SoC01 Kijana na dunia ya uchumi wa kidigitali, teknolojia na utandawazi

Stories of Change - 2021 Competition

rbens K

New Member
Sep 20, 2021
2
3
1. UTANGULIZI;
Habarini zenu wadau wote wa jamii forums, vijana wenzangu, waandaaji​
na wafuatiliaji wa jukwaa hili la “story of change”, Makala hii fupi ni kwa lengo la kuelimishana na kufundishana hasa vijana wenzangu Walioko katika jukwaa hili la jamii forums (story of change), kuhusiana na nafasi aliyopo kijana wa Kitanzania, Teknolojia ya Dunia, pamoja Utandawazi na mambo yaliyobebwa katika utandawazi huo.
Karibuni tujifunze na kuelimishana maswala mbali mbali hasa ya kiteknolojia pamoja na uchumi wa kidigitali, utandawazi pamoja na mikumbo ya utandawazi huo.​

Maana ya Uchumi,
Uchumi huweza kuelezewa kama jumla ya shughuli zote za binadamu zinazolenga kutosheleza mahitaji yao, huhusisha uzalishaji, usambazi, na utumiaji wa bidhaa, ikiwa ni pamoja na kutolewa kwa ajili ya huduma mbali mbali, uchumi mara nyingi hutazamwa kwenye ngazi za kijiji, jumuiya, mkoa, taifa au Dunia kwa ujumla.
Uchumi ndio hutafsiri uwezo wa kumudu mahitaji.

Teknolojia pamoja na utandawazi
Teknolojia, ni kukua kwa sayansi ya uzalishaji katika Nyanja mbali mbali ka ma vile, kiuchumi, kisiasa, na kijamii,
na utandawazi ni uongezekaji na muunganiko wa kiutendaji katika Nyanja mbali mbali kama vile kisiasa, kijamii, na kiuchumi, mara nyingi teknolojia ndiyo huzaa na kuieneza utandawazi.

2. MATABAKA YA KIUCHUMI DUNIANI
Ni ukweli uliodhahiri kuwa utofauti wa kiuchumi katika nchi zetu, ndio unaopelekea hata uchumi wa watu wake wanaoishi humo, Kutokana na utofauti wa uchumi na mafanikio ya nchi zilizopo duniani, Dunia imejikuta katika matabaka ambayo yamekuwa ni vigumu kuepukika, ambayo ni kama;

Nchi za daraja la kwanza (First world countries)
Hizi nchi ni za dunia daraja la kwanza, ni nchi zilizokwisha kuendelea ambazo wao ndio wazalishaji wakubwa wa bidhaa na waanzilishi wakubwa wa mambo mbali mbali, ni mataifa yanayomiliki viwanda vikubwa na yanaendesha | yanafadhiri mashirika yenye nguvu Duniani, mataifa haya hujiendesha kwa misimamo na mawazo yao wenyewe na teknolojia zao wanazitengeneza na kuanzisha wao wenyewe, huwa sio wategemezi katika kufanya mambo wala wategemezi kimawazo kutokea nchi ambazo zipo chini kiuchumi, mataifa haya pia ndiyo hulenga kuendelea kuyafanya mataifa yanayoendelea kuwa tegemezi wa kimawazo, misimamo na kiteknolojia kwao. miongoni mwa nchi hizi ni kama Marekani(U.S.A), China, Urusi, Uingereza, Hispania, Ujerumani n.k

Nchi daraja la pili (Second world countries)
Hizi ni nchi ambazo bado znaendelea, hazijafikia maendeleo ya nchi za daraja la kwanza, lakini pia hazilingani na nchi za daraja la mwisho, hizi ni nchi ambazo zenyewe zna uwezo wa kujiongoza zenyewe, kwa sera na mawazo ya watu wake, ni nchi ambazo huwa na viwanda vikubwa vya wastani vyenye uwezo wa kawaida tofauti na vile vya nchi za daraja la kwanza, japo huwa ni tegemezi katika maswala ya kiteknolojia mpya na mawazo kutoka nchi zilizokwisha kuendelea, lakini hizi ni nchi zenye watu(vijana) wanaojaribu kutengeneza mawazo yao ili nchi hizi ziweze kujiendesha bila kuwa tegemezi kutoka mataifa ya daraja la kwanza. Mfano Tanzania, uturuki, Poland, India, nk

Nchi daraja la tatu (Third world countries)
Hizi ni nchi za daraja la mwisho, hizi ni nchi ambazo znaendelea na bado ziko chini katika kila Nyanja, nchi hizi ni tegemezi katika kila kitu, ni nchi zenye viwanda vidogo visivyokidhi mahitaji ya watu wake, na hivyo nchi hii hutegemea bidhaa zakuingizwa kutoka nje katika nchi za daraja la kwanza na la pili, hizi ni nchi ambazo hufuata mawazo na misimamo ya mataifa ya daraja la kwanza na la pili, nchi hizi nyingi hutokea baani Afrika na chache Asia, mara nyingi nchi hizi znakumbwa na madeni kutoka mataifa makubwa, pamoja na taasisi znazofadhiliwa na mataifa makubwa miongoni mwa nchi hizi ni Burundi, Malawi, Uganda n.k

3. MAENDELEO YA TEKNOLOJIA DUNIANI
Hivi sasa ni tupo katika kipindi ambacho dunia inapitia teknolojia kubwa na za kisasa, matumizi ya smu janja(smartphones), matumizi ya roboti viwandani(robotics), kuenea kwa mitandao ya kijamii, internet za kasi kama 3G na 4G, zmerahisha sana dunia katika kusafirisha habari, ikiwa ni pamoja na utendaji kazi katika Nyanja mbali mbali, lakini pia kushirikishana katika fursa mbali mbali ambazo zmeibuka kutokana na teknolojia kukua.
Maendelao ya Teknolojia yameibua mawazo na fursa, pamoja na michezo mbali mbali ambazo, pamoja na changamoto za kibiashara kama zilivobioashara zingine, hizi pia zmeweza kuajiri vijana wengi ulimwenguni, teknolojia hizo ni pamoja na…

Teknolojia ya mifumo ya kubadisha pesa za kimtandao (Block Chain Technology)
Hii ni mifumo ambayo huwawezesha watumiaji wake kuweza kutuma au kutoa hela, na pia kununua na kuuza sarafu(coin) za kimtandao mfano wa coin hizo ni bitcoin na etherium.

Kununua, na kuuza Sarafu za kimtandao (Crypto Currency Trading)
Hii huhusisha ununuji wa sarafu inapokuwa imeshuka kwenye mzunguko, na kisha kuiuza wakati itakapopanda

Biashara za mtandaoni (Online Networking and marketing bussiness)
Hizi ni mifumo ambazo huanzishwa na makampuni na hutumia watu kuwekeza hela zao, ambapo baadae hurudishiwa hela zao walizowekeza pamoja na faida ya uwekezaji, makampuni haya hujihusisha pia utengenezaji wa mtandao wa watu ambapo watu hulipwa kama wakiwaalika na kuwasajili wenzao.

Kubeti (gambling | Sports betting)
Hii ni michezo inayohusisha kubashiri matokeo ya michezo mbali mbali kama mpira wa miguu, mpira wa kikapu, nk, ambapo watu hupata pesa kama matokeo ya michezo yakiwa sawa sawa na bashiri zao.

Televisheni za mtandaoni (online TV)
Hizi ni televisheni(TV) ambazo znaanzishwa mtandaoni, kwa malengo mbali mbali kama kuburudisha, kufundisha, au kuhabarisha, watu huweza kupata pesa kwa mikataba ya kurusha matangazo kupitia televisheni hizo, na pia hulipwa na mitandao kama youtube kwa kuwa na watazamaji na wafuatiliaji wengi.

Ufundishaji kwa njia ya mtandao (online learning)
Hizi pia ni njia za kujiajiri ambapo watu hutengeneza platforms za kujifunzia mtandaoni, na hivyo hulipwa kwa kufundisha watu wahitaji wa elimu au maarifa anayoitoa.

Urushaji wa matangazo ya kibiashara mtandaoni (online branding)
Hii nayo ni njia ambayo vijana wanaweza kujiajiri kwa kufungua blogs au websites, na wakawa wanalipwa kila wanapotuma matangazo ya mashirika mbali mbali ambayo wameingia nayo mikataba ya kuitangaza.

NB: Hizo ni fursa mbali mbali ambazo sasa teknolojia imerahisisha Zaidi, Katika kuchagua fursa na biashara hizi ni vyema mhusika aamue kufuatilia changamoto za kila moja pamoja na risk za kila biashara, mahitaji na vitu vingine vinavyohusiana na hiyo biashara.

4. MAPOKEO YA TEKNOLOJIA HIYO DUNIANI
Mapokeo Duniani
Hivi sasa mapokeo ya teknolojia ulimwenguni ni makubwa sana, biashara nyingi na kubwa znafanyika mtandaoni, utajiri mkubwa wa dunia sasa unahamia mtandaoni, na hiyo ni misimamo na mawazo ya mataifa yaliyoendelea kuhakikisha kuwa biashara kubwa na sehemu kubwa ya utajiri wa Dunia, pamoja na maisha ya wanandamu kwa ujamla yanahamia mitandaoni.

Mapokeo Tanzania
Mapokeo ya teknolojia hizi kwa upande wa Tanzania na Afrika haswa tukizingatia vijana ambao wao ndio taifa la leo na kesho bado Mapokeo ni madogo, ukilinganisha na kasi ya teknolojia hizo znavokwenda,
Ni vyema vijana wa kitanzania na Afrika kwa ujumla kujiandaa kuzipokea teknolojia hizo na kujifunza biashara hizo, kila mtu kwa nafasi yake na elimu yake.

Kama ni wataalamu wa Teknolojia(ICT);
  • Wajifunze namna wanavyoweza nao pia kutengeneza mifumo itakayotambulika serikalini, na itakayoweza kufanya kazi pamoja na mifumo hiyo mingine kutoka kwenye mataifa ya daraja la kwanza la uchumi ambao wao ndio waanzilishi wa teknolojia hizi.
  • Wasaidie katika kutoa elimu kuhusiana na elimu hizi za biashara na uwekezaji wa mtandaoni kwa vijana wenzao, na hata viongozi wa kisiasa ili kuendelea kudumisha uzalendo na kurahisisha Zoezi la ukusanyaji wa kodi katika biashara hizo za kimtandao
  • Watoe mawazo na misimamo ya namna gani ambavyo teknolojia hizo hazitoathiri upatikanaji wa huduma zingine za kifedha kama za Kibenki.
  • Washauri namna ambavyo biashara hizo zitaweza kurahisisha katika kutuma au kutoa pesa, kununua bidhaa na kufanya malipo mbali mbali katika taasisi za kiserikali na binafsi
Lakini pia kwa wengine wasiokuwa na elimu katika maswala ya kiteknolojia(ICT) ni vyema pia wakajifunza juu ya biashara hizi, ni vyema kila mtu kwa elimu yake hata kama ni elimu kidogo, bassi kujituma, kusoma na kujifunza kwa bidi sana ili kuweza kwendana na kasi ya teknolojia ya Dunia, ikiwa ni pamoja na;

  • kujifunza namna ya kuiendesha na kuwekeza katika mifumo hiyo, katika mlengo umbao hauathiri shughuli zingne katika jamii inayowazunguka.
  • kufikilia na kutoa mawazo na misimamo ya uendeshaji wa mifumo hiyo katika mlengo utakaofuata sheria na misimamo ya nchi,
  • Lakini pia kushauri kuhusu uelekeo na dira ya nchi katika mswala mbali mbali ya kidemokrasia, na maendeleo na ustawi wa jamii, pamoja na haki za binadamu, ikiwemo na zile haki za kimitandao ili kuweza kwendana na kasi ya teknolojia ya dunia.
  • Kuwasaidia na kuwapa elimu vijana wenzao ambao bado hawana elimu juu ya maswala ya teknolojia,
  • Kushirikishana na kuhamasishana katika fursa zingne zote za kawaida zinazotokea mtaani.

5. KIJANA NA UTANDAWAZI
Utandawazi ni juhudi za kibinadamu katika kuhakikisha kuwa Dunia inakuwa kama kijiji kwa kutumia teknolojia, katika utandawazi ndipo tunapata hoja za kurahisisha mawasaliano baina ya watu, kusambaa kwa habari, na kasi ya mtandao, ushawishi wa kimitandao na kuingiliana kwa mitindo ya kimaisha kwa watu wa Duniani.

Ni vyema Tanzania kama taifa huru, na lenye vijana wenye nguvu, kuishi katika misingi ambayo itadumu kuenzi tamaduni zetu zilizo njema za mababu na mabibi zetu, kuliko kufuata mitindo ya maisha ya watu wa mataifa mengine.

Zifuatazo ni faida za utandawazi;

Utandawazi husaidia kwa kiasi kikubwa uchangiaji wa mawazo
.
Kama kijana wa kitanzania ni vyema kutumia vyema utandawazi katika kuchangia mawazo chanya, na kujenga hoja katika maswala mbalimbali ya kitaifa na kijamii na kiuchumi.

Utandawazi hudumisha demokrasia, utawala bora na uwajibikaji.
Utandawazi husaidia sana kudumisha demokrasia ikiwa ukitumika vyema na katika mlengo mzuri, kama kijana ni vyema ukatumia fursa hii katika kudumisha demokrasia lakini pia uwajibikaji katika majukumu mbalimbali Aidha ya kitaifa, kijamii, kifamilia, au kiuchumi.

Utandawazi husaidia kukuza uchumi na biashara.
Kutokana na kukua kwa sayansi na teknolojia ni vyema pia vijana wakitumia utandawazi kama sehemu ya ajira kwao kujiajiri katika fursa mbali mbali znazopatikana mitandaoni kama ilivoainishwa awali, katika kufanya hivi kutawasaidia vijana kujiepusha na vitendo vya kiharifu visivyofaa katika jamii.

Utandawazi huongeza Zaidi uwazi katika utendaji na uendeshaji wa maswala mbali mbali ya kiserikali na kijamii
Kutokana na hii sababu vijana wanaweza kujifunza namna ya utendaji na uendeshaji wa majukumu katika nafasi mbali mbali kwenye Nyanja za kijamii, kisiasa, na hata kifamilia.

Utandawazi husaidia kusambaza na habari
Kutokana na utandawazi swala la kuenea kwa habari limerahisishwa na kuwa jepesi zaidi, hivyo ni vyema vijana wakawa pia wafuatiliaji wa habari ili waweze kufahamu juu ya maswala mbali mbali yanayowahusu na yanayolihusu taifa na Dunia kwa ujumla, ambayo pia huweza kueleza fursa mbali mbali kama vile kiuchumi, kijamii, kisiasa na kifamilia.

Utandawazi husaidia katika kujifunza
Utandawazi kupitia mitandao husaidia watu kujifunza na kupata maarifa kuhusiana na maswala mbali mbali ya kijamii, kiuchumi, kisiasa, na hata kifamilia, hivyo ni vyema kwa vijana kutumia utandawazi ili kijipanua kimawazo na kifikra, ili waweze kuwa tayari kukabiliana na changamoto ambazo znaweza kuwakabali.

Mbali na faida zifuatazo ni hasara za utandawazi ambazo ni vyema kwa vijana kuziepuka;

Utandawazi huweza kuharibu utamaduni wa kitanzania na Africa kwa ujumla
Kutokana na muingiliano wa watu katika mitandao hii huweza kupelekea kwa baadhi ya jamii kuanza kuiga tamaduni za jamii nyingine, hivyo ni vyema kwa vijana kutumia utandawazi katika mlengo unaohamasisha na kudumisha mila, tamaduni na desturi za kitanzania na kiafrika kwa ujumla.

Huchochea vitendo vya uovu
Pia kukua kwa teknolojia huweza kuchochea utapeli na wizi wa kimtandao, hivyo ni vyema vijana wakatumia mitandao kuelimishana maswala mbalimbali na ambayo sio mambo hayachochei uovu.

Huchochea tabia mbaya
Kutokana na kurushwa kwa baadhi ya maudhui yasiyofaa mitandaoni, mfano picha za uchi, video za ngono, au utumiaji wa madawa ya kulevya, nk, hii huweza kuchochea kuibuka kwa tabia mbaya miongoni mwa vijana wa Tanzania na Afrika kwa ujmla

Hupotosha umma
Baadhi ya maudhui zinazochapishwa mitandaoni huwa sio za kweli, hivyo kama vijana ni vyema kuhakikisha habari kabla hajaisambaza, lakini pia ni vyema Zaidi ikiwa vijana watakuwa wanatembelea majukwaa ambayo hutoa taaarifa zilizothibitishwa mfano jamii forums.

///// AKHSANTENI /////​
 
Uzi murua sana. Nasikitika ulikosa wachangiaji.
 
Back
Top Bottom