Kijana Chacha Makenge aendelea kuishi kwenye handaki ndani ya pori la chuo kikuu

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,673
2,000

Kijana Chacha Makenge aliyerejea na kuendelea kuishi katika handaki ndani ya pori la chuo kikuu lililoko karibu na Mlimani City baada ya kuondolewa kwa nguvu anaomba msaada wa kisheria kutoka katika taasisi za kutetea haki za binadamu alodai utamsaidia kuondokana na maisha ya kuishi katika handaki kutokana na dhuluma aliyofanyiwa zaidi ya miaka minne iliyopita sasa.December 18,2013 kwa mara ya kwanza ITV inatangaza habari za kijana huyu ajulikanae kwa jina la Chacha Makenge na kisha baadae anatoweka katika eneo hilo kabla ya kurejea tena hivi karibuni na kueleza ITV alikamatwa na watu aliodai kuwa ni polisi kwa madai kuwa ni mgonjwa wa akili na kupelekwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili alikokuwa akitibiwa.

Kijana huyo mwenye umria wa miaka 38 sasa machoni anaonekana mwenye afya ya mwili na akili pamoja na siha njema huku akilalamikia kitendo cha ustawi wa jamii kumpeleka kwa nguvu katika wodi ya vichaa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jambo analodai limemwathiri kisaikolojia na kimaisha miongoni mwa jamii baada ya jamii kuaminishwa kuwa yeye ni mgonjwa wa akili jambo analolikanusha vikali na kwamba kila akijieleza anachukuliwa kama ni kichaa.

Hivi sasa Chacha Makenge anayeishi katika handaki lake baada ya kulikarabati kutokana na kuharibika kwa kipindia ambacho hakuwepo anasema hana uwezo wa kuendelea na shughuli zake kama kawaida kutokana na kuvunjika baadhi ya pingili za uti wa mgongo kutokana na kile anachodai kuwa ni kipigo kutoka kwa polisi miaka minne iliyopita wakati anachomewa nyumba yake na kuiomba jamii kumsaidia matibabu pamoja na fedha za kujikimu.

Kutokana na hali hiyo ITV kwanza inafika katika ofisi za kata ya ubungo na kuzungumza na afisa mtendaji wa kata hiyo Bwana Shaban Kambi ambaye anasema hana taarifa za Bwana Chacha kurejea na kuishi katika handaki na kwamba atawasiliana na ofisi ya ustawi wa jamii kinondoni kwa msaada zaidi.

Katika ofisi za ustawi wa jamii manispaa ya Kinondoni wanakiri kumtambua Bw Chacha baada ya kuona taarifa zake kupitia ITV na kuhusika katika zoezi la kumpeleka Muhimbili kabla ya kuachiwa baada ya kupata nafuu kutokana na kile walichokuwa wakimtibu.

Mh Dr Pindi Chana ni naibu waziri wa maendeleo ya jamii jinsia na watoto ambaye anaziagiza mamlaka husika kuchukua hatua kwa kufuata taratibu si kwa Bwana Chacha peke yake bali kwa wale wote wanaohitaji msaada kutokana na manyanyaso ya kijinsia ama kuathirika kisaikolojia.Mia

Chanzo: ITV
 

Mkempia

JF-Expert Member
Mar 5, 2013
1,142
1,500
hakuna kauli inanikera kama hii "NAZIAGIZA MAMLAKA HUSIKA" hii katika mamlaka na wewe Mh. Naibu waziri si unawajibika? kwa nini usioneshe mfano kwa kwenda wewe mwenyewe?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom