Kijana wa miaka 23 amwangusha Waziri; Ni Chikawe aliyepoteza U-NEC Nachingwea Ageuka Bubu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kijana wa miaka 23 amwangusha Waziri; Ni Chikawe aliyepoteza U-NEC Nachingwea Ageuka Bubu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Oct 6, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145  JUMAMOSI, OCTOBA 06, 2012 08:24 NA MWANDISHI WETU, NACHINGWEA

  *Ni Chikawe aliyepoteza U-NEC Nachingwea
  *Ageuka bubu, agoma kuzungumza na mwandishi
  *Kijana aliyeshinda aanguka, apoteza fahamu
  *DC aliyechapa walimu Bukoba aibuka kidedea

  WIMBI la mawaziri na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kushindwa katika chaguzi ndani ya chama hicho, limeendelea kushika kasi, baada ya Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, kupigwa chini na kijana mdogo mwenye umri wa miaka 23, kwenye nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).

  Waziri Chikawe ambaye pia ni Mbunge wa Nachingwea, aliingia katika uchaguzi kwa kujiamini, lakini alijikuta akiambulia kura 520 dhidi ya 780 za Fadhili Liwake.

  Akitangaza matokeo hayo, msimamizi wa uchaguzi huo, Zakinai Msongo alisema, matokeo hayo ni halali kutokana na wajumbe kutumia haki yao ya msingi.

  "Ndugu wajumbe napenda kuwatangazia matokeo haya, baada ya kazi kubwa mliyoifanya tangu asubuhi, mshindi wetu ni Fadhili Liwake, ambaye amefuatiwa na Mathias Chikawe na Fadhili Mkuchi, ameshika nafasi ya tatu," alisema.

  Baada ya kauli hiyo, ukumbi mzima uliibuka kwa shangwe na kuacha Waziri Chikawe na wapambe wake wakiwa hawaamini kilichotokea.

  Lakini katika hali ya kushangaza, baada ya msimamizi wa uchaguzi kutangaza matokeo hayo, Liwake alianguka chini na kupoteza fahamu ghafla.

  "Huwezi amini ndugu yangu, baada ya kutangazwa mshindi, Liwake alianguka ghafla na kupoteza fahamu, jambo hili limeshangaza wajumbe waliokuwa ukumbini," alisema mmoja wa wajumbe wa mkutano huo.

  Baada ya kuanguka, alikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Nachingwea kwa ajili ya matibabu.

  "Tumemkimbiza mshindi wetu hospitali kupata matibabu, watu hawaamini kilichomtokea, lakini tunamuomba Mungu amsaidie apone haraka, ili aanze majukumu yake mapya," alisema mjumbe huyo.

  WAZIRI CHIKAWE

  Katika hali ya kushangaza, Waziri Chikawe alipopigiwa simu na gazeti hili, alijibu kwa jeuri na kusema, "wewe nani, sikujui hujawahi kukutana na mimi, unataka niseme nini, mimi ni kiongozi wa Serikali bwana, najua taratibu," alisema Chikawe kisha akakata simu.

  Katika hatua nyingine, Msongo alimtangaza aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba (DC), Albert Mnali kuwa Mwenyekiti mpya wa CCM Wilaya ya Nachingwea, baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi huo kwa kupata kura 943.

  Itakumbukwa mwaka 2009, Mnali alifukuzwa kazi na Serikali, baada ya kuamuru polisi kuwachapa walimu tisa viboko, wanatoka Shule ya Msingi Katerero, 11 wa Shule ya Msingi Kanazi, ambao walichapwa viboko viwili kila mmoja na walimu 12 kutoka Shule ya Msingi Kansenene walichapwa viboko vinne vinne kila mmoja.

  Mnali alisema, alilazimika kuwatandika viboko walimu hao, baada ya kugundua kuwepo uzembe kazini, ikiwemo kuchelewa kufika kazini na kutofundisha kama mikataba yao ya ajira inavyoeleza.

  Alisema uzembe huo, umesababisha Wilaya ya Bukoba kuwa ya mwisho kimkoa, katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba na kuwa uamuzi huo utasaidia kuwakumbusha walimu wajibu wao.

  KAHAMA

  Habari kutoka Kahama, zinasema katika hali ya kushangaza, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Wilaya Kahama, Mipawa Ng'wanagolelwa (49), aliangua kilio baada ya kuangushwa na kijana mdogo Masoud Melimeli(31).

  Katika uchaguzi wa kiti hicho, ambacho kilivuta hisia za watu, Ng'wanagolelwa alitoa machozi hayo wakati akieleza hali ya uchaguzi ilivyokuwa muda mfupi, baada ya matokeo kutangazwa.

  "Mimi ninashangaa wanachama wa CCM kunizomea, baada ya kutangazwa

  Matokeo, hali hii imenisikitisha mno," alisema.

  Katika uchanguzi huo, wajumbe walishuhudia Melimeli akimbwaga gwiji huyo, kwa kupata kura 117, huku mpinzani wake akipata kura 125.

  NJOMBE

  Ludewa nako habari zinasema, mgombea wa nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Zephania Chaula, amekata rufaa ya kupinga matokeo kwa kile kilichodaiwa kutotendewa haki, kutokana na kanuni kukiukwa.

  Akizungumza na MTANZANIA, Chaula alisema amefikia uamuzi huo, kwa sababu matokeo hayakuwa sahihi.

  "Kitendo cha kufanyia uchaguzi nje ya eneo husika, kiliwafanya wajumbe kubaki wakishangaa na huku baadhi ya viongozi ambao waliwania nafasi hiyo, majina yao hayakurudi.

  "Tumeanza uchaguzi kwa mizengwe mikubwa, nikapata kura 521 na mpinzani wangu 522, huku wa mwisho alipata kura 22, jambo lililowafanya wajumbe kubaki wanalalamika kwa mizengwe," alisema.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  Nimependa kijana wa Miaka 23 kaondoa FISADI wa MIAKA mingi... sometimes CHANGE comes from WITHIN !!!
   
 3. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  M4C ni hatari kwa waliodhani kuwa wana haki miliki na siasa za nchi hii. Kijana wa miaka 23 kumpiga chini mtu mzima wa nchii ni ishara tosha kuwa kavla ya kuufikia uchaguzi ujao Chama cha Mapinduzi inabidi kiukutane katika vikao vya kukibadilisha kutoka katika cha chetu cha jenga nchi na kuwa chama kinacho kwenda na wakati kwa kutumia ishata za nyakati.
  Ni aibu kubwa waziri mtu mzima kama Chikawe kupigwa chini na kijana mdogo hivi. Hii inaobesha kuwa ingawa ni mbunge wa wananchi lakini huenda alitumia nguvu nyingi kumwingiza kwenye ubunge bila ridhaa ya wana Nachingwea.

  Na hii ni aibu kubwa kwa chama chake na hata kwa mheshimiwa wake mwenyewe maana unaweza hivi huyu akiendelea kuwa waziri Chama kinapata faida gani kupitia kwa wapiga kura wake na huku hawamtaki?

  Wallah, Ukicheka cheka na nyani unakaribisha kuvuna mavua shambani.
   
 4. G

  GENERARY Member

  #4
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 31, 2012
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Bora mafisadi waanze kuenguliwa huko huko. Aibu yaoooooo!!!!!!
   
 5. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  hoja zako nzuri sana lakini kiswahili chako ovyo kabisa,kwanini usiwe una proof read kabla ya ku post.,
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  mafisadi kwishnehi wajiengue wenyewe kabla ya M4C haijawaondoa
   
Loading...