xpl0it
Senior Member
- Feb 21, 2014
- 124
- 88
Mamlaka za Japani zimeshikilia kijana wa miaka 14 Osaka, mji wenye bandari kubwa, kwa kutengeneza na kusambaza kirusi aina ya ransomware.
Hii ni mara ya kwanza kwa Japani kukamata watuhumiwa wenye makosa ya aina hii.
Ransomware ni kipande cha malware kinachofunga mafaili kwenye kompyuta ya muathirika na kuyafanya yasipatikane hadi muathirika atakapolipa fidia, kawaida katika Bitcoins, kwaajili ya kupata funguo za kusimbua(decrypt) mafaili hayo yaliofungwa.
Ransomware zimekuwepo kwa miaka michache, lakini kwa sasa zimekuwa tishio kubwa katika ulimwengu wa kiteknolojia kwa biashara na watumiaji kutoka pande zote za ulimwengu.
Mwezi mmoja tu uliopita, WannaCry ransomware iliharibu zaidi ya kompyuta 300,000 ndani ya masaa 72 tu, na kuleta taharuki ulimwenguni.
Kukamatwa kwa mtuhumiwa hivi karibuni kumekuja baada ya kijana, ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa high school, alitengeneza kirusi cha ransomware na kupakia(upload) source code yake kwenye internet, kutokana na chombo cha habari cha Japani.
Mwanafunzi huyo ambaye alikiri kwa tuhuma hizo, aliunganisha program ya kufunga(encrypt) ya bure kutengeneza maambukizi ya ransomware yake na hivo kuzipakia kwenye tovuti ngeni na hata kuwafundisha watu kuipakua(download) na kuitumia kusambaza zaidi kwaajili ya kujipatia fedha.
Kijana huyo pia alitangaza tovuti yake kupitia mitandao ya kijamii, ukijumlisha Twitter, akiwaambia watumiaji "Nimetengeneza ransomware. Jisikie huru kuitumia," vyanzo vilisema.
Kutokana na police wa kijapani, ransomware wa kijana huyo ilimruhusu mpakuaji kuathiri kompyuta za waathirika, wakidai malipo katika mfumo wa sarafu za kidijitali. Framework ya ransomware yake imepakuliwa zaidi ya mara 100.
Mamlaka hayo hayajafichua utambulisho wa kijana, lakini vimetaarifu tu kwamba mwanafunzi huyo alichukua karibia siku 3 kutengeneza program hiyo ya ransomware akitumia tarakilishi(personal computer) yake.
Mwanafunzi huyo aliziambia mamlaka kwamba alijifunza kutengeneza program kipeke yake na alitengeneza ransomware huyo kutokana na hamu yake ya kufaamika.
Polisi wa kijapani walishtukia ransomware huyo wakiwa katika "cyber patrolling" mwezi Januari na kuichukua tarakilishi ya kijana huyo baada ya kuchunguza nyumba yake mwezi April.
Unachochote cha kuchangia kuhusu taarifa hii? Andika katika nafasi iliyoachwa apo chini...