Kijana Sospeter Shindika unatumiwa kisiasa, utakufa!

Sasa si kwanza asubiri amalize kuzunguka nchi nzima ndio atoe conclusion?! Ameanza kusema mambo yamebadilika huku hajamaliza mizunguko? Ni sawa na mtafiti anayesema nchi hii ina waisilamu wakorofi wakati amefanyia utafiti Zanzibar pekee!
 
Nani amemtuma mpk anapata media coverage?nani anamlipia mafuta yake?amewekewa bima ya afya na maisha au wanamtumia?kwa kigezo kipi anapokelewa ikulu?
 
....Kuna kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Sospeter Shindika anayesema atazunguka nchi nzima hususani Tanganyika kujionea maendeleo yaliyofikiwa ndani ya miaka 50 kwa kutumia pikipiki tena ya kichina..amedai mambo ni mazuri tofauti na watu wanavyosema,amesema safari yake itaitimishwa tarehe 9 desemba wakati wa kilele cha sherehe hizo na atapokewa na viongozi wa juu wa nchi.

My take;
Jamaa atakufa kwa kutaka sifa za kijinga...

Source:TBC-CCM C news bulletin

Pamoja na kwamba simjui lakini ni wazi hii ni propaganda ya hao viongozi atakaokutana nao December 9 wakati wa kilele na si kwamba anaubavu wa kutenda hayo, Pikipiki ya kichina hapo pana fisadi mmoja kajificha kutangaza Biashara ya hiyo Model wakati kiukweli kwa siku zilizobaki hawezi zungukia hata mikoa kumi kwa kunyoosha tu barabarani, sidhani kama inawezekana hata kama atapatiwa lifti za usiku, kuhusu wasiwasi wako wa kuwa jamaa atakufa kwa kutaka sifa hilo napingana nawe kwani watu wa hivyo walikuwa akina Seth Benjamin na TANU ya wakati huo ambayo leo ni CCM na haina watu wa hivyo, ila kwa hivi sasa mie wasiwasi wangu ni kwamba hao jamaa waliompangia hiyo fix wanaweza kujipromote kwa kumkorimba jamaa ili nao angalau wampate shujaa aliyekufa akiwa anazunguka Tanzania nzima kujionea maendeleo ambayo tunalazimishwa kuwa yapo na tukisema hayapo tunaambiwa hatuna macho....

CCM ENDELEENI HIVYO HIVYO KWANI MKIRUDIA MANENO YENU MARA 1000 WATU WATAFUNGUA MACHO YAO
 
Hiyo source ya habari yako vp? Nachojua mimi CDM ndio CCM-C. Itakuwa vizuri kama ukiiedit ili ireflect hali halisi

crap.gif

Ndio mkuu Rejao..kanawe!!
 
....Kuna kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Sospeter Shindika anayesema atazunguka nchi nzima hususani Tanganyika kujionea maendeleo yaliyofikiwa ndani ya miaka 50 kwa kutumia pikipiki tena ya kichina..amedai mambo ni mazuri tofauti na watu wanavyosema,amesema safari yake itaitimishwa tarehe 9 desemba wakati wa kilele cha sherehe hizo na atapokewa na viongozi wa juu wa nchi.

My take;
Jamaa atakufa kwa kutaka sifa za kijinga...

Source:TBC-CCM C news bulletin

Ndo wanachotumia kufikiria hicho.
 
Back
Top Bottom