Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,746
- 11,877
MADAI YA RUSHWA KWA DIWANI WA KIJICHI: MAAFISA WALIOHUSIKA SIO WA TAKUKURU
Diwani wa Kijichi, Eliasa Kassim Mtarawanje
VIDEO:
Maafisa waliohusika katika video inayoonekana ikimhusisha Diwani wa Kijichi, Eliasa Kassim Mtarawanje (28) sio wa kutoka TAKUKURU. Baada ya kuwasiliana na mamlaka hiyo, imekiri kuwa na taarifa za tukio hilo lakini imesema maafisa wake hawajahusika katika tukio hilo.
Aidha, JamiiForums imefuatilia sakata hili na kubaini maafisa wawili wanaoonekana kwenye video hiyo ni kutoka Kituo cha Polisi Chang’ombe jijini Dar na askari waliohusika wametambulika kwa jina moja moja “Afande Jumanne” na “Afande Lugoma”.
KILICHOTOKEA
Chanzo chetu kimebaini kuwa chanzo ni mgogoro unaohusisha ardhi inayodaiwa kuwa ya Serikali ambapo mfanyabiashara mmoja wa eneo hilo, Shaaban Matimbwa almaarufu “Timbwa” anadaiwa kuhusika kwa kiasi kikubwa na imebainika watu wengine waliohusika katika tukio hili (wasiovaa sare) ni walinzi (mabaunsa) wa Timbwa.
Diwani Mtarawanje anadaiwa kupigwa na kuumizwa wakati wa tukio hilo kwa mujibu wa mashuhuda. Shuhuda wetu amemuona akiwa Hospitali ya Kijichi alikoenda kwa matibabu kufuatia majeraha kichwani na mdomoni ambapo jino lake limelegea
MGOGORO WA ARDHI
Inadaiwa kuna eneo ambalo Serikali imelitenga ajili ya ujenzi wa Stendi ya Mabasi ambapo taarifa zinaonyesha kuwa waliokuwa eneo hilo walishalipwa isipokuwa mtu mmoja aliyetambulika kwa jina moja “Mzee Mkumba” na Timbwa anadaiwa ‘kununua kesi’ ya eneo hili ili adai fidia ya takribani Sh. Milioni 700 toka serikalini. Eneo hilo ambalo inakadiriwa ni nusu ekari, linatambulika na Serikali ya Mtaa huo kuwa bado mmiliki wake (Mzee Mkumba) hajapewa fidia na kuwa suala hilo lipo hadi kwenye kumbukumbu za Halmashauri
Timbwa anadaiwa kujaribu ‘kuwaweka sawa’ watu wengi ili aweze kupata fedha hizo na tayari Diwani Mtarawanje aliripoti ofisi za TAKUKURU mnamo Februari 4, 2020 juu ya kinachoendelea kabla ya kuwekewa ‘tego’ tarehe 6 Februari 2020 (tukio linaloonekana kwenye video)
JamiiForums ilipomtafuta diwani huyo, alikiri kushawishiwa na Timbwa achukue kiasi cha fedha lakini akakataa na amesema ndiyo sababu alipoombwa na mwananchi huyo wa eneo lake (Timbwa) waonane, aliamua kwenda na Mwenyekiti wa CCM wa eneo lake ili yasiwepo mazingira ya rushwa. Simu ya Timbwa ilikuwa ikiita bila kupokelewa.
Diwani huyo ambaye alipatikana baada ya uchaguzi mdogo 2017 ni diwani wa 3 kuongoza kata hiyo tangu uchaguzi Mkuu wa 2015, ameiambia JamiiForums kuwa yeye anaviachia vyombo vya dola vifanye kazi lakini akaonyesha kusikitishwa na alivyotendewa na askari walioshiriki katika tukio hilo.