Kijiji cha Nganjoni Wilaya ya Moshi vijijini Watembea umbali wa km 35 kutafuta huduma ya afya

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,000
WANANCHI wa Kijiji cha Nganjoni Wilaya ya Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro, wanalazimika kutembea umbali wa kilometa 35 kutafuta huduma ya afya. Wananchi hao wamekuwa wakitembea hadi katika Hospitali ya Kilema, iliyopo Marangu kutafuta huduma hiyo, kutokana na zahanati iliyopo kijijini hapa kutokuwa na dawa.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Salehe Zuberi alisema licha ya kuwapo kwa zahanati yenye daktari na wauguzi watatu iliyojengwa na wafadhili, lakini hakuna huduma yoyote.

Alisema wananchi wa kijiji hicho ambao ni zaidi ya 5,000 wanalazimika kutembea umbali mrefu na wengine kubebwa na machela, huku wajawazito wakijifungulia njiani kutokana na eneo hilo kuwa mbali na kituo cha afya.

Alisema kijiji hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali na kuiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kuwasaidia wananchi wa kijiji hicho kupata huduma za afya katika zahanati hiyo.

Alisema iwapo Serikali italeta huduma muhimu katika hospitali hiyo, kwa kiasi kikubwa itapunguza idadi ya vifo vya akina mama wajawazito na watoto katika kijiji hicho.

“Kwa kweli hii hospitali uwepo wake tulifikiri tumepata msaada, lakini ni kinyume na matarajio ya wananchi wetu jambo ambalo linafanya wananchi kukosa imani na Serikali yao,” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirikika la Kuwezesha Wanawake Kiuchumi mkoani Kilimanjaro (WEECE), Valeria Mrema, alisema matatizo mengi yanayokabili kijiji hicho yanatokana na wananchi kutoshirikishwa katika miradi ya maendeleo.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Ibrahimu Msengi ambaye alitembelea zahanati hiyo aliwaagiza watendaji wa kijiji hicho kuhakikisha wanakutana na wananchi, ili kutoa taarifa ya mapato na matumizi.
 
Makupa

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,538

hayo ndio matunda ya kumpa Lyatonga ubunge
 
Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
14,908

"Kwa kweli hii hospitali uwepo wake tulifikiri tumepata msaada, lakini ni kinyume na matarajio ya wananchi wetu jambo ambalo linafanya wananchi kukosa imani na Serikali yao," alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirikika la Kuwezesha Wanawake Kiuchumi mkoani Kilimanjaro (WEECE), Valeria Mrema, alisema matatizo mengi yanayokabili kijiji hicho yanatokana na wananchi kutoshirikishwa katika miradi ya maendeleo.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Ibrahimu Msengi ambaye alitembelea zahanati hiyo aliwaagiza watendaji wa kijiji hicho kuhakikisha wanakutana na wananchi, ili kutoa taarifa ya mapato na matumizi.

No wonder, 2015 wataichagua SSM!!! Mbunge wao ni Lyatonga Mrema au? Maana naye ni mwana SSM hana jipya!! Anatumikia asante yake ya ubunge wa SSM kupitia TLP!! Dhaifu tu.
 
kindafu

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
1,342
2,000
Mkuu weka kumbukumbu sahihi! Hospitali ya Kilema haipo Marangu! Pia kutoka Nganjoni kwenda Kilema Hospitali hazifikii hizo 35km!!! Ni wakati sasa umefika kwetu wananchi tunaotozwa kodi kila upande kuidai serikali huduma bora ya afya! Hii ni haki yetu ya msingi na sioni sababu gani "tuiombe serikali itufikirie!" Tusipowaonyesha hao viongozi wa serikali kuwa sisi ndo tuliowaajiri na ndo tunaowalipa mishahara na kuwapatia marupurupu mbali mbali bado wataendelea kufikiri kuwa kutuhudumia ni "favour"!!! Tafakarini wana Nganjoni!!!!
 
KXY

JF-Expert Member
Dec 31, 2011
877
250
WANANCHI wa Kijiji cha Nganjoni Wilaya ya Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro, wanalazimika kutembea umbali wa kilometa 35 kutafuta huduma ya afya.

Kwa jiografia ya huu mkoa nina wasiwasi na huo umbali, yani umbali wa km 35 kusini, magharibi, mashariki na kaskazini hakuna huduma za afya?

Ndani ya hizo km 35 kuna vijiji/kata ngapi na wanategemea huduma za afya toka wapi?
labda, ila nina mashaka na hii taarifa wenyeji watuambie
 
Mwikimbi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,762
2,000
hiki kijiji ni maarufu kwa kutengeneza pombe ya gongo, au chasoo, au inueni mioyooo, mabega juu, au chang;aa
 
Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,863
2,000
Hivi Lyatonga bado yuko hai jamani? Nilimuona mara ya mwisho akiwa na mabaka kama mamba. Kweli avumaye baharini papa. Baada ya Lyatongwa kuwekwa kinyumba na CCM unategemea nini? Baada ya Lyatonga kuyafakamia matapishi yake tutegemee nini?
 
lucid mosha

New Member
Apr 13, 2014
1
0
kiukwel hata kwenda hospitali na kurudi haiwezekan ukafikia umbali huo. Umbali huo urekebishwe kwan pana kilomita nane tu kutoka kilema hospitali hadi nganjoni....... Hata google map hatuwez kutumia asee?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom