Kijana Sospeter Shindika unatumiwa kisiasa, utakufa!

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
....Kuna kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Sospeter Shindika anayesema atazunguka nchi nzima hususani Tanganyika kujionea maendeleo yaliyofikiwa ndani ya miaka 50 kwa kutumia pikipiki tena ya kichina..amedai mambo ni mazuri tofauti na watu wanavyosema,amesema safari yake itaitimishwa tarehe 9 desemba wakati wa kilele cha sherehe hizo na atapokewa na viongozi wa juu wa nchi.

My take;
Jamaa atakufa kwa kutaka sifa za kijinga...

Source:TBC-CCM C news bulletin
 
Bado siku 6 kufika Tarehe 9 Desemba, ameishapita mikoa mingapi hadi sasa?
 
Anasifia majengo ya shule zilizojengwa kando ya barabara bila kuchungulia ndani ili aone kama kuna madawati au la!
 
....Kuna kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Sospeter Shindika anayesema atazunguka nchi nzima hususani Tanganyika kujionea maendeleo yaliyofikiwa ndani ya miaka 50 kwa kutumia pikipiki tena ya kichina..amedai mambo ni mazuri tofauti na watu wanavyosema,amesema safari yake itaitimishwa tarehe 9 desemba wakati wa kilele cha sherehe hizo na atapokewa na viongozi wa juu wa nchi.

My take;
Jamaa atakufa kwa kutaka sifa za kijinga...

Source:TBC-CCM C news bulletin

mgönjwa wa akili huyo pikipiki ya mchina ukiendesha Dar hadi Mpanda atakua tayari Kafa ! PUNGUANI
 
Mwacheni nae ajitangaze afahamike. Ila anaongea mambo ya kusadikika.
 
cha ajabu viongozi wa serikali wataweka kando tafiti kama za Haki Elimu juu ya uhalisia wa elimu instead watabeba na kuhubiri atakachoona Shindika
 
....Kuna kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Sospeter Shindika anayesema atazunguka nchi nzima hususani Tanganyika kujionea maendeleo yaliyofikiwa ndani ya miaka 50 kwa kutumia pikipiki tena ya kichina..amedai mambo ni mazuri tofauti na watu wanavyosema,amesema safari yake itaitimishwa tarehe 9 desemba wakati wa kilele cha sherehe hizo na atapokewa na viongozi wa juu wa nchi.

My take;
Jamaa atakufa kwa kutaka sifa za kijinga...

Source:TBC-CCM C news bulletin
Hiyo source ya habari yako vp? Nachojua mimi CDM ndio CCM-C. Itakuwa vizuri kama ukiiedit ili ireflect hali halisi
 
Mwacheni nae ajitangaze afahamike. Ila anaongea mambo ya kusadikika.

Hata wewe unaona kua kusema Chama "Twawala" kimeleta maendeleo toka uhuru ni hadithi za kusadikika??
Kweli dunia imebadilika siku hizi!!
 
...nadhani Rejao anaweza kuwa kichaa kuliko hata huyo Shindika tumjadiliye!! Rejao angekuwa yuko timamu,asingeshindwa kujua ukweli uliowazi kuwa TBC ni CCM-C, ikiifuatia CUF ambayo ni CCM-B.
 
...nadhani Rejao anaweza kuwa kichaa kuliko hata huyo Shindika tumjadiliye!! Rejao angekuwa yuko timamu,asingeshindwa kujua ukweli uliowazi kuwa TBC ni CCM-C, ikifuatia CUF ambayo ni CCM-B.

Na CDM ni CCM ngapi? Turudi kwenye mada..:focus:
 
Safiii sana lengo zuri sana kijana.

Lkn ninacho msikitia kashindwa kutambua kuwa alikopatia wazo hili ndiyo pa kuanzia kama pangekuwa pazuri(shule) asingekuwa na mawazo finyu kiasi hk.

Wanajamvi naomba msimlaum kijana tatizo kubwa ni ile st kayumba aliyo soma nazan pale kwenye lile tangazo la haki elim mwalim anapowafundisha kuhus ma2miz ya computer ticha -'hiii ndiyo sipiyuu....,
na hii ni screen...,unashut down.

Nazan kijana wakati mwalim anamfundisha somo hili alizungumzia swala la 'dunia kuwa kama kijiji' sasa nazan mwalim alikatisha pindi kabla hajamalizia kumweleza vizuri hivyo kijana akatoka nayo hiyo sentens na kuifanyia kaz sasa.

Kwanza darasan kwenyewe alikuwa anasinzia kwa njaa na uchovu.

Kumlaum huyu kijana ni sawasawa na kubishana na kumcheka mtoto mdogo anayejifunza kuongea pale anapokosea.
 
HATA HUO NI UJASIRIAMALI............ anafanya ajira jamani

si ndio ajira milioni hizo tulizoajiriwa?? sio kila kazi lazima itangazwe na iwe na job description
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom