piper
JF-Expert Member
- Jan 17, 2012
- 3,253
- 612
Mimi inaniumiza japo sikumwambia maana kama mwanamke ana miaka 44 je wataweza kuzaa hata mtoto mmoja wa kuwaunganisha? Ila nilimwambia anipe wiki moja kuanzia jana nitampa ushauri anaoutaka barabara. Ninajua JF ni kisima cha mawazo, kuna weledi wa mambo hapa. Ninawaomba sana changia mada hii kwa ukweli na busara maana ni kitu cha ukweli si cha kufikirika ili nipate mawazo yako nipate kumshauri kijana ipasavyo. Asante sana na karibu kwa maoni na ushauri. Mimi Zogwale.
Maadamu wanaelewana hilo ndo jambo la msingi, ndugu yako tayari ana mtoto so siyo lazima wazae na huyo mwanamke, mtoto ni majaaliwa toka kwa Mwenyezi Mungu huenda akaoa hata mwanamke ambaye hajafika menopause na asipate mtoto vile vile (God forbid).