Kijana kati ya miaka 18-35 anaesapoti CCM akapimwe akili

Kwa mtizamo wangu katika kipindi hiki cha miaka 50 ya uhuru Kama yupo kijana mwenye umri huo tajwa hapo juu ambae bado anaishabikia CCM inabidi akimbizwe milembe kwani kwani akili yake itakuwa ina ufa na hvo anahitaji uchunguzi wa kina. Katika nyanja zote kiuchumi, kisiasa,kijamii n.k. bado tuna safari ndefu ya kutembea........ukweli CCM haijaitendea haki nchi yangu Tanzania hivyo sioni sababu ya kijana ambaye bado uwezo wake wa kufikiri bado uko juu ashabikie upumbavu.
Mtazamo wangu mtu yeyote anayeshabikia siasa kama mtazamaji nadhani kiwango chake kidogo sana kufikiria na anamda mwingi sana kupoteza. Kama siasa ni kazi yako ndo unapokula sawa sitakuona kichaa kama wewe washabikia iwe ccm cdm au cafu na unaakili timamu na unazani yeyote katika hivyo vyama anaweza kutuondolea matatizo yetu nazani hujawahi fikiria hata siku moja. Hebu fikiria tuu kama wewe umechaguliwa mbunge ingunga leo hii utafanya nini kwa wananchi wa ingunga mwaka huu ulio bakia na mwakani kionekane na pia utoe mchango ulete maendeleo kwa nchi uonekana. Kama kuna mtu anaweza kuielezea mambo ambayo akipewa madaraka leo zaidi ya kufuidi kamshahara kuna jambo atatuongezea watanzania natamani kumjua.

Hao vijana, wazee, akinamama wanaopewa khanga, wanaume wanaopewa kilo1 ya nyama mi nawaona ni legelege kama serikali na viongozi wa chama tawala, vitu hivyo vinakufanya unapoteaza kura yako na kupata shida, kuishi kwenye giza miaka mitano! AIBU HII
WATANZANIA AMKENI

Ukikuta kijana wa umri huo anapanua mdomo wake kushabikia CCM kuna matatu:

1. Baba yake alikuwa (ni) kiongozi chama hicho ama

2. Hana kazi maalum ya kufanya nje ya siasa (anatafuta ajira kwa mgongo wa chama) ama

3. Mjinga tu (hana elimu)

4. Yote hapo juu

atakuwa ana maslahi binafsi ndani ya chama.

Ukikuta kijana wa umri huo anapanua mdomo wake kushabikia CCM kuna matatu:

1. Baba yake alikuwa (ni) kiongozi chama hicho ama

2. Hana kazi maalum ya kufanya nje ya siasa (anatafuta ajira kwa mgongo wa chama) ama

3. Mjinga tu (hana elimu)

4. Yote hapo juu

5. Baba yake ni mfanyakazi wa serikali anayeiba fedha za umma

Kwa mtizamo wangu katika kipindi hiki cha miaka 50 ya uhuru Kama yupo kijana mwenye umri huo tajwa hapo juu ambae bado anaishabikia CCM inabidi akimbizwe milembe kwani kwani akili yake itakuwa ina ufa na hvo anahitaji uchunguzi wa kina. Katika nyanja zote kiuchumi, kisiasa,kijamii n.k. bado tuna safari ndefu ya kutembea........ukweli CCM haijaitendea haki nchi yangu Tanzania hivyo sioni sababu ya kijana ambaye bado uwezo wake wa kufikiri bado uko juu ashabikie upumbavu.

sasa nimeamin CDM ni marufuku kupewa nchi hii kama hzi dharau na kejeli ndio zinaongoza akili zenu,mimi nipo ktk hyo miaka na naipenda ccm na ntaendelea hvyo daima chamsingi tuheshimiane ktk maamuz ye2 na sio kudharauliana hapa au mnataka kutumwagia tena tindikali ??

Ukikuta kijana wa umri huo anapanua mdomo wake kushabikia CCM kuna matatu:

1. Baba yake alikuwa (ni) kiongozi chama hicho ama

2. Hana kazi maalum ya kufanya nje ya siasa (anatafuta ajira kwa mgongo wa chama) ama

3. Mjinga tu (hana elimu)

4. Yote hapo juu
5.Au ni puuzipuuzi hivyo ni wakupuuzia!!

Namnumkuu Mh Warioba alisema "Ukiona jamii yeyote wazee na vijana wapo kundi moja basi iyo jamii itakuwa na mapungufu makubwa ya kufikiri". Mimi binafsi nitaendelea kuamini hii kauli ya Warioba, au vp mwana FA?

Sija kuelewa? Kwa hiyo vijana wawe na chama chao na wazee chama chao, au? Kwa sababu hakuna chama kinacho weza endelea bila wote. Chama cha siasa ni uwakilishi wa wananchi sasa utakuaje na chama ambacho kina support ya kundi moja tu ya jamii?

Ukikuta kijana wa umri huo anapanua mdomo wake kushabikia CCM kuna matatu: 1. Baba yake alikuwa (ni) kiongozi chama hicho ama 2. Hana kazi maalum ya kufanya nje ya siasa (anatafuta ajira kwa mgongo wa chama) ama 3. Mjinga tu (hana elimu) 4. Yote hapo juu
Na la mwisho atakuwa anafikiri kwa kutumia masaburi!

Si vijana peke yao. Mwaka jana baada ya uchaguzi Moshi njiani kurudi Dar-es-Salaam tulisimama Korogwe kuongeza mafuta. Gari ya mbele ilikuwa ya Freeman Mbowe na mimi nilikuwa gari inayofuatia.

Ukaja umati pale kutupa sapoti na alikuwepo mzee mmoja mwenye umri nakisia kuwa miaka 75 kuendelea mbele akitembea kwa taabu. Akaelekea gari ya Freeman na mimi nikashuka kusikia anachotaka kumwambia mwenyekiti wa Chadema.

Mzee huyo alisema "ninyi ndio wakombozi wetu." That is all the message he wanted to share with Freeman. Nikamwangalia yule mzee sikummaliza. Nikasema huyu mzee amekuwepo enzi za TANU. Alikuwa kijana na amekomaa enzi za CCM. Leo anatambua kuwa CCM si mkombozi wake tena.

I carry that picture in my head all the time. Kwa hiyo si vijana peke yao. Kwa wote wale wanaoitakia mema Tanzania CCM si mkombozi wao.

Sasa kama mzee tena mkulima ameweza kupambanua na kujua kwamba sehemu sahihi sembuse kijana ambae bado ubongo wake una uwezo mkubwa wa kufikiri!!! ndio maana mimi naona kijana anaeshabikia upumbavu akili yake itakuwa na matatizo tena makubwa

CCM...
Ni chama gani cha kufanananisha na CCM?
Jibu ni hakuna..live long CCM

sasa nimeamin CDM ni marufuku kupewa nchi hii kama hzi dharau na kejeli ndio zinaongoza akili zenu,mimi nipo ktk hyo miaka na naipenda ccm na ntaendelea hvyo daima chamsingi tuheshimiane ktk maamuz ye2 na sio kudharauliana hapa au mnataka kutumwagia tena tindikali ??

Naomba utumie akili yako vizuri kusoma na kuelewa.....kwenye hii thread sijaongelea habari ya chadema hapo. nimeongelea ushabiki usio na msingi dhidi ya ccm. unaweza usione chama cha kujiunga nacho lakini still ccm haijatutendea haki hivyo haistahili ushabiki.

Nadhani kuna kitu tunakikosea hapa. CCM ilishapoteza mwelekeo na kupendwa na watanzania mara tu mwenyewe(Mchonga) alipoondoka. Baada ya jamaa kuondoka chama kikatekwa na mafisadi na kupigwa 'nyuma geuka' kuelekea kusikojulikana.

Tangia hapo watu wote ambao hawakubahatika kuwa kwenye njia ile ambayo ccm mpya ilipokuwa inapita waliachana nayo.

Na ndiyo maana huwezi kuamini kwa nini CCM iliyokuwa na wananchama karibia watanzania wote(zaidi ya 35m), lakini uchaguzi wa mwaka 2010 ilikuwa na wananchama 5m tu tena pengine ni uongo.

Kimsingi 95Perc ya watanzania si wananchama wa chama chochote cha siasa maana walishadharau . Kinachotokea sasa hivi ni upenzi wa chama fulani tu ambacho lazima kiwe na uwezo wa kuwavutia watu hawa.

CCM haina mvuto hata mdogo kwa sasa zaidi ya kuwavutia watu kwa kutumia pesa za umma maana pesa haishindwi.

CCM imebakiwa na kete moja tu ya wananchi wa vijijini bado hawajui kuwa wanaweza kula hela za ccm wakati wa uchaguzi na bado wakachagua wagombea wa vyama vingine pasipo ccm kujua. Wananchi wanamini wanaweza kufatiliwa baada ya uchaguzi kwa kutoichagua ccm na huku wamekula hela zao.

Kifo chao kinakuja maana vijana hawaogopi kula hele zao na bado wakawapiga chini na hii ndo hatari iliyo mbele ya ccm. Hakuna kitu kibaya kama kutumia hela yako kwenye uchaguzi halafu ukashindwa matokeo yake huwa ni mabaya siku zote.

ukweli ndio huo lakini njaa zinawasumbua watu wengi sana kwa hiyo tutafuteni adhabu ambayo itakuwa nifundisho ili vijana tuachane na ccm maana haina mpya bali ni uhuni na utaperi uliojaa ndani ya chama

Nadhani kuna kitu tunakikosea hapa. CCM ilishapoteza mwelekeo na kupendwa na watanzania mara tu mwenyewe(Mchonga) alipoondoka. Baada ya jamaa kuondoka chama kikatekwa na mafisadi na kupigwa 'nyuma geuka' kuelekea kusikojulikana.

Tangia hapo watu wote ambao hawakubahatika kuwa kwenye njia ile ambayo ccm mpya ilipokuwa inapita waliachana nayo.

Na ndiyo maana huwezi kuamini kwa nini CCM iliyokuwa na wananchama karibia watanzania wote(zaidi ya 35m), lakini uchaguzi wa mwaka 2010 ilikuwa na wananchama 5m tu tena pengine ni uongo.

Kimsingi 95Perc ya watanzania si wananchama wa chama chochote cha siasa maana walishadharau . Kinachotokea sasa hivi ni upenzi wa chama fulani tu ambacho lazima kiwe na uwezo wa kuwavutia watu hawa.

CCM haina mvuto hata mdogo kwa sasa zaidi ya kuwavutia watu kwa kutumia pesa za umma maana pesa haishindwi.

CCM imebakiwa na kete moja tu ya wananchi wa vijijini bado hawajui kuwa wanaweza kula hela za ccm wakati wa uchaguzi na bado wakachagua wagombea wa vyama vingine pasipo ccm kujua. Wananchi wanamini wanaweza kufatiliwa baada ya uchaguzi kwa kutoichagua ccm na huku wamekula hela zao.

Kifo chao kinakuja maana vijana hawaogopi kula hele zao na bado wakawapiga chini na hii ndo hatari iliyo mbele ya ccm. Hakuna kitu kibaya kama kutumia hela yako kwenye uchaguzi halafu ukashindwa matokeo yake huwa ni mabaya siku zote.
Sioni cha maana ulichoandika hapa!

Back
Top Bottom