Kijana mwenye tatizo la kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja utamsaidiaje aweze kuacha? Soma kisa hiki

kipusaah

JF-Expert Member
Oct 15, 2017
252
243
Jamani mimi sio mwandishi mzuri mtanisamehe ila ntajitahidi kuandika kwa namna nitakavyoweza

Jana nilikaa mahali fulani akaja kijana ambae ni 25yrs age sina hakika kamili na age yake ni kijana ambae niko nae mtaani i mean tunafahamiana japo sio mtu wangu wa karibu jina sitamtaja, alinikuta nakunywa juice nae akaja kwa sababu namfahamu tulisalimiana na akavuta kiti akakaa pembeni sikuwa na shaka nae huku natabasamu tukasalimiana na yeye akaagiza lakini niliona ni kama mtu aliekosa raha kabisa ana msongo wa mawazo akaniambia kuwa jana alikuja nyumbani akanikosa kwani ana shida na mimi niliogopa kidogo kwa sababu sina ukaribu nae nikajiuliza maswali kimoyomoyo “ anataka kunikopa hela ?“ ana shida gani ? Akaendelea kuniambia kuwa jioni atakuja nyumbani nikamuuliza hapa hatuwezi kuongea ? Akasema hapana nitakuja home nikasema poa akalipa akaondoka .

Saa 20:30 hrs nikasikia mtu anagonga hodi mimi naishi peke yangu nikauliza nani akataja jina nikasimama kufungua akaingia baada ya salamu kimya kilitawala cha sekunde kadhaa mm niko busy macho kwenye Tv, akaniambia samahani nataka unipeleke kanisani unakosali kwa sababu mim ni mtu ninayesali sio sanaa ila mtaani naonekana mwema akaendelea kusema “nimekufata kwa sababu nimekuamini kuna vitu nataka kuacha ila nashindwa na sipendi nafikiri nikianza kusali vitanitoka” wakati huo mimi sijaongea chochte namsikiliza akaendelea “ mimi najihusisha na mapenzi ya jinsia moja (homosexual) sijui kama nimepatia “nimejaribu kuacha nashindwa na hii hali siipendi “ niliogopa aisee ukimuangalia ni kijana ambae huwezi kumdhania kabisaaa na ameajiliwa serikalini.

Nilichobahatika kumuuliza ulianzaje kafnya hivyo vitu ? Jibu lake “ hizi hisia toka nikiwa mdogo nilizaliwa nazo nilianza kutamani watu wa jinsia yangu toka nikiwa mtoto na hii hali siipendi ila nashindwa kujizuia kila ninapojaribu kuacha nashindwa naona bora nianze kusali maana hii michezo nikija kugundulika nitafukuzwa kazi (analiwa na kula) “ nilimuonea huruma sana anaongea huku analia nilichokifanya nilimwambia Jumapili nipitie tuanze kwenda kanisani hata kumgusa niliogopa maana anasema kuna muda anajiona mkosaji mbele za Mungu, kuna muda anatamani bora afe maana hapendi hizo hisia.

Sikutaka kumuhoji sana nikamwambia tuatenda kanisani ila nimeweka hapa bandiko tumsaidie huyu mtu kiushauri maana mimi nimekosa cha kmwambia zaidi ya kwenda nae kanisani. Ajabu ana mademu na kuna mwanamke anafanya nae kazi kazaa nae ila hawaishi pamoja . Nimejiuliza iweje analiwa na anapata mtoto? Yaani hii Dunia ina mengi sana
 
kuna kisa kingine kilindikwa leo kuusu kijana aliemaliza form four na anajihusisha na mapenzi kinyuma na maumbile. nao wimbi linaongozeka.
 
Back
Top Bottom