Kijana kama unakesha usiku kucha kusoma ufaulu; kama ajira huna unatakiwa kukesha pia usiku kucha kuwaza ufanye nini upate pesa

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,908
51,904
Vijana wengi hukesha hata usiku kucha kusoma ili wafaulu mtongani

Akishamaliza vyuo na kupata vyeti hushinda tu akilalamika ajira hamna huku akikesha kuchat na simu kuhangaika kuangalia movie na ujinga mwingine wa mitandaoni.

Hakeshi kuwaza na ku-brain storm afanye nini ili apate pesa.

Vijana wa Kenya wako vizuri Mon kwenye hili asilimia kubwa kuanzia simu hadi mitandao kutumia kutafuta fursa tofauti na vijana wa Mtanzania wanaomaliza vyuo utanikuta anachat usiku na mchana kazi hana anachat ujinga mtupu mitandaoni ukiingia ni kuhangaika na ujinga tu.

TV zina vipindi vingi vya kuamsha akili lakini utakuta muda wote yuko kwenye kuangalia movie. Hana muda wa kuhangaika kuhangaika kuwaza fursa au nini afanye apate sijui anangoja nani amuwazie kwa niaba yake?

Dunia hii mtu kukaa anasubiri mtu mwingine akuwazie kuwa ufanye nini? Utasubiri sana mbona. Utachakalia nyumbani kwa wazazi shauri yako
 
Matatizo yanaanzia katika elimu yetu. Haijajengwa kumnufaisha kijana kimatendo hasa kama hatarndelea na masomo ya juu.

Jirani yetu alikua na mradi mkubwa sana wa kuku wa nyama na wa mayai. Alikua na mabanda 20 nyenye uwezo wa kufuga kuku 500 kila banda. Alitusimilia ujuzi ile aliupata Kibaha sekondari , yeye ni kati ya wanafunzi walioingia Kibaha ya wa Nordic.
 
Tunawasifu sana wake ya kwa mambo mengi lakini mbona wana umasikini kama sisi tu!
 
Nyinyi wazee mnashindwa kuachia ofisi mkajiajiri mnazeekea maofisini kila siku kutuambia vijana tujiajiri nyie mmeshindwa nini?

Wekeni mazingira wezeshi watu tutajiajiri sana tu.
Mfano mikopo haipatikani hadi uwe na asset ya kuweka utaanzaje kupata capital?
 
Mkuu jua huko kukesha kusoma hakukua ni Overnight Success kwamba tumekesha leo kesho tumetoboa pepa ni imechukua muda wa miaka 4 Secondary 2 Alevel na 3 mpaka 5 Chuoni just jumla tumetumia miaka kama 10 kimakadirio ya kukesha na imefanikisha sisi kutoboa kipepa.

10 Yeas Consistency imetufanya tutoboe mitihani mbalimbali.

Swali
Kwanini leo hii mtu kamaliza chuo leo unataka akeshe na afanikiwe leo hii ku-make PESA au kutoboa kimaisha bila kumpa timeline ya kueleweka.

Ku-Make PESA sikitu rahisi hata kidogo hapa Duniani hata uki Brainstorm vipi finally katika Reasoning zako uta outline changamoto ambazo zinabidi ziwe solved kwenda mbele...hizi changamoto zinamfanya mtu a-delay au awake timelines za kuzitatua sasa kipindi ambacho mtu yupo ndani ya timelines zake akija jamii isiyo jielewa inaanza kumpa pressure “Kasoma hana kazi, pesa nk”...Hawajui Timelines wakati kipindi anasoma walijua kuna timelines.
 
Kwani wataisoma namba siku zote, si mapito tu ujui ajae atafungua Milango ya ajira na uwekezaji.
 
Kama huna pesa hata ukeshe milele hakuna kitu utafanya, mimi ni muhanga wa yote haya. Nilikesha kusoma nakuja mtaani hakuna ajira nikakesha kuwaza at the end nahitaji pesa kulilisha wazo langu ili lishibe naishia ukingoni baada ya kukimbia sana sakafuni.
 
Matatizo yanaanzia katika elimu yetu. Haijajengwa kumnufaisha kijana kimatendo hasa kama hatarndelea na masomo ya juu.

Jirani yetu alikua na mradi mkubwa sana wa kuku wa nyama na wa mayai. Alikua na mabanda 20 nyenye uwezo wa kufuga kuku 500 kila banda. Alitusimilia ujuzi ile aliupata Kibaha sekondari , yeye ni kati ya wanafunzi walioingia Kibaha ya wa Nordic.
Badili hata Swahili utumie English yao jamaa zako ambao wamekuandaeni nyie. Pole kwa kuwa BRAINWASHED na Tiivii za Joe B.
 
Kama huna pesa hata ukeshe milele hakuna kitu utafanya, mimi ni muhanga wa yote haya. Nilikesha kusoma nakuja mtaani hakuna ajira nikakesha kuwaza at the end nahitaji pesa kulilisha wazo langu ili lishibe naishia ukingoni baada ya kukimbia sana sakafuni.
Rudi tena ka Brainstorm jinsi ya kupata mtaji
 
Kuna kitu kinakusumbua kinaitwa Cognitive desonance .kwamba kwa vile wale ni maskini na wewe lazima uwe maskini kwa kuwa tu tupo nao jirani..

MÊmENtO HoMO
Asante mkuu kwa kunifungua macho, sikuwa najua congitive dissonance, nimejifunza kitu. Lakini comparison katika maisha huwezi kuzikwepa.
 
Nyinyi wazee mnashindwa kuachia ofisi mkajiajiri mnazeekea maofisini kila siku kutuambia vijana tujiajiri nyie mmeshindwa nini?

Wekeni mazingira wezeshi watu tutajiajiri sana tu.
Mfano mikopo haipatikani hadi uwe na asset ya kuweka utaanzaje kupata capital?
Badala kulalamika tuu hebu msikilize huyu milionea mkenya aliyetoka familia maskini ya kutupwa alivyoanza umilionea wake kwa kuwaza solution enzi zake

Mkuu umeongea point. Lazima kijana uwe na future plan, siyo kusoma tu.
Wengi hawana future plan

Uliza hata mhitimu yeyote unayemjua kama kichwani kwake ana hata wazo la kujiajiri anawaza kuwa ajiajiri kwenye nini ? wengi weupe tu kichwani hamna kitu nimefanya utafiti binafsi wengi hawana wazo hata moja

Tuombe wazazi waulize watoto wao kuwa kama nikitafuta mtaji mwanangu waweza kupenda kujiajiri kwenye kipi? Nakuhakishia wazazi wengi wakiuliza watoto hili swali watashangaa mtoto hana alijualo ni mweupe kabisa kichwani

Nawasihi wazazi jaribuni kuuliza wanenu hilo swali hata sasa hivi tumeni meseji au wapigieni simu ghafla kuwauliza mtashangaa wenyewe kuwa mna mitoto isiyojielewa mkifa leo itaishia pabaya
 
Badala kulalamika tuu hebu msikilize huyu milionea mkenya aliyetoka familia maskini ya kutupwa alivyoanza umilionea wake kwa kuwaza solution enzi zake

Tolea mfano wa tajiri Mtanzania basi. Maana mifano yote naona ni kina Bill Gates, Tajiri Mkenya

Huko waliko siyo Tanzania, kuwa nchi hii tu tayari ni tatizo.

Hata kina Manji wangekuwa wanatunzia pesa zao bongo, sasa
hivi angekuwa masikini wa kutupa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom