Kijasusi tunajifunza nini kuchapwa kofi kwa Rais wa Ufaransa?

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,850
2,000
Tukio la kushambuliwa kwa makofi Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron linatupeleka mbele na kulazimika kujifunza mambo machache anuawi katika uwanda wa Ujasusi ulimwenguni. Nimeliangalia katika pande nyingi na sasa ninaweza kulichambua kwa sehemu fulani ili kusherehesha na kufunza walinda viongozi wetu. Kabla sijachambua tukio hili kupitia video hii, naomba nielezee nadharia kadhaa za kiusalama na ulinzi ambazo ndizo msingi wa kufikia hapa katika tukio hili.

Duniani kwanza kuna Usalama na Ulinzi haya mambo mawili yanafanana lakini yanatofautiana katika medani, Usalama ni katika msingi wa "taarifa" na ulinzi ni katika msingi wa "udhibiti" baada ya kupata taarifa. Hivyo katika ujasusi kinachotangulia ni Taarifa ndipo ulinzi uwepo. Na huo ndio msingi mkuu wa Jina la Tanzania Intelligence and Security Services (TISS). Huwezi kuanza na Security kisha intelligence. Itakuwa sawa na kumeza kabla ya kula.

Sasa kwenye eneo la ulinzi wa viongozi kwa mjibu wa taaluma ya Executive Protection, Kama kiongozi anatembea kwa miguu ni kwamba idadi yoyote ya watu wanaomlinda kiongozi husimamiwa na mtu mmoja ambae yeye ndie huwaongoza kwa kila hatua,

Na nadharia hii inakazia kuwa kama kiongozi (Angel's) anatembea kwa miguu walinzi hawa watatakiwa kumweka hatua moja nyuma ya mstari wa mbele, hii inamaana kwamba, kama kiongozi analindwa na watu sita, wawili watakaa nyuma ya kiongozi (Angel's), wawili watakaa pembeni (kulia na kushoto) mwa kiongozi huyo, na wawili watakaa mbele kidogo ya kiongozi huyo kwakufuata mstari wa wale wawili wa pembeni ili kutomziba kabisa kiongozi asione mbele.

Mtu wa saba ambae anaweza kuwa kuwa katika msafara huo wa miguu ama anaweza kuwa katika gari la mitambo ya kuongozea msafara hii inategemeana sana na teknolojis mnayoitumia katika kikosi husika cha ulinzi. Kama mnatumia Walkie Talkie Radio Frequency (WTRF) hii inamaana controller sio lazima awe katika gari bali, lakini huyo ndie atakuwa na protocol yote ya msafari, na katika hili huyu ndie atafahamu kwamba Rais atasalimiana na nani, atasimama wapi na atatembeaje. Ifahamike na kuheshimika kwenye muundo huu wa ulinzi Rais hana mamlaka ya kubadilisha mwelekeo wowote bila idhini ya kiongozi wa ulinzi, bali rais anaweza kuchukua hatua zozote pale atakapogundua kuna hatari juu yake na walinzi wake hawajaiona ama wameiona na kuipuuza kwa maksudi.

Dhana hii pia iko katika majeshi ya vita, kwa nchi za kijamaa (Chinese styles) anayepiganisha vita (mtaalamu wa ramani ya vita) maranyingi walikuwa ni Maluteni Kanali, hawa ndio walikuwa uwanja wa vita. Lakini Tanzania tukiwa katika ujamaa katika vita vya Uganda, Mbinu zilibadilika na vita vikapiganwa kwa muundo wa kibepari ambapo Mabregedia ndio walipiganisha vita katika uwanja wa vita. like Mzee General Lupogo, Mzee General Kiwelo, Mzee General Mkisi nk). Kwamiaka ya karibu alijizoelea sifa sana Luten General Mwakibolwa hasa kwa staili yake (yakipekee) alipoongoza vita vyakuwazima M23 kule Kongo.

Sasa tukirejea katika video hii nimebaini mapungufu kadhaa ambayo nafikiri hadi leo waliohusika watakuwa wameshachukuliwa hatua, nikimaanisha kikosi cha ulinzi wa rais na mkuu wao. Kwanza inaonyesha Rais aliponyoka toka kwenye mikono ya Controller anayeongoza msafara wake na kuamua kukimbia hovyohovyo kufuata walipo raia ili akasalimie.

Kitendo hiki naweza kukitafsiri kuwa rais alikuwa na mtazamo wa kisiasa kuelekea siasa za Uchaguzi zijazo huko kwao na kwamba kutokeza mbele ya watu na kuwasalimia kwa kuwashika mikono kulikuwa na maana kwenye akili ya Macron na siasa za Paris japo matokeo yametoka sivyo kwa jicho letu huku Afrika, lakini kwa siasa za Paris hili laweza kuwa turufu muhimu sana. Hili maranyingi huwa linatokea kama rais ni mbishi hasikilizi walinzi wake. Na hili naliona kwenye video hii kwamba licha ya rais kuokolewa na mlinzi lakini aligoma kwenda kwenye gari badala yake alirudi kwenda kumsuta aliyempiga kofi.

Pili nafikiri ama muongoza ulinzi kwa maksudi ambayo hayamithiriki aliamua kuwanyamazia walinzi wenzake wanaomuongoza Rais na hivyo uelekeo wa rais kwenda kwa raia bila kujiridhisha kwamba anaosalimiana nao ni watu salama waliamini ni sahihi. Lakini dhana hii inakinzana kutokana na kwamba rais ametoka kwenye gari anaonekana ana walinzi wanne waliovaa suti, anachomoka mbio akiongozana na walinzi wawili hadi anafika kusalimia raia na anachapwa kofi ndipo hawa walinzi wengine wawili wanakuja mbio kusaidia kuokoa.

Nadharia kuu zote mbili zinaweza kuwa sio sahihi na badala yake ikahesabika kuwa ni ajali ya kirais, lakini maswali ni mengi huku dhana ya ulinzi ikiwa inakinzana kabisa na namna tukio hili lilivyotokea. Ingawa kwa maoni yangu dhana ya kwanza ina nguvu zaidi.

Jibu lipo kwa Mtikila.

Kwaundani zaidi kuelewa haya na mengineyo Soma kitabu cha Ujasusi

WAHI OFA MAALUMU.

1. Kitabu: Mtu baada ya Mtu, OFA ni 20,000 badala ya 80,000/=

2. Kitabu: Ujasusi, OFA ni 20,000 badala ya 80,000/=

Nunua kwa:

TigoPesa 0715865544
M-Pesa 0755865544
Airtel Money 0788887887
HaloPesa 0624452045
(Yericko Nyerere)

Tuma majina yako na ulipo

(Dar ni free delivery)

Nje ya Dar nauli 8,000/=

 

T14 Armata

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
4,260
2,000
Yeriko nilikwambia mwaka jana hivi vitabu vyako kutwa promotion, kwanini usiwe na bei moja? je walionunua kwa bei ya 80,000 utawarudishia? uza elfu 20 tosha kuliko kuyumbisha watu. Nakumbuka uliahidi haitatokea lakini ukarudi kule kule
Hii ni pricing policy mbovu sana ambayo wateja wa kudumu huwa inawapoteza au inawafanya wasubirie bei zishuke. Hizi mambo zifanyike kwa wauza mboga ambao ikifika jioni zinapoteza ubora na zikilala haziuziki, ila sio kwa kitabu ambacho miaka nenda rudi ni kile kile.

Sasa unatokaje kwenye 80,000 mpaka 20,000 within a decade na hakuna deflation? Aliyenunua kwa 80,000 ukitoa kitabu tena let's say kwa 60,000 hanunui anajua utashuka mpaka 15,000. Discount hutolewa kwa % ndogo sio kama hivi. Vigumu kuwa best seller kwa namna hii.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom