VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
NIMR walisema kuwa imebainika, kiutafiti, kuwa virusi vya ugonjwa hatari wa Zika vipo nchini Tanzania. Utafiti ukasema kuwa asilimia zaidi ya kumi ya waliotafitiwa wamebainika kuwa na vimelea vya Zika.
Lakini, Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu alikanusha haraka yenye baraka kuwa utafiti huo haujathibitisha kuwepo kwa Zika nchini. Waziri Ummy akasema, na kuwatoa hofu watanzania, kuwa Tanzania haina Zika. Akasema kuwa utafiti huo ulifanyika kwa kipimo cha Zika.
Sasa, inawezekanaje kutafiti kuhusu kipimo cha Zika mahali pasipo na Zika? Inawezekanaje kutafiti ulaji wa matunda kusipo na matunda? Mniwie radhi kwa kuchelewa kukauliza kaswali haka kwakuwa nilikuwa 'bize'.
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam