Kijana tapeli akamatwa na milioni 15 za mfuko wa Rais

mtu watu

JF-Expert Member
Dec 10, 2017
2,123
1,615
Kijana mmoja ambaye amefahamika kwa jina la Mohamedy Msangi (28) mkazi wa Kilakala Manispaa ya Morogoro anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kughushi nyaraka na kujipatia mkopo wa milioni 15 katika taasisi ya mfuko wa Rais Kanda ya Morogoro.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa jambo hilo na kusema kuwa jeshi la polisi lilipata taarifa na askari walifuatilia na kumkamata mtuhumiwa huyo ambapo baada ya kuhojiwa alikiri kufanya kosa hilo kwa kuomba mkopo katika taasisi hiyo inayojihusisha na utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake na vijana.

Matei amedai kuwa kijana huyo alipoomba mkopo huo aliorodhesha majina ya vijana wengine wanne akijifanya kuwa vijana hao wamejiunga kwenye kikundi hicho kisha kupatiwa mkopo huku hao vijana aliowaorodhesha wakiwa hana taarifa yoyote.

Mbali na hilo Kamanda Matei alitoa rai kwa wananchi wa Morogoro na kuwataka wananchi kuacha wizi "Tuache huu wizi kwa kutumia vyombo vinavyotoa mikopo kwani mikopo hii imewekwa kwa ajili ya kuwasaidia watu wa chini na hilo ndiyo lengo la Serikali kuwaondolea watu umasikini ili waweze kufungua viwanda vidogo vidogo na kujipatia kipato, lakini wapo watu wanatumia vibaya vikundi hivi" alisema Matei.
 
yaani wabongo ni waoga wa kuanza maisha mapya, asa umesha wakwapua 15m. unabaki moro kufanya nini

nenda zako mbeya, sumbawanga, katavi fanya biashara ya mazao, samaki, mitumba.

acha kuwasiliana na ulio waorodhesha kwenye mkopo ukifanikiwa kila la kheli ikibuma bora ulijaribu
Ndyo hvyo sema mipango yake ndyo imefail!
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom