Kijana mmoja akutwa amekufa katika nyumba inayojengwa, kigogo, dar

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,040

Mwili ukiwa eneo la tukio.
3.jpg

Ukiwa umefunikwa.
4.jpg
Mashuhuda wa tukio hilo.​

Kijana mmoja aliyefahamika wa kwa jina la Kobero, leo asubuhi amekutwa akiwa amekufa kwenye

chumba kimoja cha nyumba ambayo ilikuwa haijamalizika kujengwa maeneo ya Kigogo Luhanga

jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, marehemu alikutwa na chupa iliyokuwa na masalia ya

pombe haramu aina ya gongo. Mpaka mwandishi wetu anaondoka eneo la tukio askari polisi

walikuwa bado hawajafika kwa ajili ya kuuchukua mwili na kuanza upelelezi wa tukio hilo.​

chanzo. KIJANA MMOJA AKUTWA AMEKUFA KATIKA NYUMBA INAYOJENGWA, KIGOGO, DAR - MPEKUZI HURU
 
Dah, inasikitisha sana, ila nahis atakuwa amekunywa kiasi kingi cha chang'aa bila kula. Mungu amlaze panapostahili ndugu Kobero!
 
Tusihitimishe haraka, anaweza akawa ameuawa alafu akawekewa kichupa cha Chang'aa jirani ili ionekane imemuua pombe, kwasasa kifo chochote kinachotokea kuna haja ya uchunguzi wa kina kufanyika, hivi unahabari Mlipuko wa Arusha uliambatana na risasi zilizolenga TANK la mafuta la gari la Matangazo? unafahamu kwamba mafuta yangelipuka na kuua watu zaidi na gari kuteketea ingetangazwa kwamba mlipuko ulitokana na Hitilafu za kwenye gari? unajua kwamba ishu ingewageukia wenye gari la Matangazo kwa kufanya uzembe mpaka Tank kulipuka?
 
Your a True Great Thinker!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom