Kijana apiga mbizi kutekeleza agizo la Magufuli!

We Jason bourn na kitengo cha usalama wa taifa kwangu ni sifuri, ndoa yenu na mafisadi, ushirika wenu na wawekezaji hata wasio na viwango, ninyi ndo waficha nyaraka za ushahidi wa ubadhilfu kisa zinawahusu washirika wenu wana siasa, ninyi ndo waratibu wa uchakachuaji wa kura, sasa naona mmeanza kufuatilia wapiga mbizi, kesho mtakuwa waganga wa kienyeji!
 
Update:
Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa kijana alitumwa na wapinga nauli mpya, kijana kabainisha wazi kuwa alipewa elfu hamsini, na watu ambao sasa tunawafatilia ili kujua zaidi kilicho nyuma ya pazia.

Suala hili linaonyesha limeingiliwa na vita ya kisiasa, hasa likilenga kukosoa kauli ya Magufuli!
Katika mahojiano niliyofanya nae kitaalamu zaidi kijana ni mvuvi wa pale feri na tenda hiyo alipewa tangu jana, anazidi kuweka wazi kuwa watu waliompa kazi hiyo walikuwa wawili wakitumia gari plado nyeusi na walivaa mmoja shati jeupe,na mwingine hakumbuki vema!

Kulingana na maelezo yake nimeamua kumtoa mahabusu kwa kutumia oda ya kiwanausalama na sasa nimempa laki moja kwa maelezo kuwa nampongeza kwa ujasiri wa kuvuka bahari,
lakini lengo langu anisaidie kujua nani zaidi walimtuma na lengo lao zaidi ya kupinga nauli kingine nini?? Nimemrudisha mpaka feri lakini ktk mazingira ambayo hajui kuwa mimi ni mmoja ya waliyomchukua pale kigambo feri!

Nahisi lipo kubwa zaidi ya nauli, nalo ni vita ya wanasiasa wabunge na waziri magufuli!

Subirini nitawajuza!

kumbe we ni polisi....

mi najua darasa la saba hawez kuwa na akili!! kuna polisi msomi!??!!!"'''' 99% ni vilaza, sina cha kuongea nao!!!!
 
Yesu alikanwa mpaka leo hii na Muyahudi sembuse mimi??
Mie sintokaa kukubali uongo wako kama Great Thinker. Kwa sababu haina mantiki na ulichokiandika. Hujaweka hata source, sijaona hata kwenye gazeti hata la udaku! halafu unajifanya eti mtu wa usalama uongo mtupu! Wewe endelea kupandikiza fikra zako, na kwa watanzania umeshawaweza, maana wanakuamini mauongo yako, eti mara upo DRC, uongo mtupu!!
 
Nauli ya 200/- si kigezo cha kupiga mbizi eti kwa kushindwa kulipa. Mbona ubungo Terminal tunalipa 200/- ili uvuke geti kwa miguu yako. Wasafiri na wanawaunga mkono tutafakari zaidi!

Ubungo watu wanaenda kwa nadra,tofauti na fer ambako inamlazimu mtu kuvuka kuja kuganga njaa katkat ya jiji.
 
huyo atafikishwa mahakamani kwa kuwa kesi yake inafanana sana na mtu aliyetaka kujinyonga ikashindikana,so dogo atashitakiwa kwa kosa la kutaka kujitoa uhai.hakuna lingine na hii itatoa fundisho kwa wale wote waliokuwa na nia kama yake,hahahahahaha

kazi kwelikweli tz

au kwa kosa la kupinga armi halali ya waziri
 
Hivi mtu anapoogelea bila nguo kuvuka ng'ambo ya pili, akifika huko ataenda uchi hadi kwao? Nguo si zinakuwa zimebaki huko alikotoka?

si tumekosa vazi la taofa bora kutoka kivyetuvyetu. na taifa la wenda uchi
 
Ktk hali nisiyo amini, tumepokea taarifa za tukio lenye kufanana na la kigaidi pale feri, na tupofika amini usiamini tumekuta kijana anaekadiriwa kuwa na miaka 26 hivi, akiwa kituo kidogo cha polis kwa kutuhumiwa kuvuka kwa kuogelea,
Imeniwia vigumu sana kuamini, lakini nipo jaribu kumhoji akanimbia kuwa alikosa nauli ya shilingi 200 akaona bora apige mbizi kama agizo la magufuli lilivyo semwa!

Kutokana na taratibu za kiusalama imebidi tumchukue kwenda nae makao makuu kwa mahojiano zaidi!

UPDATES:

Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa kijana alitumwa na wapinga nauli mpya, kijana kabainisha wazi kuwa alipewa elfu hamsini, na watu ambao sasa tunawafatilia ili kujua zaidi kilicho nyuma ya pazia.

Suala hili linaonyesha limeingiliwa na vita ya kisiasa, hasa likilenga kukosoa kauli ya Magufuli!
Katika mahojiano niliyofanya nae kitaalamu zaidi kijana ni mvuvi wa pale feri na tenda hiyo alipewa tangu jana, anazidi kuweka wazi kuwa watu waliompa kazi hiyo walikuwa wawili wakitumia gari plado nyeusi na walivaa mmoja shati jeupe,na mwingine hakumbuki vema!

Kulingana na maelezo yake nimeamua kumtoa mahabusu kwa kutumia oda ya kiwanausalama na sasa nimempa laki moja kwa maelezo kuwa nampongeza kwa ujasiri wa kuvuka bahari, lakini lengo langu anisaidie kujua nani zaidi walimtuma na lengo lao zaidi ya kupinga nauli kingine nini?? Nimemrudisha mpaka feri lakini ktk mazingira ambayo hajui kuwa mimi ni mmoja ya waliyomchukua pale kigambo feri!

Nahisi lipo kubwa zaidi ya nauli, nalo ni vita ya wanasiasa wabunge na waziri magufuli!

Subirini nitawajuza!

Tuna subiri utujuze hiyo vita ya wabunge na maghufuri.
 
Nikweli hapa nilipo kichwa kinaniuma sana, kwanini tumemkamata?? Yani najiuliza na kila mmoja wetu hapa anajiuliza kwanini tumemkamata? Lakini viongozi wetu wanasema afikishwe mbele ya sheria!

Mtamfikisha mbele ya sheria kwa kosa gani? Je ni kosa la jinai kuvuka upande wa pili kwa kuogelea? Au ni kosa kuvuka kwa kuogelea kwa sheria gani? Kama kuna sheria inayozuia kuvuka bahari kwa kuogelea mtaeleweka kama hakuna mtaishia kuonekana vichaa tu.
Zaidi ya hapo, kama kuna sheria ya namna hiyo kwa nini Magufuli aliwaagiza wasio na sh 200 wavuke kwa kupoga mbizi?
 
kumbe we ni polisi....

mi najua darasa la saba hawez kuwa na akili!! kuna polisi msomi!??!!!"'''' 99% ni vilaza, sina cha kuongea nao!!!!

Acha dharau za jumla jumla mkuu. Wapo polisi wasomi wengi tu. Tatizo lao ni hilo suala la amri amri.
 
Usikubali kuchezewa akili yako kama mtoto mdogo. Wabunge wa Dar Es Salaam ni WANAFKI. Haiingii akilini wapinge ongezeko la shilingi MIA na wakati huohuo wafurahie ongezeko la posho zao. TUMIA AKILI, USIKUBALI KUTUMIWA.
 
Acha dharau za jumla jumla mkuu. Wapo polisi wasomi wengi tu. Tatizo lao ni hilo suala la amri amri.

hii kweli na si dharau. Wengine wamefali drs la saba, f4 na f6. Rafiki zangu wengi walio feli wako polisi, wakuu wa idara mbalimbali.
 
Usikubali kuchezewa akili yako kama mtoto mdogo. Wabunge wa Dar Es Salaam ni WANAFKI. Haiingii akilini wapinge ongezeko la shilingi MIA na wakati huohuo wafurahie ongezeko la posho zao. TUMIA AKILI, USIKUBALI KUTUMIWA.

kwa hiyo wabunge wakikubali posho hawatakiwi kuwatetea wananchi?
 
Nachukulia kivuko cha kigambon kama daraja tu! Unavuka toka nyumbani unakuja mjini kutafuta ugali! Haina tofauti na lile daraja la salender!

hili jambo linapotoshwa sana na wanasiasa ... watu hamuongelei gharama zote badala yake mnakomalia sh 200 tu ... nani kagoma kulipa hiyo sh 200?? wanachohoji wananchi ni ushirikishwaji wa kufikia maamuzi hayo pamoja na rationale nzima; mbona hamjadili kupanda kwa bei ya kuvusha guta kutoka sh 300 mpaka 1800 wakati gari ndogo ni kutoka sh 800 mpaka 1500?? bei za mizigo kuanzia kilo 50 sh 500??

... kwani haongeli wizi unaofanyika na vibarua na wafanyakazi wa kivuko pale?? hili liko wazi na kila mtu kule analijua ... wafanyakazi pale wanafukuzwa kila leo kwa michezo yao ya risiti feki ... na wale maafande wanaopiga dili kila siku pale kwa wanaopita juu kwa juu mbona hamliongelei?? ... kwa nini msiyadhibiti haya?? mnadhani wananchi ni vipofu na maovu yanayofanyika pale hawayaoni?? kwa nini sasa mnawatwisha wao huo mzigo??

binafsi namkubali sana magufuli lakini katika hili namshauri awe mstaarabu sana sababu kuna mahali watendaji wake wamemuingiza chaka l... watetezi na washauri wa magufuli inabidi pia mjipange sana maana response ya wananchi wa kigamboni though wako kimya lakini iko very negative; politically huu uamuzi utawa cost sana magamba ... mbaya zaidi wengine hata huko kigamboni hawajawahi kufika wanabaki kupayuka tu hapa .... only time will tell!
 
hii kweli na si dharau. Wengine wamefali drs la saba, f4 na f6. Rafiki zangu wengi walio feli wako polisi, wakuu wa idara mbalimbali.

jamani wapo polisi waliosoma na kufaulu vizuri na wengi wao ndo waliobadilisha fani na kuacha upolisi. waliobaki ndo hao felia ambao wamebaki kuitikia tu NDIO AFANDE
 
kwa hiyo wabunge wakikubali posho hawatakiwi kuwatetea wananchi?

Huitaji kuwa na elimu hata ya darasa la saba kujua jibu la swali lako. Tatizo watanzania wengi tunapenda kuishi maisha ya ujanjaujanja sana, wewe nauli hiyo ya shilingi mia ipo tokea 1997. Sasa hivi hakuna nauli ya shilingi 100 kwenye daladala hata kama utaenda kituo kimoja tu. Mwanza watu wanalipa hadi shilingi 500 kwenye vivuko how comes Dar ulipe sh. 100???! Siipendi CCM lakini kusema la ukweli wa Mungu hawa wapinzani wanachemsha sasa, UPINZANI HAUNA MAANA YA KUPINGA KILA KITU. 1. PIGA MBIZI 2. ZUNGUKIA KONGOWE 3. RUDI KIJIJINI. Kama hao wabunge wanatuonea huruma kweli wakichukue kivuko wakiendeshe kwa hiyo shilingi mia, Magufuli ameshakubali.
 
Huitaji kuwa na elimu ya chekechea kuwa na mtazamo mzuri zaidi ya huu na kuona mantiki halisi ya kelele za watu juu ya ongezeko la nauli na hasa kauli tata iliyoambatana na upandishwaji nauli zenyewe
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom