Kijana unaefikiria kuoa ukiwa na miaka 18-26

floow

JF-Expert Member
Mar 20, 2017
411
852
Vijana wengi wamekua wakifikiria kuoa pindi tuu wanapoanza maisha ya kujitegemea, kijana anapokua anamiliki geto, ana kitanda ka sofa ka TV ka jiko ka gesi na tuvindoo twa kuhifazia maji hapo anajiona sasa anauwezo wa kuoa.

Kabla kijana hujaoa jitafakari kwanza unaplan maisha yako yaweje, uwe mwenye pesa nyingi au uwe masikini mzuri, kama unahitaji kuishi maisha ya kifahari basi tambua mwanamke anaweza kua kikwazo cha wewe kuendelea.

Pindi utakapo oa/ kuishi na mwanamke tambua utakua na familia tatu(3) familia ya kwenu ,familia ya kwako na familia ya mke wako. Je upo tayari kubeba mzigo mkubwa pindi ukiwa na umri wa utafutaji. Utashindwa kufanikisha malengo kwasababu utakua na mzigo mkubwa.

Mwanamke anaamini njia bora ya yeye kutoka kimaisha ni kuolewa, hapo ana rahisisha maisha yake yeye jamani mwanamke ni mzigo sana tena ni mzigo mzito, usikubali kuoa ukiwa na umri chini ya miaka 26 wanawake wengi humfanya mwanaune kitega uchumi chake.

Tafakari kidogo kipato chako ni sh ngapi kwa mwezi, utatakiwa uache nyumbani sh.ngapi kwa siku(kodi ya meza). Ikitokea dharura utatakiwa utumie sh ngapi hapo utagundua pesa yako itaishia kwenye matumizi ya kawaida, pesa ya malengo itakua ni kidogo kuliko ya matumizi.

Utakapofikia kuoa basi fanya chaguo sahihi usichukue mwanamke eti sababu ana makalio makubwa hayo makalio yake hayata kuongezea uchumi wako, angalia mwanamke mwenye future, mwanamke anaefikiria utafutaji sio madada zetu wanaofikiria kukufinyia kwa ndani.

NB; watu waliofanikiwa ki maisha baada ya kuoa ni wachache wakati mzuri wa kujipanga kimaisha ni kabla ya kuoa.
 
Mwanamke sio mzigo kijana ngoja nikuambie hivi mfano umeoa ukiwa na miaka 35, jumlisha mwaka mmoja wa mkeo kutafuta mimba inakuwa 36 ,akipata mimba jumlisha miezi 9 ya mimba sawa na mwaka atakuwa na 37, mtoto anazaliwa kwa desturi za elmu ya tanzania miaka saba darasa la kwanza 7 atakuwa na miaka 37 +7 ni sawa na 44 ,anahitimu darasa la saba akiwa na miaka 14 ,44+7 ni sawa na 51, form one hadi four 4 ,51+4 nisawa na 55,six hadi chuo 6 maxmam 55+6 ni sawa na 61 bado kufeli ,kudisco n.k pili life expectance Tanzania 52 je kwa hali hiyo mwanao utaona matunda yake, vijana oeni mapema .
 
Usikariri. Mimi nimezaliwa baba yangu akiwa zaidi ya miaka 40 nimesoma mpaka najitegemea na bado yuko hai
 
43 Reactions
Reply
Back
Top Bottom