Kijana apigwa kwa kukosa uzalendo

SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
4,040
8,895
Kijana mmoja maeneo ya Tabata Liwiti amepigwa na wananchi wazalendo baada ya kuongea maneno mabovu kuhusu viongozi wa nchi.

Moja ya maneno aliyoongea kuwa "hawa viongozi ni manunda hawajielewi licha ya wenzao kufa kwa Corona ila bado hawachukui tahadhari, watalitia hasara taifa watakapoanza kufa kama kuku wa kideli".

Maneno yake mabovu yalisababisha wananchi wazalendo wampe kipigo cha mbwa koko na kuacha kutazama kuapishwa kwa Mawaziri.
 
Hao waliompiga watajuta kwa kujichukulia sheria mkononi
Wanatetea uzalendo wa nchi ndio maana mh. Hayati alisema somo la historia ya Tanzania lifundishwe kuanzia darasa la kwanza hadi form six.
 
Kijana mmoja maeneo ya Tabata Liwiti amepigwa na wananchi wazalendo baada ya kuongea maneno mabovu kuhusu viongozi wa nchi.

Moja ya maneno aliyoongea kuwa "hawa viongozi ni manunda hawajielewi licha ya wenzao kufa kwa Corona ila bado hawachukui tahadhari, watalitia hasara taifa watakapoanza kufa kama kuku wa kideli".
Maneno yake mabovu yalisababisha wananchi wazalendo wampe kipigo cha mbwa koko na kuacha kutazama kuapishwa kwa mawaziri.
Hao wananchi nao ni manunda tu!

Huyo kijana ndio mzalendo wa kweli anayejali maisha ya viongozi wetu na wananchi kwa ujumla.

Ni jambo la hatari kuendelea na maisha kama kawaida bila kuchukua hatua za kujikinga na korona kwa kufuata miongozo ya wataalamu wa afya.

Korona ipo. Vaa barakoa. Epuka mikusanyiko. Nawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni.
 
Rekebisha heading yako.Andika kuwa mwananchi apigwa kwa kukejeli viongozi.Uzalendo siyo kuwapenda viongozi wala kumpenda mtu fulani wala kukipenda chama fulani.Uzalendo ni kuipenda nchi yako.Unaandika mambo ya ajabu ajabu kama haya ina maana wakati wenzako wanaenda shuleni kusoma civics wewe ulikuwa unakula makamasi?
 
Back
Top Bottom