Kijiji chadai hakina maji tangu uhuru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kijiji chadai hakina maji tangu uhuru

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Dec 27, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 414,924
  Trophy Points: 280
  Kijiji chadai hakina maji tangu uhuru


  Na Raphael Okello, Rorya

  WAKAZI wa Kijiji cha Panyakoo, Kata ya Goribe wilayani Rorya mkoani Mara wameilalamikia serikali kwa kushindwa kuwapatia huduma ya maji ya mifugo na matumizi ya majumbani tangu uhuru na kusababisha kufuata huduma hizo katika nchi jirani ya
  Kenya.

  Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi mwishoni mwa wiki baadhi ya wakazi hao wamesema kutokana na ukosefu wa maji kijijini hapo na vijiji jirani vya Ng’ope, Charya na Nyamusi, wananchi wanalazimika kunywesha mifugo yao katika malambo ya Olasi nchini Kenya ambapo licha ya kutozwa fedha katika huduma hizo, lakini pia wanateseka kutembea umbali mrefu wa wastani wa km 30 kwenda na kurudi pamoja na mifugo yao.

  Wamedai kutokana na hali hiyo baadhi ya mifugo yao imekuwa ikipotea au kuibwa na watu wasiojulikana hivyo wameiomba serikali kuwachimbia lambo kwa ajili ya mifugo yao na visima kwa matumizi ya nyumbani.

  Wananchi hao wamekuwa wakipata maji katika msimu wa mvua katika visima vifupi vya asili kwa matumizi ya nyumbani, na Mto Ondoche kwa mifugo, lakini vyanzo hivyo huchukua muda mfupi tu kukauka mara baada ya msimu wa mvua kumalizika.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 414,924
  Trophy Points: 280
  Ni vyema wafugaji wetu wakaacha ushamba wa kuiona mifugo ni wa kuwaletea masifa au heshima kijijini kwao au kwa minajili ya kulipia mahari tu......................kwa kufanya hivyo wanakuwa ni watumwa wa mifugo hiyo wakati ambapo mifugo hiyo inapaswa kuwa ni ya kuwarahisishia maisha kama kuchimba malambo kwa kuiuza baadhi ya mifugo yao na wao kunufaika na kazi ya ufugaji.................
   
 3. mdoe

  mdoe JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 436
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  vijiji kama hivyo vipo kibao.
   
 4. B

  Bull JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii nimoja kati ya Failures za Nyerere.

  Alipo leta vijiji vya ujamaa, agriculture sector ndio ikafa kabisa, pamoja na yote hakuweza kuleta huduma za maji, umeme, nk, vijijini kama alivyo dai. kpumzike mzee,,,,,,
   
 5. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #5
  Dec 27, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Inasikitisha kuona mafisadi wanavyotesa wakati kuna watu wana hali duni hivyo!Huko hata rais wanamjua kweli?
   
 6. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #6
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,088
  Likes Received: 1,157
  Trophy Points: 280
  hao hao ndio wana ccm dam, na wanampenda mkwere na kundi lake. Tusimlaum nyerere sana alijitahidi kadri ya uwezo wake. Wakuwalaum ni hawa manyangau. Mkwere, mkapa na wenzao ambao wamefeli kwa asilimia zote kutatua matatizo ya wananchi.
   
 7. K

  Kimanzi Member

  #7
  Dec 27, 2010
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha kumlaumu Mwl. Nyerere aliacha misingi kumbuka vizuri wewe Bull.
   
 8. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #8
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ruta wewe vipi?Hivi unaifahamu Tanzania kweli?Mbona híi ndiyo kawaida.Kijiji changu nilichozaliwa hakijawahi kuwa na bomba na kwa sasa vijito vyote vilivyokuwa vinatiririsha maji vimekauka kabisa.Hali ni mbaya kupindukia.
   
 9. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #9
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,088
  Likes Received: 1,157
  Trophy Points: 280
  mwenyetu paul kagame,kaanzisha program wanayoiita bye by nyakasi. Yaani kwaheri nyumba za majani.wanavunja nyumba zote za mbavu za mbwa na kujenga za kisasa. Ni aibu na fedheha kwetu. Na utajiri wote tulionao tuna shindwa na ka rwanda kwa maendeleo na utawala bora. Tatizo hapa ni uongozi mbovu na viongozi mazuzu waliosoma ili kufaulu mitihani na sio kuelimika. Inatia kichefu chefu ndio maana nimeoa mnyarwanda angalau wanangu wana cha kujivunia na sio huo ufisadi uliojaa nyumbani.
   
 10. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #10
  Dec 27, 2010
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 135
  Babu hapo Nyerere unamuonea.Nyerere alijitahidi ukizingatia nchi ilikuwa changa sana sasa leo hii gharama ya chai na vitafunio ni bilioni kadhaa wakati wananchi hata maji bado ni hadithi..
   
 11. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #11
  Dec 27, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Maskini kama wangejua kwamba kilio chao si cha kwao peke yao wasingetoa kura kwa Ayila. Sasa wasubiri Ayila atawajengea visima maana ilikuwa ahadi zake! Sina huruma na watu wanaojitakia shida wenyewe. Walidanganywa na wakina Sarungi weeee sasa wameingia choo ya kike!
   
 12. T

  Topical JF-Expert Member

  #12
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Si wachimba maji wanakijiji wote (i mean wanaume wote hapo) kijijini wangeanza kuchimba maji kwenda chini ya ardhi tangu 1961 wakapokezana hadi leo wangepata maji nina hakika au siyo?

  Mwishowe watasema kijiji hakina vyoo tangu uhuru

  Wajiulize wamefanya nini kujiletea maendeleo wakiwa huru..siyo kuletewa maendeleo

  Hizi line of thinking ndio zinatakiwa kubadilika period..chimbeni maji chini yapo tele
   
 13. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #13
  Dec 28, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Haya ndio majibu yenu wana ccm baada ya uchaguzi!!!!! Sawa bwana wamewasikia!!!
   
 14. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #14
  Dec 28, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,807
  Likes Received: 1,973
  Trophy Points: 280
  Vijiji vyenye matatizo haya vipo vingi mno na tena vijiji kama hvyo unakuta vina wanavijiji wao ambao wana nyadhifa za juu serikalini mfano mzuri ni kijiji cha Tanganyika Masagati ambako gavana wa benki kuu aliyepita ni mwenyeji wa kule lakini hakuna barabara wala maji pamoja na huduma nyingine za muhimu.....
   
 15. m

  maarufu Member

  #15
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha adhabu iwarudie kwa kuendekeza ccm
   
 16. n

  nyantella JF-Expert Member

  #16
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45

  Waongo hao. yaani wakati wa ukoloni maji yalikuepo baada ya uhuru yakaisha hadi leo!!!!!!!! wanakunywa nini? Halafu wana JF wilaya ya rorya inapakana na ziwa victoria wanavua samaki humo kwa kitoweo halafu maji hawana? si wahame Miaka hamsini wapo na maji hakuna is it possible? tuache uongo bana!!!!!!!!!!!
   
Loading...