Kijana Ibrahim Maximillian anamtafuta baba yake kwenye picha hizi hapa

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
2,858
7,846
Wadau, kuna kijana ambae nafahamiana nae, ameniomba nimsaidie kuleta uzi humu ndani wa kumtafuta baba yake, ambae anaonekana katika picha hizi ambazo zimeambatanishwa hapa chini.
Andiko lake hili hapa chini. Kama una chochote cha kumsaidia, mcheki kupitia mawasiliano yake aliyoweka hapo. Ahsanteni.

NAMTAFUTA BABA YANGU NA NDUGU ZANGU, DUNIA NISAIDIENI.
TAFADHALI JARIBU KUNISAIDIA KUSHARE POST HII POPOTE ILI NIMPATE BABA YANGU MZAZI.
Ninaitwa IBRAHIM MAXMILLAN, jina langu la tatu ni SPIRIAN (CYPRIAN), hili jina sina uhakika mzuri kuwa ndio jina la baba ila nilipoanza shule niliandikishwa, nina miaka 25 ( nilizaliwa 1994 mwezi wa tisa tarehe 8) Iramba, mkoani singida.
Jina la Mama yangu ni UPENDO DANIEL KISSUU (Mnyaturu)
Kwa bahati mbaya alishafariki tangu 2004.
Sikupata bahati ya kukaa na baba yangu ambaye niliambiwa na mama yangu kuwa aliitwa kwa jina moja la MAXMILLAN
ambaye walikutana MKOANI ARUSHA Miaka ya 90 na ndio mimi nilipopatikana.
Naambiwa baba yangu alikuwa mpishi kwenye moja ya Migahawa mjini Arusha. Lakini baadae alihamia Dar, ambapo pia alifanyakazi kigamboni, msasani kwenye hotel za humo. (hizi ni taarifa tu nilizochunguza sina uhakika sana.)
KWA MAELEZO YA MAMA, BABA YANGU ALIKUWA NI MTU KUTOKEA MKOANI KAGERA, KIUKWELI SIJUI KABILA LAKE VIZURI JAPO ILINILAZIMU KUTUMIA KABILA LA WAHAYA KAMA KABILA LANGU, JAPO NAAMINI KAGERA KUNA MAKABILA MENGI, SO HUWA SINA UHAKIKA HAPA.
Nimewahi kumuona baba mara chache sana MIAKA YA 2000 alipokuwa akija nyumbani kujaribu kumuona mama aliyekuwa anaumwa sana lakini mama alimfukuza bila kujali.
Baba alilazimika kuondoka, sijui ugomvi wao ulikuwa nini na sihitaji kujua. NINACHOTAKA NI KUKUONA BABA YANGU japo sijui kama bado uko hai baba au na wewe ulishaniacha, lakini walau mahali ulipozikwa nijue ni wapi baba.
Na hata ndugu zangu upande wako niwafahamu, niwajue. Ona sina historia kuhusu wewe, natamani kuita BABA hata kama nimekuwa bado unaumuhimu kwangu hakuna anayeweza kuwa kama wewe.
MARA YA MWISHO MIMI NA WEWE BABA TULIKUTANA OYSTERBAY POLISI KOTA ZA POLISI ZA ZAMANI KWA BABU (MJOMBA AKE MAMA ANGU - AFANDE DANIEL SENGE).
Kwenye hii post nimeambatanisha picha mbalimabali zinazoonesha baba angu na watu wake wa karibu.
Yupo bibi yangu alikuwa anaishi Arusha (picha 1992).
Yupo bibi yangu mdogo alikuwa chuo kikuu cha Dar es salaam (picha 1993)
Yupo shangazi yangu, jina lake ni Jeni (Jane) alikuwa pia Arusha.
Picha ambayo baba yangu ameshika mtoto (katikati) na wanawake wawili pembeni. Wa kulia ni shangazi yake baba na huyo aliyeshikiliwa ni mtoto wa huyo shangazi (ambaye walifariki wote yy na mtoto wake) na huyo wa kushoto picha haijamuelezea. (picha 1993).
Kuna picha baba yangu amevaa kofia ya kiislamu (barkashee naomba radhi Sijui kuiandika hiyo) yupo kama jikoni anakata nyanya, huyo wa pembeni ni rafiki ake kwa jina la PASKALI (PASCHAL) Picha tarehe 1/12/1994.
Hizi zote ni details ninazozichukua kutoka nyuma ya picha ambapo mama aliandika.
Picha nyingine hazikuandikwa lakini naamini kuna mmoja anaweza kuwa yupo hai akanisaidia kujua baba yuko wapi
Na MUNGU abariki nimpate baba yangu. KWA NAMNA YOYOTE UNAWEZA KUMTAMBUA MTU MMOJAWAPO KWENYE PICHA HIZI, PLEASE NISAIDIENI. NATANGULIZA SHUKRANI. MUNGU AWABARIKI.
Napatikana kwenye namba ya simu MUDA WOTE 0686002420,
0745 218987
0678 593050
Email: ibrahmaxmillan@gmail.com /ibrahimmaxmillan@yahoo.com
UNAWEZA KUNIPIGIA AU KUNITUMIA UJUMBE WA MAANDISHI Kwenye simu hizo.
NAPATIKANA TABATA KIMANGA, DAR ES SALAAM.
Naombeni mnisaidie ndugu zangu,nitafurahi kuwaona ndugu zangu.
Mimi Ibrahim Maxmillan
1566913676610.png



1566913707017.png




1566913723055.png



1566913748569.png


1566913763033.png







1566913802090.png


1566913828000.png



1566913847523.png


1566913861706.png
 
Mungu akusaidie uweze kumpata Baba yako mkuu


























Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Chakwale
Mungu Ibariki Gairo
 
Duh afazali. Rip huyo mzazi.

Ndugu sasa mumtafute huyo kijana ameshajitambulisha kwenu.
Nimeongea na kijana, anafurahi amepata baadhi ya ndugu zake, ila ameambiwa Mzee wake alifariki yangu 2009. R.I.P Kwa mzazi wake.
 
Nimeongea na kijana, anafurahi amepata baadhi ya ndugu zake, ila ameambiwa Mzee wake alifariki yangu 2009. R.I.P Kwa mzazi wake.
maskin! pole sana kwa kijana na hongera san kwa ushujaa alionyesha kwa izo details lazm angempata tu
 
Back
Top Bottom