likes
0
Points
0
T

TANURU

Senior Member
Joined Jan 13, 2010
162 0 0
As long as I hate these "fake degrees"

Hivi Tanzania tuna body inayo accredit vyuo kwamba hivi ni vya kweli na hivi ni fake?

Unless tuna kitu kama hicho, au mtu kanunua degree na hajaingia darasani, itakuwa vigumu kusema "hiki chuo fake"
TCU ipo.
 
Brooklyn

Brooklyn

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2009
Messages
1,461
Likes
55
Points
145
Brooklyn

Brooklyn

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2009
1,461 55 145
Aiseee ameweka mambo kinagaubaga!! Tafuteni copy wadau mkisome!
 
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined
Sep 3, 2009
Messages
4,891
Likes
198
Points
160
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined Sep 3, 2009
4,891 198 160
katika Ujumla wake elimu ambayo imeniacha hoi ni ya ndugu William Lukuvi , kumbe elimu yake ni ya darasa la saba, akiwa nacheti ha ualimu wa UPE...SASA jamaa anajitambulisha kuwa anashahada ya masuala ya kimataifa BA (international studies and Diplomacy) na amekua akipata fursa kadhaa kama kuiwakilisha nnchi katika makongamano ya kimataifa kupitia Bunge ambako yeye ni mmbunge
 
Kasheshe

Kasheshe

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2007
Messages
4,699
Likes
101
Points
145
Kasheshe

Kasheshe

JF-Expert Member
Joined Jun 29, 2007
4,699 101 145
Namfahamu Mh. Diallo, na nakumbuka nilivyokuwa namuona akipiga book. na nisikuwa nikimsifia kwamba hakika yeye unawezo mkubwa kuliko vijana wengi, kwa maana kuweza kusoma, siasa, biashara etc. But I saw that man... is extraordinary.

Jamaa amesomea degree yake... sasa kama munadhani kusoma lazima uwe darasani... kama hamtambui distance learning... that is your proble.
 

Forum statistics

Threads 1,250,456
Members 481,354
Posts 29,733,684