SISIS
JF-Expert Member
- Jan 14, 2019
- 10,671
- 2,028
Leo nimetoka kumzika rafiki yangu kipenzi, alifariki juzi kwa ajali ya pikipiki ametoka kuinunua juzi tu hapo ni kama usafiri wa kuanzia katika safari yake ya maisha maana ndivyo alivyosema kipindi anaplan za kuinunua, huyu ni mtu wangu wa karibu wa 9 namzika mean marafiki wa karibu, bado ndugu 4 niliowazika ndani ya miaka 3 tu kwa ajali za pikipiki.
Kifo kipo popote ila pikipiki zinamaliza watu sana, yaani ni heri ukajenge au ujichange ukanunue gari lakini sio pikipiki, kwa nchi yetu hii unaweza ukawa ni dereva mzuri wa pikipiki ila ukashangaa unakuja kuuliwa na madereva wa magari makubwa hata madogo wasiofuata sheria.
Ni ushauri wangu tu.