• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Kijichi, Dar: Maafisa feki wa TAKUKURU, wakishirikiana na Polisi wadaiwa kumbambikia Kesi ya Rushwa diwani

  • Thread starter Roving Journalist
  • Start date
Roving Journalist

Roving Journalist

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2017
Messages
360
Points
1,000
Roving Journalist

Roving Journalist

JF-Expert Member
Joined Apr 18, 2017
360 1,000
MADAI YA RUSHWA KWA DIWANI WA KIJICHI: MAAFISA WALIOHUSIKA SIO WA TAKUKURU

2300023_IMG_20200208_120732_112.jpg

Diwani wa Kijichi, Eliasa Kassim Mtarawanje

VIDEO:

Maafisa waliohusika katika video inayoonekana ikimhusisha Diwani wa Kijichi, Eliasa Kassim Mtarawanje (28) sio wa kutoka TAKUKURU. Baada ya kuwasiliana na mamlaka hiyo, imekiri kuwa na taarifa za tukio hilo lakini imesema maafisa wake hawajahusika katika tukio hilo.

Aidha, JamiiForums imefuatilia sakata hili na kubaini maafisa wawili wanaoonekana kwenye video hiyo ni kutoka Kituo cha Polisi Chang’ombe jijini Dar na askari waliohusika wametambulika kwa jina moja moja “Afande Jumanne” na “Afande Lugoma”.

KILICHOTOKEA
Chanzo chetu kimebaini kuwa chanzo ni mgogoro unaohusisha ardhi inayodaiwa kuwa ya Serikali ambapo mfanyabiashara mmoja wa eneo hilo, Shaaban Matimbwa almaarufu “Timbwa” anadaiwa kuhusika kwa kiasi kikubwa na imebainika watu wengine waliohusika katika tukio hili (wasiovaa sare) ni walinzi (mabaunsa) wa Timbwa.

Diwani Mtarawanje anadaiwa kupigwa na kuumizwa wakati wa tukio hilo kwa mujibu wa mashuhuda. Shuhuda wetu amemuona akiwa Hospitali ya Kijichi alikoenda kwa matibabu kufuatia majeraha kichwani na mdomoni ambapo jino lake limelegea

MGOGORO WA ARDHI
Inadaiwa kuna eneo ambalo Serikali imelitenga ajili ya ujenzi wa Stendi ya Mabasi ambapo taarifa zinaonyesha kuwa waliokuwa eneo hilo walishalipwa isipokuwa mtu mmoja aliyetambulika kwa jina moja “Mzee Mkumba” na Timbwa anadaiwa ‘kununua kesi’ ya eneo hili ili adai fidia ya takribani Sh. Milioni 700 toka serikalini. Eneo hilo ambalo inakadiriwa ni nusu ekari, linatambulika na Serikali ya Mtaa huo kuwa bado mmiliki wake (Mzee Mkumba) hajapewa fidia na kuwa suala hilo lipo hadi kwenye kumbukumbu za Halmashauri

Timbwa anadaiwa kujaribu ‘kuwaweka sawa’ watu wengi ili aweze kupata fedha hizo na tayari Diwani Mtarawanje aliripoti ofisi za TAKUKURU mnamo Februari 4, 2020 juu ya kinachoendelea kabla ya kuwekewa ‘tego’ tarehe 6 Februari 2020 (tukio linaloonekana kwenye video)

JamiiForums ilipomtafuta diwani huyo, alikiri kushawishiwa na Timbwa achukue kiasi cha fedha lakini akakataa na amesema ndiyo sababu alipoombwa na mwananchi huyo wa eneo lake (Timbwa) waonane, aliamua kwenda na Mwenyekiti wa CCM wa eneo lake ili yasiwepo mazingira ya rushwa. Simu ya Timbwa ilikuwa ikiita bila kupokelewa.

Diwani huyo ambaye alipatikana baada ya uchaguzi mdogo 2017 ni diwani wa 3 kuongoza kata hiyo tangu uchaguzi Mkuu wa 2015, ameiambia JamiiForums kuwa yeye anaviachia vyombo vya dola vifanye kazi lakini akaonyesha kusikitishwa na alivyotendewa na askari walioshiriki katika tukio hilo.
 
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2015
Messages
28,705
Points
2,000
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2015
28,705 2,000
Tunasubiri video clip na audio clip ili tuchangie, wekeni hata Kama ni mtego feki
 
chagu wa malunde

chagu wa malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
1,021
Points
1,500
chagu wa malunde

chagu wa malunde

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
1,021 1,500
Diwani amepigwa akiwa wapi? Kituo cha polisi? Na kama aliumizwa amefungua kesi? Je ni kweli alichukua pesa? Je polisi wanaruhusiwa kukamata mchukua rushwa?
 
stroke

stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Messages
19,471
Points
2,000
stroke

stroke

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2012
19,471 2,000
Mimi ni kijana mwenzenu.
 
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Messages
33,824
Points
2,000
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2007
33,824 2,000
Hivi Jamiiforums ina mwandishi wake wa habari za uchunguzi anayejulikana kama Roving Journalist siku hizi?
Sikupata kulijua hilo?
 
BLUE DOG

BLUE DOG

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2016
Messages
452
Points
1,000
BLUE DOG

BLUE DOG

JF-Expert Member
Joined Dec 10, 2016
452 1,000
Waache wamalizane fisiem na rushwa ni sawana mgonjwa na uji mie ni jirani kabisa na eneo husika ila sikuwa nalifahamu hilo swala
 
mng'ato

mng'ato

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2014
Messages
21,772
Points
2,000
mng'ato

mng'ato

JF-Expert Member
Joined Oct 27, 2014
21,772 2,000
Timbwa mmiliki wa Giraffe paleni Sudan temeke.

Ila jamaa anapenda kweli kununua kesi za ardhi
Atakuja kupata anachostahili.

Michael Wambura wa TFF alikua mmoja wa watu wanaopenda kesi sana,kitu kidogo tu kakimbilia mahakamani wakaona huyu asituchoshe kapigwa kesi ya utakatishaji fasta tu kakaa ndani karibu mwaka mzima,ametoka na kutakiwa kulipa Tsh.100mil.

Kamuulizeni sasa hivi kama kiherehere cha kupenda makesi kesi bado anacho,akiona mahakama anaipita kwa mbaali bila kugeuka.

dodge
 
X

X-bar

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
391
Points
500
X

X-bar

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2019
391 500
Ila huyu dogo diwani naye anapenda kujiingiza katika ishu kama hizi. Anapenda sifa na kuonesha kuwa ana mamlaka kwa kila jambo. Anahusika sana kujenga mazingira ya kula rushwa na ubaguzi wa kisiasa kwa kuzuia maeneo au shughuli za kibiashara. Hicho kilichompata ni matokeo ya tabia zake za kujifanya yeye ndo kila kitu kwa wananchi wa Kijichi.
 
chagu wa malunde

chagu wa malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
1,021
Points
1,500
chagu wa malunde

chagu wa malunde

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
1,021 1,500
Ila huyu dogo diwani naye anapenda kujiingiza katika ishu kama hizi. Anapenda sifa na kuonesha kuwa ana mamlaka kwa kila jambo. Anahusika sana kujenga mazingira ya kula rushwa na ubaguzi wa kisiasa kwa kuzuia maeneo au shughuli za kibiashara. Hicho kilichompata ni matokeo ya tabia zake za kujifanya yeye ndo kila kitu kwa wananchi wa Kijichi.
Mbona unamhukumu kabla ushahidi haujakamilika. Kwa mujibu mtoa habari alikuwa anamtetea mpiga kura wake asidhulumiwe ndipo zengwe likaanza.
 
misasa

misasa

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2014
Messages
9,839
Points
2,000
misasa

misasa

JF-Expert Member
Joined Feb 5, 2014
9,839 2,000
Atakuja kupata anachostahili.

Michael Wambura wa TFF alikua mmoja wa watu wanaopenda kesi sana,kitu kidogo tu kakimbilia mahakamani wakaona huyu asituchoshe kapigwa kesi ya utakatishaji fasta tu kakaa ndani karibu mwaka mzima,ametoka na kutakiwa kulipa Tsh.100mil.

Kamuulizeni sasa hivi kama kiherehere cha kupenda makesi kesi bado anacho,akiona mahakama anaipita kwa mbaali bila kugeuka.

dodge
Kabisa mkuu.

Anapenda kununua nyumba,ardhi zinahusiana na kesi bwana Timbww
 
X

X-bar

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
391
Points
500
X

X-bar

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2019
391 500
Mbona unamhukumu kabla ushahidi haujakamilika. Kwa mujibu mtoa habari alikuwa anamtetea mpiga kura wake asidhulumiwe ndipo zengwe likaanza.
Sijamhukumu bali nimemuelezea kutokana na ninavyomfahamu. Lakini kwanini mtoa mada anatetea diwani hana makosa kabla ya vyombo husika hawaja-rule out kama amehusika kweli au la kama anavyosema mwenyewe diwani kuwa anawaachia vyombo husika wafanye kazi yao (kubainisha ukweli)?
 
chagu wa malunde

chagu wa malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
1,021
Points
1,500
chagu wa malunde

chagu wa malunde

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
1,021 1,500
Sijamhukumu bali nimemuelezea kutokana na ninavyomfahamu. Lakini kwanini mtoa mada anatetea diwani hana makosa kabla ya vyombo husika hawaja-rule out kama amehusika kweli au la kama anavyosema mwenyewe diwani kuwa anawaachia vyombo husika wafanye kazi yao (kubainisha ukweli)?
Wote tusubili vyombo vya dola vifanye kazi.
 

Forum statistics

Threads 1,402,707
Members 530,972
Posts 34,403,007
Top