Kijipu uchungu TRA Terminal II Airport geti la wanaowasili

mbishi sana

Senior Member
May 10, 2013
102
74
habar wanajamvi!

kumekuwa na rushwa ya hatar pale TRA terminal two airport. abiria wanaosafiri na mizigo yao wakishuka pale huwa hawalipi kodi inayostaili.

utakuta mtu amekuja na mzigo toka china. kodi ni million tatu. atalialia pale jamaa watamwambia atoe milion moja na nusu. kisha anaandikiwa karatasi ya laki tatu aende kulipa benki.

huu mtindo umeshamiri saana hasa kwa miaka hii ya karibun ambako kumekuwa na kundi kubwa la watu kwenda nunua vitu toka china na dubai.

hakika hiki ni kijipu uchungu. maana mpaka sasa katika fumua fumua ya TRA na bandari hawa jamaa hawajaguswa.

nadhan waziri mteule ukipata huu uzi weka kwenye rekodi zako ili uende iokoa pesa ya serikal inayopotea kwenye matumbo ya watumishi hawa.
 
Hii ni kweli. Kuna MTU nilimsikia akimhadhia mwenzake walikuwa wamekaa sehem masikio yakabahatika kunasa mazungumzo yao. Hugo jamaa inaonekana yupo Kariakoo alikuwa ametoka China walimfanyia estimation ya kodi akaambiwa alalipie laki8 lakini ktk hizo laki 8 aliambiwa laki5 aziache pale kwenye droo na laki 3 ndio akalipie.

Inasemekana wale vijana wa pale wanafedha chafu sana ambazo hazilingani na mshahala wao.

Vyombo husika tunaomba mfikishieni ujumbe waziri na Rais pia kuwa pale airport watumishi wa TRA wanaiibia sana nchi yetu.

Mie ni mtanzania mzalendo ninayechukia ufisadi na wizi wa aina yoyote. Kama unatabia za wizi ukikaa karibu yangu utanichukia kwani Tabia chafu sipendi.

Serikali yetu nzuri tunayoiamini hili LA Airport it's True lifanyieni kazi
 
Jamani wale jamaa wana laana ramadhan ya mwaka huu nilikuja na tende kilo moja walivo wajinga walinikomalia nikailipie ushuru kwa hasira niliifungua nikamimina ndani ya debe la taka tukakosa sote
 
Jamani wale jamaa wana laana ramadhan ya mwaka huu nilikuja na tende kilo moja walivo wajinga walinikomalia nikailipie ushuru kwa hasira niliifungua nikamimina ndani ya debe la taka tukakosa sote


Mpaka tende?
 
Yes pale kweli ni uozo mtupu, wanaweza kukomalia mwenye vizawadi viwili vitatu ilihali wenye mizigo ya biashara wanalipia kiduchu serikalini nyingine zote jamaa wanatia mfukoni
 
Hayo unayozungumzia terminal 2 hayapo tena yalikuwa miaka ishirini iliyopita
 
ni kweli nami kipindi cha rais aliyepita nilipishwa kidogo nyingine wnkuambia peleka pale ungoje risti mpaka kesho kutwa
 
Back
Top Bottom