Kijiji cha Nyuki Singida, Dunia mpya usiyoijua

Suphian Juma

Senior Member
Apr 2, 2019
133
546
KIJIJI CHA NYUKI SINGIDA, DUNIA MPYA USIYOIJUA:


Ilikuwa Agosti 2, 2022 majira ya saa 10 jioni nikiwa nimeketi peke yangu juu ya mawe nyumbani Singida, nikiyatathimini maisha yangu, nilipofeli, nilipofaulu na wapi natamani kuelekea, napokea simu:


"Hello Suphian, mzima? Naomba nikupongeze kwa Barua yako bashasha uliyowaandikia Mawaziri wanne kuhusu changamoto ya INTERNET Hifadhi za Ngorongoro na Serengeti, umeiandika kwa ustadi mkubwa na kwa lugha ya staha. Sisi kama Kijiji cha Nyuki Singida tunaomba tukupe ofa ya kuja kufanya "vacation" kwetu, tutasimamia gharama zote ikiwemo malazi na chakula." Anahitimisha Mkurugenzi na Mwanzilishi

wa Kijiji cha Nyuki, Ndugu Philemon Josephat Kiemi, almaarufu "Kiemi".


Ni nani kati yenu angekataa ofa hii ukizingatia kama binadamu tunaishi katika maisha ya mvutano wa mara kwa mara, tunachoka, tuna wasiwasi, Tuna maisha ya kichaa kweli. Makataa yasiyoisha, kufanya kazi nyingi, mipasho ya habari hasi kama ambavyo mtaalamu wa saikolojia ya utambuzi Yulia Zakharova asemavyo "Ubongo wetu uliundwa wakati ambapo mtu wa kale alikuwa hatarini kila wakati," hivyo tunahitaji amani na utulivu wa Bongo zetu.


Naam.. nilipokea pongezi za Barua ya wazi kwa Mawaziri ambayo kimsingi licha ya kupokelewa chanya na WaTanzania wengi, ila pia imewafikia Mawazi wote, na wameniahidi kulishughulikia tatizo la INTERNET Ngorongoro, Serengeti na vivutio vingine ili Filamu ya Royal Tour ya Rais wetu kipenzi, Mhe

Samia Suluhu Hassan izidi kutuletea utitiri wa watalii (Nawashukuru sana).


Lakini pia nilikubali mwaliko wa Taasisi ya Kijiji cha Nyuki kwenda kufanya "Vacation" kwao Kijiji cha Kisaki mkoani Singida, Tanzania.


Kwa wasiojua maana ya Vacation; hili ni neno la Kilatini ama Kifaransa cha kale lililozaliwa kutokana na maneno "vacatio" ama "vacare" ambayo tafsiri yake ya lugha ya kiingereza ni "be unoccupied" yaani kwa Kiswahili chetu "likizo ya mapumziko" kama ambavyo tunaona watu wengi maarufu duniani hata hapa Tanzania wameanza kulitumia neno hili kwa kasi wanaposafiri nje ya Makazi yao kwenda kutuliza akili zao na wenza wao.


TURUDI KWENYE VACATION YANGU KIJIJI CHA NYUKI.


Saa nne asubuhi Singida mjini, Agosti 5, 2022 nachukuliwa na gari ya Ofisi ya Kijiji cha Nyuki kuelekea pahala paitwapo Kijiji cha Nyuki ambapo kiukweli pamoja na mwaliko ila sikudhani kama kuna cha kunikonga moyo humo ndani ukizingatia sikuwahi kwenda hata mara moja licha ya kupasikia sikia na kumsikia Mwekezaji Mwanzilishi ndugu Kiemi ama kuona akitupia picha za Asali kwenye ma-group ya mtandao wa WhatsApp ya Mkoa wa Singida tulipoungwa pamoja.


Ghafla kilomita 12 mkono wa kulia kutoka Singida mjini tukiwa tunaelekea barabara kuu kama unaenda jijini Dodoma nilijikuta "muvi linaanza" kwa kustaajabishwa na "bonge" la kibao linalovutia likinakishiwa na rangi ya karoti likisomeka "KIJIJI CHA NYUKI CO. LTD, WHERE NATURE MADE BEES AND PEOPLE BEST FRIENDS" huku linaorodhesha huduma zipatikazo humo, na ndipo geti kuu la kuingia humo "dunia mpya" linapatikana.


Nikiwa sijamaliza kushangaa, nikiwa ndani nikajikuta nashikwa na butwaa, macho kodo mithili ya mjusi kubanwa na mlango pale nilipoona ndani ya pori kubwa la miti ya asili yenye urefu wa wastani kuna nyumba kadhaa za rangi ya karoti zikijengwa mbalimbali huku umeme na miundo mbinu ya maji ikisambazwa huko ndani kikamilifu. Nauliza, naambiwa kila nyumba ina matumizi yake, zipo nyumba za Makazi, ofisi, viwanda na kadhalika.


Sio hivo tu, nakuta wafanyakazi kwa makumi wakiwa wanachakarika na kazi zao za nyuki mfanano wa mchwa wakijenga kichuguu; wapo wapishi, watengeneza mizinga, wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza asali, walinzi, waongoza watalii "Tour guides", Maafisa wa vitengo maalum kama Afya, mafunzo, miradi n.k ambapo kwa mujibu wa Mkurugenzi Kiemi, jumla yao ni wafanyakazi 114 katika Kijiji cha Nyuki ambacho kinachukua jumla ya ekari 45,000 ambapo zipo katika Kata za Kisaki, Ikungi, Iglansoni, Itigi Mkoani Singida na Kata ya Uyui iliyopo mkoani Tabora.


Na hadi hapo kabla sijaambiwa chochote kuhusu Uwekezaji huu ndipo nilipojikuta "naropoka" kwa furaha tele kwamba kweli eneo hili la Uwekezaji linastahili kuitwa na kubeba maantiki ya neno "kijiji" kwa kuzingatia tafsiri ya kuona mwingiliano wa shughuli za ufugaji wa nyuki, Makazi ya Watu (wafanyakazi), miundo mbinu ya huduma za kijamii, miti asilia, ndege, wanyama kama digidigi, Sungura na kadhalika.


Naingizwa na Bwana Kiemi akiambatana na vijana wake wa kupokea watalii katika chumba maalum cha maonesho ya bidhaa za nyuki na huduma zipatikazo Kijiji cha Nyuki.


Bwana Kiemi ambaye ni kijana ninayefanana nae miaka ya kuzaliwa, mwenye Elimu ya Shahada ya kwanza ya Sayansi ya kaya na Taaluma za walaji kutoka Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na ambaye pia Shahada yake Uzamili (Masters) ya Ufugaji nyuki Kibiashara katika Kilimo "Commercial Bee Keeping in Modern Agriculture" kutoka Chuo Kikuu cha Kiyahudi (Hebrew University of Jerusalem) cha nchini Israel, na Mwanzilishi wa Kijiji cha nyuki co.Ltd alinifafanulia kuwa Kijiji cha nyuki ni Shule, Hospitali, Kiwanda, Sehemu ya Utalii, Hifadhi, Soko , Hoteli na Ujumla wa Mambo mengine ya kawaida kwa Binadamu. Mimi na watalii wengine niliowakuta hapo juu tulipata mazao ya Nyuki na huduma zingine katika Kijiji cha Nyuki hizi zifuatavyo:


MAZAO YA NYUKI (BEE PRODUCTS).


1)ASALI ASILIA(Organic Honey).


Hii wanaiita "Singida Asali"; kwa wale wanaoifahamu hapa najua wameanza najua wameanza kujilamba
UPEKEE wake ni asali ambayo ni UNCONTAMINATED (haina mchanganyiko wowote wa kitu kisichofaa, kiwango cha maji ni kidogo sana, ina harufu nzuri na maua ya mimea ambapo nyuki wameitengeneza ni Adimu na inapatikana Singida tu. Wastani wa kuuza zao hili kwa kilo ni TZS 12'000 kwa kilo.




2) VUMBI LA SINGIDA: (Multifloral bee pollen)- Hii ni Bidhaa inayojulikana kama "Only nature complete food" au "Miracle or Magic food". Ina protini -30-40% , Vitamini na madini yote yanayohitajika na mwili wa Binadamu. Wengi wanaitumia kama bidhaa inayoongeza nguvu za kiume na za kike, inaimarisha Kinga ya mwili ya binadamu dhidi ya magonjwa nyemelezi na kuratibu ukuaji wa Watoto. Wastani wa kuuza zao hili kwa kilo ni TZS 300'000/-


3) MISHUMAA YA NTA:(Natural Air Purifiers-beewax candles); Huu ni Mshumaa ambao ni spesheli kwa kuwasha Chumbani kwa ajili ya Kusafisha hewa, kutoa Mwanga na kutoa Harufu nzuri na pia sehemu ya Matibabu ya Macho maana inakupa kitu kinaitwa "Yellow illuminate" inavutia na inanukia vizuri saana. Wastani wa kuuza zao hili kwa kilo ni TZs 15'000/-


4) SUMU YA NYUKI (Bee venom): Hii inasadikika ina peptides zinazofanana na zile ya immune system ya mwili wa Binadamu au vitu ambayo vinachangia kwa asilimia zaidi ya 80% kuimarisha Kinga ya mwili. Ukiingiza Maabara na kuangalia vilivyomo utapata zaidi ya asilimia 50% ya compound inayojulikana kama Mellitin yenye uwezo wa kutibu Kansa na kuua virusi vya UKIMWI huku ikiiacha seli hai zikiwa salama.Bidhaa hii soko lake ni kwenye Pharmacetical industries. Hapa Kijiji cha nyuki inazalishwa kwa tangu miaka sita iliyopita. Wastani wa kuuza zao hili kwa kilo ni TZS 180M


5) GUNDI YA NYUKI ( Propolis): Hii ni bidhaa ya nyuki ambayo ni "Strong anti-Bacteria , Anti-Fungi na Anti-viruses. Kwamba ni moja ingredient kwenye viwanda vya vipodozi na Madawa. Pia hutumika "ku-relax nerves" wakati wa Operation kubwa za kidaktari zinazohusisha kukata mishipa ya Fahamu. Kwa matumizi ya kawaida ni kwamba unailoweka kwenye maji na maji yanageuka kuwa meusi , Hayo maji ukiyatumia kuosha kidonda haraka kinageuka kuwa chekundu na kupona. Hakika hii ni zaidi ya Iodine solutions inayotumika kutibu majeraha. Wastani wa kuuza zao hili kwa kilo ni TZS 750,000.


6) MAZIWA YA NYUKI ( Royal jelly):- Hii bidhaa ni Anti-aging yaani Humfanya mtumiaji asizeeke mapema kwani huunganisha mwili na kuupa uimara. Usishangae kumwona wanamke wa miaka 50, akitumia bidhaa hii kufanana na Binti wa miaka 25. Bidhaa hii ni chakula pekee cha malkia wa nyuki kwenye Mzinga ambapo malkia akila huishi miaka 3-5 na nyuki wengine wasiokula hichi chakula huishi siku 55-60 toka kwenye yai. Hii ndio iliwavuta wanasayansi wengi kufanya utafiti uliopelekea binadamu wanaotumia zao hili kuchelewa kuzeeka. Wastani wa kuuza zao hili kwa lita TZS 12M.


(7) SUPU YA NYUKI (BEE BROOD): Hili ni zao la nyuki ambalo ni watoto wa nyuki au larvae lina protini nyingi. Wazee wengi na wavunaji wa asali wanatafuna masega yakiwa na matoto yale pamoja. Hii kwa historia inasadikika wanaokula hivi wawaumwi maradhi mbalimbali mara kwa mara. Hii kwangu ilikuwa mara ya kwanza na nilijikaza na mwisho nikazoea. Wastani wa kuuza zao hili kwa lita ni TZS 50'000.



HUDUMA(SERVICES);


1) Mizinga, pollen trap (Mitego ya chavua ya nyuki) , mavazi ya kujikinga na nyuki ( Bee protectives gears) na kadhalika.



2) Mafunzo ya Ufugaji wa nyuki Kibiashara kwa Vitendo


-Monthly Courses; Hizi ni Kozi za kila mwezi ambapo Tsh milioni moja kwa wazawa na 1600 USD kwa wanafunzi Wageni.


-Field attachment; wanafunzi wa kufanya mafunzo kutoka vyuo wanakaribishwa na chakula na malazi ni bure.


-Exchange programs; Hii ni fursa ya wataalam wa nyuki kutoka Kijiji cha Nyuki kubadilishana uzoefu na wenzao kutoka aidha Mkoa na Mkoa ama Nchi na Nchi.




Baada ya kuelezwa haya katika siku hiyo ya kwanza nilipelekwa kiwanda cha kutengeneza mizinga ambapo nilijionea vijana wengi wa kike na wa kiume wakitengeneza mizinga mizuri sana, kuanzia kwenye muonekano hadi kwenye uimara wa "material" ya miti ya utengezaji huku nikibaini mizinga yote ikipigwa rangi ya karoti kuvutia nyuki na pia kuwekwa Lebo za kampuni ya Kijiji cha Nyuki.


Kwakuwa usiku uliingia tulifanya Utalii wa moto "Born Fire" na kupiga soga nyingi na baadae masaa yalivyoyoyoma ikatubidi tusitishe Utalii na hivyo nikapelekwa kwenye sehemu ya kulala ambapo ni kwenye hema "tent" maalumu lililoandaliwa kwa ajili yangu kando ya mto mdogo unaotiririsha maji yake ukikatisha ndani ya eneo hili.


Guys, kulala ndani ya "tent" ni raha mno. It's beyond advanture itself. Hewa nzuri, majani ubichi, kuna ka-joto fulani "amazing" yaani unajikuta unaufanya Ubongo wako kujiliwaza na kutafakari namna nzuri ya kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. I truly enjoyed kulala kwa tent siku zote nne za "vacation" yangu.


Siku iliyofuata (day 2) nilipata fursa ya kwenda kutembelea kiwanda cha kuchakata Asali. Ilikuwa ni uvunaji wa uzoefu wa kipekee mno. Nilibahatika kuona namna na pahala Asali ghafi inavyoanza kuwekwa kwenye mashine maalum, mashine ya kuchuja, mashine ya kuhifadhi na hadi inatolewa kama Asali Safi, na hatimaye kufungwa kwenye chupa maalumu zenye Lebo ya "Asali ya Singida" tayari kwa matumizi ya binadamu.



Siku ya Tatu (Day 3): Ilikuwa siku ya aina yake pia kwani nilitembezwa kilomita zaidi ya 10 kuona pahala mizinga inatengenezwa. Nilishuhudia maelfu na maelfu ya mizinga ikiwa imepangwa vema mithili ya wanafunzi ama wanajeshi wakiwa parade. Kwa mujibu wa Tour Guide wangu, Kijiji cha Nyuki kina idadi ya mizinga zaidi ya elfu 31 ambayo imesambazwa porini, huku mizinga yenye nyuki ikiwa ni elfu 19.



Tukiwa huko majira ya saa 2 usiku nikiwa nimevaa mavazi Maalum ya kurina Asali (Bee Protective Gears), nilirina Asali kwa mara ya kwanza maisha mwangu. Nyuki walikuwa wakali mno, ila kwakuwa sikuwa na sehemu ya wazi mwili mzima niliufunika, sikuumwa ingawa baadae niliumwa kwa maelekezo ya Tour Guide kwamba kuumwa na nyuki ni tiba ya mwili (Apatherapy). Ha ha ha ha


Nilichukua masega hadi kiwandani na hatimaye nilifuata hatua zote za kusakata asali hadi kutokea asali halisi. It was a marvelous experience never felt before.


Siku ya 4 (Day 4): Nilitembezwa sehemu mbalimbali za ndani kumalizia kuona madhari nzuri ambazo sikuona na pia kuagana na wafanyakazi, ila cha ajabu kabla sijaondoka nililetewa barua na Afisa Utumishi wa Kijiji cha Nyuki, guess what was inside!!? Ilikuwa ni barua ya ombi la kuajiriwa kuwa Afisa Habari na Masoko wa kampuni ya Kijiji cha Nyuki. Tulijadili kwa kina Mkurugenzi Mtendaji na hatimaye licha ya kubanwa na majukumu yangu mengine NILIIKUBALI OFA HII, na nimesaini MIKATABA ya kazi, hivyo hadi sasa naandika makala mimi Suphian Juma Nkuwi ni Afisa Habari na Masoko wa Kijiji cha Nyuki Singida. What a blessing!!


Something else to tell you, hakika siku zote nne nilisahau kabisa kama nipo Singida wala Tanzania, nikijumlisha na kulishwa vyakula vya asili hususani vya kabila la Wanyaturu (ugali wa uwele, mlenda, maziwa mtindi) ayamkini nilijiona nipo dunia mpya inayovutia na kushibisha roho, moyo na mwili na furaha zisizohesabika.


Wito wangu kwenu ndugu wasomaji karibuni sana Kijiji cha Nyuki kama watalii, mje msome Kozi ya mwezi mmoja utakula na kulala, trips utapelekwa na kadhalika kwa shilingi Milioni moja tu ya KITANZANIA.


Msiache pia kutumia bidhaa Adimu za nyuki kutoka Kijiji cha Nyuki Singida. Popote ulipo duniani tutakutumia. Wasiliana Nasi kwa namba +255717027973 au +255 765 895 805 au kwa akaunti zetu za Kijiji cha Nyuki kwenye mitandao ya kijamii ya Twitter, Facebook na Instagram ama kupitia website yetu ya www.kijijichanyuki.com kwa mawasiliano zaidi.



Karibuni tufuge nyuki kuunga juhudi za Serikali ya Rais Samia za kuboresha Sekta ya Ufugaji kama ambavyo Sera ya Taifa ya Ufugaji nyuki ya Mwaka 1998 inahimiza uanzishwaji wa hifadhi za nyuki za Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na watu binafsi ili kulinda makundi ya nyuki pamoja na malisho yao.


Kulingana na takwimu za Shirika la Chakula Duniani(FAO),Tanzania ni nchi ya 2 kwa ufugaji nyuki Afrika baada ya Ethiopia, njooni tufuge kwa wingi kwa kisasa na kibiashara kupitia Kijiji cha Nyuki Singida, ili tuifanye Tanzania yetu kuwa Nchi ya kwanza Afrika kufuga nyuki.


Mwisho: niwape wosia; Tunatoa nguvu zetu kuwajali wengine, lakini mara chache tunachukua wakati wa kupendezwa na sisi wenyewe. Njooni Kijiji cha Nyuki "tujipe raha wenyewe".


KAZI IENDELEE!!



Suphian Juma Nkuwi,

Singida, Tanzania,

Agosti 11, 2022.

Phone: 0717027973

Email: yessuphian@gmail.com


IMG_20220811_141453_108.jpg
IMG_20220811_141607_226.jpg
IMG_20220811_174327_484.jpg
IMG_20220811_174041_141.jpg
IMG_20220811_141146_124.jpg
IMG_20220811_173420_843.jpg
IMG_20220811_174545_217.jpg
IMG_20220811_174207_176.jpg
IMG_20220811_173211_211.jpg
IMG_20220811_141317_162.jpg
IMG_20220811_141214_661.jpg
IMG_20220811_174807_815.jpg
IMG_20220811_174836_910.jpg
IMG_20220811_175346_964.jpg
 

Attachments

  • IMG_20220811_174731_896.jpg
    IMG_20220811_174731_896.jpg
    29.5 KB · Views: 63
  • IMG_20220811_174327_484.jpg
    IMG_20220811_174327_484.jpg
    57.2 KB · Views: 62
Wajifyaaa munyampaa.

Hapo kwenye vumbi la Singida ni kama vumbi la Mkongo Kwa manufaa na matumizi?

Sijapitia tovuti ila ingefaa ukaweka gharama za utalii, hapa kwenye Uzi imeweka Bei za bidhaa na gharama za mafunzo pekee, au Kwa watalii ni kuzurura tu hakuna kulala huko huko?

Hao wahitimu wakishapata elimu na ujuzi, asali Yao soko ni hapo hapo Kijiji Cha nyuki ili ichakatwe au wanatafutasoko la asali yao wenyewe?

Hongera Kwa andiko zuri na pongezi Kwa kupata ajira.
 
Hongera kwa andiko zuri,na pia hongera kwa kuwa msemaji wa Kijiji,niliwahi kuona hicho kibao lakini sikudhani kama eneo hilo ni kubwa kiasi hicho na mambo yote hayo yanafanyika humo,ni uwekezaji mkubwa,safi sana

Nina maswali kadhaa hapa naomba
1.Kutembelea hapo gharama ni kiasi gani?
2.Vumbi la Singida linatengezwa kwa kutumia nini?
3.Sumu ya nyuki wanavunaje na inauzwa wapi?
4.Maziwa ya Nyuki yanapatikanaje?
5.Bei cha hicho kichupa cha Vumbi la Singida ni bei gani?

Asante.
 
Hongera sana, nimefika hapo, bwana Kiemi ni mtu mkarimu sana, tulipiga supu ya mbuzi , vumbi la Singida na Asali
 
Back
Top Bottom