Uchaguzi 2020 Kijana Ibzan Michael (24) atia nia Ubunge jimbo la Arusha Mjini kupitia CCM

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,744
21,194
Watia nia kwenye kinyang'anyiro cha ubunge Arusha mpaka sasa wanakadiliwa kufikia 40 kwa wale walichokua fomu na miongoni mwao ni kijana mdogo wa chuo kikuu cha Dodoma UDOM ambaye amejitokeza kuchukua fomu na kusubiri kwa hamu kurudisha fomu na kuomba kudra za kikao cha kuteua jina moja.

IMG_9375.JPG

PICHA: Ibzan Michael (kushoto) akipokea fomu za kuwania ubunge jimbo la arusha mjini kutoka kwa katibu wa ccm.

Ibzan mwenye umri wa miaka 24 ameoneka kuwa ndiye mtia nia ya ubunge mdogo yawezekana kuliko wote wanaochukua fomu kwa tiketi ya CCM, anasema ana sababu nyingi zilizompelekea kuchukua fomu, japo muda wa kampeni bado ila anasema miongoni mwa sababu kama kijana anaona vijana wenye rika kama yeye wengi bado hawajapewa nafasi na fulsa hivyo wana changamoto ikiwemo ajira.

Ameongeza kuwa amejipanga kimwili, kiakili, akiwa na akili timamu huku akitambua kila mtu amezaliwa akiwa na utofauti wa kitu chake cha msingi, hicho ndicho kinacholeta utofauti katika nyanja ya uongozi.

Hata hivyo Ibzan anajiandaa kukumbana na majina makubwa ambayo bado hayajachukua fomu ukiachilia mbali meya aliyepita Kalist Lazaro ambaye kachukua fomu leo, majina hayo yanatajwa lakini bado wanatizamiwa kuchukua fomu siku za mbele kabla ya tatehe ya mwisho July 17.2020.

Mtia nia Ibzan anatembea akiwa na nia inayopewa nguvu ya kauli mbiu yake isemayo I born to impact the societies.

NB. Vijana wanaonyesha ujasiri wangali na damu changa kwenye wigo wa siasa zenye ushindani.
 
Kumbe ndio maana leo nimeona tweet ya Lema, anasema angependa wote wanaochukua fomu kuomba kugombea hiyo nafasi ya ubunge Arusha Mjini kwa tiketi ya CCM wapitishwe wote kama ingekuwa inawezekana, halafu akawachape wote kwa pamoja kwenye sanduku la kura.
 
Huyo jamaa anaemkabidhi facial expression yake ni kama anajiuliza "huyu dogo chenga sanaa, hizi mbilinge mbilinge za huku ataziweza kweli"


Let's meet at the top, cheers 🥂
 
Kumbe ndio maana leo nimeona tweet ya Lema, anasema angependa wote wanaochukua fomu kuomba kugombea hiyo nafasi ya ubunge Arusha Mjini kwa tiketi ya CCM wapitishwe wote kama ingekuwa inawezekana, halafu akawachape wote kwa pamoja kwenye sanduku la kura.
Hahahaha!!!
 
Hizo form shilling ngapi kwa ngazi ya ubunge?

Kuna uwezekano siku ya leo pekee wagombea zaidi ya 5000 wamejitokeza nchi nzima.
 
Tujiandae saa tatu kamili kutazama mahojiano mahsusi Kati Dr. Hussein Mwinyi(Rais mtarajiwa wa Zanzibar) na Tido Muhando UTv(Channel 108 azam tv)
 
Sasa kila Mwananchi anataka kuwa Mbunge ili kuwatumikia Wananchi.

Inaonekana hakuna anayeitaka taabu ya kubaki kama Mwananchi na kutumikiwa....kuna kila dalili kuwa ki siasa kutumikia ni neema kuliko kutumikiwa.
 
Back
Top Bottom