Kijana Yunus Mtopa aondoka na kitita cha dola elfu tano za STATOIL Tanzania

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,500
3,481
k1.jpg

Mshindi wa Shindano la Mashujaa wa Kesho lilihusisha vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 25 kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi, Yunus Omary Mtopa, akionekana ni mwenye furaha sana baada ya kujinyakulia kitita cha dola elfu 5, kwa kuonekana wazo lake la Biashara ya Miwa kuwa bora zaidi ya wenzake. Hafla ya shindano hilo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, katika Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es salaam.

Mwaka huu shindano hili lilivutia vijana zaidi ya 400 ambao waliwasilisha mawazo ya biashara zao zinazolenga sekta mbalimbali za uchumi kama kilimo, ufugaji, mawasiliano, na biashara nyingine ndogondogo. Vijana waliruhusiwa kushiriki mmoja mmoja au hata kuunda vikundi vya watu wawili mpaka watatu
k2.jpg

Jaji Mkuu katika Shindano la Mashujaa wa Kesho lilihusisha vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 25 kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi, Dkt. Neema Muro, akitoa maelezo mafupi ya washiriki wa shindano hilo kabla ya kumtangaza mshindi.
k3.jpg

Sehemu ya Wageni mbali mbali waliohudhulia hafla hiyo, wakiwa makini kumsikiliza jina la Mshindi wa Shindano la Mashujaa wa Kesho lilihusisha vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 25 kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi, katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, katika Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es salaam.
k4.jpg

Mgeni rasmi katika Hafla ya kumtangaza Mshindi wa Shindano la Mashujaa wa Kesho lilihusisha vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 25 kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bengi Issa, akikabidhi mfano wa hundi kwa Mshindi wa Shindano hilo, Yunus Omary Mtopa.
k5.jpg

Mgeni rasmi katika Hafla ya kumtangaza Mshindi wa Shindano la Mashujaa wa Kesho lilihusisha vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 25 kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bengi Issa (wa nne kulia), Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanna-Marie Kaarstad (wa pili kushoto), Meneja Mkazi wa Kampuni ya Statoil Tanzania, Øystein Michelsen (shoto) wakiwa katika picha na washiriki wa shindano hilo.
 
Mshindi alieleza kuwa wazo lake ni kufanya.kitu gani? Tupe japo kwa ufupi ili pia.itupe hamasa zaidi na kujifunza pia
 
hongera sana kijana. hata mm nilishiriki kuandika wazo la biashara, ila sikufanikiwa kuingia 40 bora. hongera sana kijana.
 
Back
Top Bottom