Kijembe cha Spika: Wanaotafuta Uwaziri ni wengi na Waarabu wa Pemba wanajuana kwa vilemba!

Anne(5).jpg

Spika wa Bunge, Anne Makinda

Kuhusu Mawaziri
Spika wa Bunge, Anne Makinda, jana aliwashukia mawaziri baada ya kuwataka kufanya kazi waliyopewa kwani itafika kipindi watageukwa na ukumbi mzima wa Bunge. Aliyasema hayo jana mchana, muda mfupi kabla ya kuahirisha shughuli za Bunge. “Hivyo nyie waheshimiwa mawaziri inawabidi mfanye kazi mliyopewa, itafika mahali mtageukwa na ukumbi mzima.” Alisema wabunge, ambao wanawaunga mkono wapo, lakini ni vizuri na wao (mawaziri) wakafanya kazi zao kwa uhakika. Aliwataka mawaziri kufanya kazi zao kwa kujiamini kwa sababu wamepewa vitendea kazi.

Alisema wiki iliyopita alikuwa katika mkutano wa maspika wanaotoka katika nchi, ambazo ni wajumbe wa Jumuiya ya Madola. Spika Makinda alisema mkutano huo, ambao hufanyika kila baada ya miaka miwili katika moja ya nchi wanachama, ulifanyika nchini Malawi. Alisema katika mkutano huo wamekuwa wakijadiliana kuhusiana na mambo yanayohusu nchi zao na maspika wanashirikiana kupeana uzoefu kuhusiana na mambo wanayokubaliana.

Kuhusu Wabunge

Alisema miongoni mwa mambo waliyokwenda kuzungumza katika mkutano huo ni nafasi ya vyama vya upinzani katika Bunge kuweza kuimarisha demokrasia na kufanya maendeleo ya nchi kuonekana. “Kitu, ambacho napenda kuwashukuru, hamuwezi kuwa wabunge wa Tanzania halafu mkawa wabunge wa CCM, wabunge wa Chadema, wabunge wa NCCR, kwa maslahi ya wananchi hatufanyi sawa. Hivi sasa mlivyoanza mkikubaliana jambo kwamba hili ni la National Interest (manufaa ya taifa), mnasimama kama wabunge wa Tanzania, kitu ambacho ni kizuri,” alisema. “Lakini tuwe na hoja ya msingi ya kuwasaidia wananchi wetu wale wanaotusikiliza. Kwa hiyo, mimi nasema hili lazima tutofautishe. Kwa mfano mnapitisha bills (miswada) za sheria ya nchi haiwezi kuwa sheria ya CCM ama ya Chadema, lazima iwe sheria ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ubaya wake uzungumzwe, uzuri wake uzungumzwe, manufaa kwa wananchi yazungumzwe bila hata kukopesha, tusifanye mchezo usiokuwa na akili nzuri.”

Alisema “Utatungaje sheria ya Chadema, utatungaje sheria ya CCM, hakuna kitu kama hicho mimi naomba kama ile ninayosema networking (mtandao), ni muhimu, ila tuwe genuine (halisi), tuwe wakweli hii ni maslahi ya wananchi ama maslahi ya siasa tu? Haya mambo ya siasa tuna muda mwingi sana wa kufanya huko nje, wapi lakini hapa tutunge sheria zitakazowalinda Watanzania wa leo, wa kesho na wengine na historia itatukumbuka.” Aliwataka wabunge kutofautisha na kwamba wanapofikia katika suala la kitaifa ni lazima kutoa maoni kama wanataka kuwasaidia Watanzania.

(Subheadings imehaririwa na mtoa mada)

IPPMedia
 
ujumbe kwa cdm. walidhani baraza la mawaziri litavunjika halafu iwe serekali ya msto. waoooooooooooooooooooo, wanaona haya

kweli we gamba! unataka kusema makamba na kamati yake ya nishati na madini na wao ni CDM? We ni gamba ambalo pia ni hatari hata kwa magamba wenzio.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Kwa hiyo ndio tuseme kijembe hich chaweza kuwa na sura mbili,moja sura ya wanaccm na nyingine sura ya wanachadema?
 
ujumbe kwa cdm. walidhani baraza la mawaziri litavunjika halafu iwe serekali ya msto. waoooooooooooooooooooo, wanaona haya

Serikali ya mseto haiwezi kuja bila kufanyia marekebisho vifungu vya sheria mama (Katiba). - hilo moja.
Lakini pia, kama umekuwa mfuatiliaji mzuri wa hii bajeti ya Nishati na Madini utakumbuka wabunge walioongoza kwa kuikataa walikuwa ni wa ccm. Na hata barua ya Jairo ilitolewa na mbunge wa ccm - Mh Beatrice Shellukundo (Kilindi). Madai kwamba 'cdm' (nadhani ulimaanisha CHADEMA) wananyemelea serikali ya mseto ni uzumbukuku. Hoja zako nyingi tangu umeingia hapa jamvini zimejikita zaidi kwenye uzushi. Jitahidi kulinda heshma yako wewe na hao unaowawakilisha kwa kuleta hoja zenye mashiko.
 
Hivi kuna mbunge asiyetaka kuwa waziri au hata cheo kikubwa zaidi? Maana nzima ya kuwa mwanasiasa ni kutafuta madaraka na kuya shikilia. Sasa kuna ubaya gani mbunge akitaka uwaziri?
 
Hivi kuna mbunge asiyetaka kuwa waziri au hata cheo kikubwa zaidi? Maana nzima ya kuwa mwanasiasa ni kutafuta madaraka na kuya shikilia. Sasa kuna ubaya gani mbunge akitaka uwaziri?

Ubaya ni implication alioitoa kwamba jamaa walikataa hii bajeti sio sababu ya maslahi ya wananchi bali kwa tamaa ya madaraka.
 
Ubaya ni implication alioitoa kwamba jamaa walikataa hii bajeti sio sababu ya maslahi ya wananchi bali kwa tamaa ya madaraka.

Hakuna jipya hapo mkuu. Siku zote ndivyo walivyo. Sasa itanishangaza kama speaker kagundua hilo leo baada ya kuwepo kwenye ulingo wa siasa miaka yote hii.
 
Hakuna jipya hapo mkuu. Siku zote ndivyo walivyo. Sasa itanishangaza kama speaker kagundua hilo leo baada ya kuwepo kwenye ulingo wa siasa miaka yote hii.

Hivi kuwa mbunge ni wito wa kutetea wananchi au ni ngazi ya kupata vyeo vingine vikubwa (hata kama ni hivyo hio ni siri yao na kama kuna proof mtu anafanya kazi zake kwa maslahi binafsi na sio kwa kutetea wananchi basi huyo kiongozi hafai....) na mtu akikwambia hivyo hakupi sifa bali anakutukana.
 
Mkuu mimi nakubaliana na wewe wala sija kubishia. Nasema tu kwamba hilo Makinda alilo point out ni kitu obvious sana ambacho watu wenye uelewa wanafahamu. Everything a politician does is in order to gain power awe wa CCM au Chadema, Tanzania au Marekani. Hiyo ya kusaidia wananchi comes second. Ni wachache sana ambao wanakua na nia ya dhati ya kusaidia wananchi na watu kama hao n nadra sana kudumu kwenye siasa.
 
Kauli kama hiyo ndiyo tunayoitaka kwa mkuu wa mhimili muhimu wa bunge badala ya kuendekeza uchama ndani ya mhimili huu. Tunafuatilia kwa makini yatakayoendelea. Maana anayoyafanya Ndugai yanachefua mno afadhali na huiyu mama ameanza kufunguka akili na kutetea nafasi yake kihistoria isijemharibia. Akifanya alichosema ni hakika atajitengeneza historia yake.
 
namshukuru na kumpongeza kwa vision ayake hii mpya, sasa asiishia hapo tu, ajitahidi kuondoa double standards wakati wa mijadala anayoiongoza na kuwadhibiti naibu wake na wenyeviti wa bunge nao wawe neutral wanapoongoza vikao vya bunge
 
That is true. Kwa vision hii anayoanza kuonyesha ni dhahiri anaweza kuturudishia imani ya kuweka historia ya Spika wa kwanza mwanamke nchini, maana mtangulizi ndiye mtengeneza mazingira mazuri ya watakao mfuata. Katika hili bila kinyongo nampongeza Spika Makinda na kusubiri utekelezaji wake.
 
Its too late, every one is now aware of her callowness on translating laws. It's enough to say that she fortuitously found herself in that chair but she holds no credentials and not in the same league with her predecessor.
 
Not really too late. Huu ni mwaka wa kwanza wa utumishi wake kuendesha mhimili huu. Tunatakiwa tuwe watu wa mawazo chanya katika jema tumpongeze na hii itampa moyo wa kufanya kazi yake kwa kujiamini zaidi kwa vile tunaona mazuri anayoanza kuyaamini katika kazi yake. Amesoma alama za nyakati pamoja na kupata ushauri wa kufaa na kubadilishana uzoefu na speakers wengine. Tutarajie mabadiliko kidogo ingwa si kwa kasi sana maana damu nzito kuliko maji.
 
Back
Top Bottom