Kijana wa kisasa unatakiwa uwe na hivi vitu

Kwanza uwe na Bible au Quran
Then uwe na amani moyoni

The rest vina maana kama huna, ukishavipata utaona havina maana
 
Habari za usiku wadau wa JF na poleni na mihangaiko ya maisha yenu. Hakika mungu atawapa rehma zaidi.

Niende moja kwa moja kwenye mada.

Maisha yamebadilika sana tena sana, wasomi ni wengi, wasiosoma pia ni wengi lakini mbaya zaidi fursa za kiuchumi ziko shared kwa pande zote mbili hizo. Sasa basi kutokana na maisha kubadilika niko na mambo au vitu kadhaa ambavyo kijana wa kisasa anatakiwa kuwa navyo angalau anaweza kushindana katika nyanja mbalimbali kupitia sifa za ziada hizi.

1. LESENI YA GARI
Kijana anayejitambua lazima awe na angalau leseni ya gari hata iwe class A, D poa tu. JIFUNDISHE GARI ni muhimu sana. Yes leseni hukutofautisha sana na vijana wengi, hapa hata ukipata kazi kampuni au taasisi wanaweza kukuajiri kwa sababu tu gari unajua hivyo utawapunguzia gharama za kuajiri dereva. Leseni/kujua gari pia inaweza kukusaidia pindi itokeapo dharua njiani umepakizwa na mtu uliyefatana nae ameshindwa kudrive unaweza msaidia ili kupata msaada. LESENI NI 70,000/= kwa miaka 5. Gharama zingine ni lena 10,000 na testng fee 3000 kwa kila daraja. Punguza mambo yasiyo na msingi na ujipatie leseni yako.

2. PASSPORT YA KUSAFIRIA
Yes unaweza ona kama kitu kidogo ila ni very potential kwa vijana hasa watafutaji wa maisha. Asikwambie mtu maisha yanatofautiana kati ya nchi na nchi hivyo passport inaweza kukusaidia kwenda nchi nyingine zenye unafuu wa maisha kuliko hapa Bongo. Lkn pia hata uombapo kazi unaweza pata advantage kama ukiwa na passport kwamba unaonekana mtu unayejitambua na unayekwenda na wakati.
Passport pia inaweza kukusaidia kama dhamana sehemu mbalimbali. Kijana wa kisasa lazima uwe na PASSPORT maana hata kibiashara UG huwezi linganisha na BONGO. Passport gharama zake ni 150,000 kama inazidi hapo ni zile indirect cost kama usafiri wa kumtafauta mwenyekiti nk. Hakikisha unaipata na inawezekana.

3. CHETI CHA LUGHA
Ndio ni cheti cha lugha moja muhimu hapa duniani. Achana na ENGLISH maana kwetu kiingereza ni second language. Tafuta lugha nyingine uimudu vizuri (spanish, french, arabic, chinnese, portuguese nk) tafuta moja hapo jifundishe utakuja kunishukuru baadae. Ndio ni muhimu kujua lugha za kidunia kwa maana hujui kesho yako kupitia ujuzi huo unaweza pata ajira mbalimbali hata hapo UHAMIJI, POLISI, JWTZ, POLISI na TISS ukiwa na uwezo wa kuzungumza lugha moja wapo ya hizo ww unakuwa potential kwao. Kwa kijana nakushauri jiongeze kwa kujifunza hizo lugha na inawezekana.

4. UFUNDI WOWOTE ULE
Ndio kijana lazima ujue hata ufundi wa kushona viatu. Sio kila kitu wewe unapeleka kwa fundi lazima uwe smart kutengeneza au kurekebisha kitu chochote ikiwa ufundi saa, ujenzi, computer nk. Hii inakusaidia hata uwapo kazini unaongeza thamani yako. Mfano kazini kwetu kuna intern anajua kutengeneza printer balaa ingawa hakusomea bt yuko vizuri kiasi kwamba anaongeza thamani yake.

5. UWE NA ABC YA YANAYOENDELEA DUNIANI JUU YA FANI NK (UHASIBU, UALIMU NK)
Ndio lazima ujue kitu kipya katika fani uliyosomea maana mambo hubadilika kila leo mfano kwenye uhasibu zamani hatukuwa na accrual basis tulitumia only cash basis lkn miaka 20 hii hiyo kitu ipo hivyo ni muhimu sana kujiupgrade katika carrier yako hata usaili huuliza zaidi mambo yanayotukia sasa hivi.

Kwa leo niishie hapa. Niwatakia sikukuu njema na niwakumbushe kesho ni siku ya kazi.

Ahsanteni.
Kijana wa kisasa unatakiwa uwe na chanzo cha kudumu cha mapato.....hayo mengine yanakuja.....chanzo cha mapato ambacho hata kama ukipata ajali leo ukapata ulemavu wakudumu........pesa inaendelea kuingia
 
Usisahau upige mashine mademu wenye nyota kali ili uonekane

Sasa weye gonga kina mwajuma ndala ndefu walisha logwa kitambooooooooooooo!
 
Asante sana kwa nondo hizi mkuu. Nitaanza na driving licence, then passport and the rest will follow.
 
Mimi sina leseni wala nin na ajira nimepata sehemu nzuri tu nikitaka gari hata msharaha wa miezi mitatu nanunua na sina mpango wa kununua gari na mafoleni ya dar lazima niwe na business na nyumba kwanza kwa vile bado mdogo mno miaka 25 sina papara watu wameenda na maleseni yao kwa interview wamechezea cha mbavu kiukweli mimi nimkulia famili ya kimaskini siwezi kupapukia magari kwa fasta maana naona kama linahitaji malezi kama mtoti
Wewe kwenye ufahamu wa maisha bado sana kijana fikira za kimaskini ziache, fanya what is trending. Mtoa mada katoa nondo nzuri sana.
 
Back
Top Bottom