Kijana wangu anakesha kwenye games analala alfajiri

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Nikiwa kama mzazi, nililea watoto kwa msaada wa dada huku nikiwa na majukumu mengine. Mtoto wangu wa kiume alipenda gadgets na kila siku yake ya kuzaliwa alichagua game au play station mpya. Kwakua alikuwa na bodi shuleni niliona hii ni kama asante yake ya kuitendea vyema ada tunayolipa na Baba yake.

Sasa yuko chuo anaingia mwaka wa pili. Chuo chao kilifungwa tangu March mwaka huu kwaajili ya corona lakini walipata online lectures na walituma kazi zao huko huko online.

Tangu aache kwenda chuo amekuwa ni mtu wa kujifungia chumbani kwake tu. Nilitumia nafasi hii kumlipia mafunzo ya udereva. Hii ilimhamasisha alikuwa na hamu ya kujua kuendesha gari. Tangu apate leseni amerudia tabia zake za zamani.

Mtoto anakesha kwenye michezo mpaka asubuhi. Huyu atakua raia wa aina gani? Ana miezi miwili ya kukaa nyumbani mpaka September atakapo rudi chuoni. Siku nifanye nini kukomesha hii tabia?
 
Madam, “An idle mind is the devil's workshop”. Shukuru Mungu anakesha kucheza GAME. Watoto wa wengine, kipindi hiki wanawashangaza wazazi wao kwa kufanya vitu vya hovyo.

Ulipomtafutia mafunzo ya udereva kwa sababu alikuwa na hamu ya kujua kuendesha gari, yale mabadiliko ndio somo.

Mtafutie kingine anachopenda na wewe unapenda akifanye, au mtambulishe kwenye kipya ambacho ni wewe unapenda afanye ili kama atakipenda umuache afanye.

Tofauti na hapo, chagua kwenye ambavyo anavipenda Japo wewe huvipendi ila kiko afadhali ya usivyopenda acheze Game muda mrefu.

Hakikisha kama hujui anapenda nini. Mtafute anayemjua vizuri akwambie. Usilazimishe mambo.

Japo huwa una vielement vya UCHADEMA na mimi siyo Mwana CCM sisi ni ndugu.

I hope itasaidia.
 
Shukran 🙏🏾
 
Mtoto habadilishwi kwa kumfanya apende anavyopenda mzazi, bali ni kwa anavyopenda yeye.

Ndio maana shule za kindergartens kwa watu weupe huwa zina michezo Mingi ya kitoto na vitu vya kuwavutia. Ili shule iwe ni miongoni mwa maeneo wanayoyapenda.

Huku kwetu huwa tunawapeleka shule kwa fimbo.
 
Kikubwa ni uliishawahi kuongea nae kuhusu Hilo? Pia mtazomo wake kuhusu maisha unaujua? Ukitoa Hilo linalokusumbua kuhusu yeye ana potential unayoiona? Muhimu unaona hilo litasumbua future yake? Baba yake nae Yuko aware na Hilo? Talk to him as a mother, but do it with love. Mimi pia nilikua na shida hio, Ila mama yangu alikaa na mimi na akanijenga Sana katika shida hio. Wewe ni mtu mzima Sana kunizidi sababu una mtoto tunaendana umri. Fanya ujue mtazomo wake kuhusu maisha. Hilo ni muhimu
 
Tumesha ongea nae sana, tukiwa na baba yake haikusaidia
Mnambembeleza kupitiliza. Hapo MAWILI ama achague kusikiliza ninachosema au akaishi huko kwenye hizo games. Mtoto hata umkaangie debe la mayai usidhani unamsaidia fikiria siku haupo duniani.
NB: Mimi nampenda Sana mwanangu Ila akizingua anapata bakora za kumtosha nikirudi tunafanya wote homework (yupo primary) usiku wakat mwingine hadi saa 7 wakat namalizia kazi zangu.
 
Vijana wengi tu wapo hivyo miaka hii. Hasahasa wale wanaopenda gadget & Internet.

Kiasi fulani inaathari kwake kwa maana kwamba hatakuwa free sana kusocialize na watu wake wa karibu kwasababu anahisi wahafikirii kama yeye. Trust me vijana wa namna hii most of them wana element za ujiniasi.

Kuwa na uwezo mkubwa wa concentration ni akili kubwa.

Lakini hiyo haimaanishi ndiyo amefanikiwa maisha. Kwasababu kwenye life inabidi ukutane na “real people” in real life ili uwe member kamili katika jamii.

Kwa sababu inaonyesha uko na pesa kiaina na yeye anapenda Private life (amefika chuo mkubwa huyo) muulize nini anahitaji ili afanikiwe zaidi. Huu ni mwanzo.

Taratibu utaanza tena kuwa na influence positive kwake.

Wazazi sometimes mnazingua mnadhani kwasababu eti wewe ni baba au Mama basi unaweza kuniambia kila kitu na mtoto asikilize tu kama nyumbu

Watoto wenye IQ kubwa lazima ata rebel tu.

Ili uweze ku-influence life yake inabidi kwanza uonyeshe una-support life yake .

Kwasababu watoto maginiasi wanawajua wazazi wazushi

Ni hayo tu Sky Eclat, I think you are amazing woman, great citizen of this country, supportive wife to your husband and a loving mother to your children.

Nilitaka tu nikuonyeshe upande mwingine jinsi watoto wa namna hii wanavyofikiri ndani ya medulla 🧠 zao.
 
Kwani kunashida gani kama anatimiza majukumu yake vizuri, Mimi menyewe siku nisipo enda kazini nakesha ama kushinda nikiangalia movies, ndio kilema changu siezi ku socioliz na watu, nimejaribu kuacha hii tabia lkini nimeshindwa.
 
Malezi yako yalikuwa mabovu tangu awali pole, games ni ugonjwa mbaya ukiunza hata masomo utakuwa hufaulu vizuri
 
Sasa kama mamaake unakesha jf kuendekeza siasa na kuwatetea kina Mbowe unategemea uwape watoto wako malezi bora kweli?

Na uhakika hapo ulipo wewe ni single maza, maana hakuna mwanaume atakubali kukaa na mwanamke anaekesha kuwatetea kina humu jf!
 
Vijana wengi tu wapo hivyo miaka hii. Hasahasa wale wanaopenda gadget & Internet.

Kiasi fulani inaathari kwake kwa maana kwamba hatakuwa free sana kusocialize na watu wake wa karibu kwasababu anahisi wahafikirii kama yeye. Trust me vijana wa namna hii most of them wana element za ujiniasi.

Kuwa na uwezo mkubwa wa concentration ni akili kubwa.

Lakini hiyo haimaanishi ndiyo amefanikiwa maisha. Kwasababu kwenye life inabidi ukutane na “real people” in real life ili uwe member kamili katika jamii.

Kwa sababu inaonyesha uko na pesa kiaina na yeye anapenda Private life (amefika chuo mkubwa huyo) muulize nini anahitaji ili afanikiwe zaidi. Huu ni mwanzo.

Taratibu utaanza tena kuwa na influence positive kwake.

Wazazi sometimes mnazingua mnadhani kwasababu eti wewe ni baba au Mama basi unaweza kuniambia kila kitu na mtoto asikilize tu kama nyumbu

Watoto wenye IQ kubwa lazima ata rebel tu.

Ili uweze ku-influence life yake inabidi kwanza uonyeshe una-support life yake .

Kwasababu watoto maginiasi wanawajua wazazi wazushi

Ni hayo tu Sky Eclat, I think you are amazing woman, great citizen of this country, supportive wife to your husband and a loving mother to your children.

Nilitaka tu nikuonyeshe upande mwingine jinsi watoto wa namna hii wanavyofikiri ndani ya medulla 🧠 zao.

Mkuu tabia hizo unazosemannadhan ziko applicable kwa wenzetu .. dunia ya 3huku mbona Kama unakuwa mtumwa tu..!unajikuta unalost
 
Back
Top Bottom