Kijana kizimbani kwa kutaka kumdhuru NAHODHA

JacksonMichael

JF-Expert Member
Mar 22, 2012
339
61
Peoples power yamtokea puani mwanachama:

KIJANA Aludo Sanga (28) mkazi wa kitongoji cha Nelo Kiloleni katika mji mdogo wa Tunduma wilayani Mbozi, amefikishwa katika mahakama ya wilaya kwa kosa la kutishia kumdhuru Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha.

Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya, Rahim Mushi, Mwendesha Mashtaka, John Mazwile alieleza kuwa, kijana huyo alitenda kosa hilo Februari 3 mwaka huu, majira
ya saa 3:50 asubuhi maeneo ya Mwangaza Hotel mjini Tunduma wakati Waziri Nahodha katika ziara ya kiserikali.

Mazwile alisema kabla hajatimiza azma yake ya kuudhuru msafara wa waziri huyo, mshtakiwa alizuiwa na Vijana wa ulinzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), maarufu kama Green Guard.

Alisema wakati hayo yakitokea mshitakiwa huyo pia alikuwa ameshikilia kipande cha mti na bendera ndogo ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Alisema kosa hilo ni kinyume cha sheria kifungu cha 89 (a) na (b), cha marekebisho ya sheria mwaka 2002 cha kanuni ya adhabu.

HabariLeo | Kizimbani kwa kutishia kumdhuru Waziri Nahodha
 
Very good utawala wa sheria uchukue mkondo wake aisee. Na Hilo litakuwa fundisho kwa waovu wengine wa namna hii
 
Naomba kijana apatiwe usaidizi wa kisheria, maana hapa kuna kila dalili za kijana huyu kuonewa na kukandamizwa kwa sababu tu alikuwa na bendera ya chama cha upinzani!!. Tangu lini waziri wa mambo ya ndani akapatiwa ulinzi na Green Guard? kama alikuwa ameenda kichama kwa nini shitaka litaje wadhifa wa uwaziri??
 
Huyo alitaka kudhuru, wengine wamemuua baba wa taifa wanapigiwa na ving'ora
 
Labda alitaka ngozi yake iliyorutubishwa kwa pesa za wavuja jasho si unajua mbeya ngozi ya binadam ni nyara adimu!
 
saaafi sana serikali ikabiliane na hawa wahuni wasifikiri serikali imekwenda likizo.

Ndugu yangu funguka, inaonekana umefungwa mwilini na akilini!! hawa unaowaita wahuni ndiyo wanakupigania wewe ambaye hujitambui!
 
Peoples power yamtokea puani mwanachama:

KIJANA Aludo Sanga (28) mkazi wa kitongoji cha Nelo Kiloleni katika mji mdogo wa Tunduma wilayani Mbozi, amefikishwa katika mahakama ya wilaya kwa kosa la kutishia kumdhuru Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha.

Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya, Rahim Mushi, Mwendesha Mashtaka, John Mazwile alieleza kuwa, kijana huyo alitenda kosa hilo Februari 3 mwaka huu, majira
ya saa 3:50 asubuhi maeneo ya Mwangaza Hotel mjini Tunduma wakati Waziri Nahodha katika ziara ya kiserikali.

Mazwile alisema kabla hajatimiza azma yake ya kuudhuru msafara wa waziri huyo, mshtakiwa alizuiwa na Vijana wa ulinzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), maarufu kama Green Guard.

Alisema wakati hayo yakitokea mshitakiwa huyo pia alikuwa ameshikilia kipande cha mti na bendera ndogo ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Alisema kosa hilo ni kinyume cha sheria kifungu cha 89 (a) na (b), cha marekebisho ya sheria mwaka 2002 cha kanuni ya adhabu.

HabariLeo | Kizimbani kwa kutishia kumdhuru Waziri Nahodha

Yaani waziri anapewa ulinzi na Green guard akiwa ziara ya kiserikali?siku hizi green guard wanaubia na serikali kulinda mawaziri?totally confused
 
Hata Makaburu Afrika ya kusini walitesa wapigania uhuru lakini hatimae ukombozi ulipatikana, na Chama Cha Magamba kitapita na udhalimu wake wote.
 
Back
Top Bottom