Kijana azawadiwa gari na wafanyakazi wenzake baada ya kugundua alikuwa akitembea km 17 kuja kazini

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Lewis-with-the-car-660x400.jpg


Habari kutoka nchini Kenya ambayo imeibua hisia za watu mbalimbali leo February 14, 2018 ni inayomhusu kijana mmoja ajulikanaye kama Trenton Lewis mwenye miaka 21 ambaye aliamua kwenda kazini kwa mguu umbali wa kilometa 17.7.


Ameeleza kuwa amekuwa akitembea mwendo huo ili aweze kufika kazini anapofanyia kazi saa 10 alfajiri kwani hakuwahi kuwa na gari wala nauli na amefanya hivyo kwa muda wa miezi saba bila kulalamika na wala hajawahi kuchelewa.


Kutokana na kufanya hivyo, baadhi ya wafanyakazi wenzie walipogundua huwa anatembea mwendo mrefu kiasi hicho kwenda kazini kila siku waliamua kufanya mchango na kufikisha Dola za Marekani 2000 sawa na Tshs Milioni 4.8 na kumnunulia gari.


Trenton alipewa gari hilo kama ‘surprise’ na kuelezea furaha yake na kwamba ni jambo ambalo hakufikiria lingeweza kutokea.


Chanzo: Millard Ayo
 
Wameamua kumwoza mke kwa lazima. Apende asipende "mtoto" wa watu lazima ale,aoge, avae nk. Hana majadiliano huyo, suluhisho labda aamue kumpiga talaka tatu.
 
Back
Top Bottom