Kijana anayeanza maisha na anataka kufunga ndoa afanye nini ili kupunguza gharama?

Akilitime

JF-Expert Member
Dec 27, 2017
581
757
Wakuu wanajukwaa wasalaam,

Msaada, kwa kijana anayeanza maisha na anataka kufunga ndoa ya kikristo bila kutumia gharama kidogo za harusi.

Au afanyeje ili kuepukana na gharama za harusi, je umewahi kushuhudia ndoa/ harusi ya bei rahisi? Je likuwaje?

Je umewahi kuhudhuria ndoa isiyo na harusi? Je ilikuwaje na ilitafsiriwaje na jamii?

Naomba tupeane ujuzi wakuu!

1621322825052.png

Hakuna shughuli ndogo ndoa ni wewe unavyojipanga, kwanza uhakikishe unamenunua nguo ya bibi harusi na bwana harusi pia ujue unataka kualika watu wangapi? Je sahani ya wali unataka ya bei gani zipo hadi 50k per plate hila hadi 15k per plate ukumbi nikitu cha msingi ukishajua hayo unayoyataka utakuwa umemaliza shughuli.
 
Aende akaandikishe ndoa kanisani kwanza ajue gharama zake

Then atafute hotel moja ya kawaida aulize gharama ya chakula akijua wakubaliane bei kwa idadi ya watu atakohitaji atalipia kwa sahani plus vinywaji

Simple iwe kama Family Dinner akitoka hapo na Mkewe wakaanze maisha.
 
Harusi rahisi ni kufanya kati kati ya wiki watu wapo busy offisini , wewe unakuwa na siku ya off , unaenda kanisani baada ya kuandikisha hiyo ndoa kanisani, baada ya hapo mnaenda kufanyia sherehe nyumbani ndugu wachache na chakula kinaweza kupikwa hapo hapo home au unakodisha wapishi wanakuja pikia nyumbani, au unaenda kuchukua chakula kwa wapishi pale Jangwani au karibu na unapoishi
 
Mkuu
Hakuna shughuli ndogo ndoa ni wewe unavyojipanga,kwanza uhakikishe unamenunua nguo ya bibi harusi na bwana harusi pia ujue unataka kualika watu wangapi?je sahani ya wali unataka ya bei gani zipo hadi 50k per plate hila hadi 15k per plate ukumbi nikitu cha msingi ukishajua hayo unayoyataka utakuwa umemaliza shughuli.
Mkuu mbona tunatishana hivi? 50/plate ?

iyo ishakuwa changamoto Mkuu, bei kubwa hivo
 
Harusi rahisi ni kufanya kati kati ya wiki watu wapo busy offisini , wewe unakuwa na siku ya off , unaenda kanisani baada ya kuandikisha hiyo ndoa kanisani , baada ya hapo mnaenda kufanyia sherehe nyumbani ndugu wachache na chakula kinaweza kupikwa hapo hapo home au unakodisha wapishi wanakuja pikia nyumbani, au unaenda kuchukua chakula kwa wapishi pale Jangwani au karibu na unapoishi
Ubarikiwe sana
 
Kaandikishe ndoa, siku ya ndoa ikifika nendeni mkafungishwe mkitoka hapo haoooooo nyumbani. Taarifa ni kwa wazazi na ndugu wachache sana ambao mtawambia siku kama kesho yake mwaenda kufungishwa ndoa.

Hakuna sherehe
 
Harusi Nini? Na Ndoa Nini? Angalia unataka Nini unataka Harusi au unataka kufunga Ndoa Takatifu? Ndoa Haina Gharama yoyote... Hakuna mahala pameandikwa Wanandoa lazima wavae suti au Shera.. Ndoa inaweza kufungwa kanisani na Mkimaliza kubarikiwa mnatawanyika na kuendelea na shughuli zenu.

Ila harusi ndiyo sherehe ifanywayo baadae ya wanandoa kupata ubarikio wa Kindoa kanisani!
Kwa kifupi Harusi ni Sherehe inayohalalisha umaskini kwa wanajumuia wanaokuzunguka ..Harusi Ni Anasa yenye majuto mbeleni..

Harusi siyo Ndoa
 
Ndoa ambazo hazina harusi ni nyingi sana kwanza kabisa kanisa katoliki linahimiza ndoa isiwe na gharama kubwa maana Jambo hili linawakwaza vijana kila wakifikiria harusi kubwa na hela hawana! Nenda kanisani kaandishe ndoa.

Nunua nguo yako ya kawaida siku ya ndoa ambatana na msimamizi wako na jamaa wachache wa karibu ndoa itafungwa vzr kama utaweka chakula kidogo kwa wageni wachache ni maamuzi yako kama utapanda bodaboda au bajaji na mkeo ni ww kama utaamua kwenda geto kwako ni ww tu! Ukitaka makuu au madogo ni maamuzi yako mwenyewe.

Haupo kuoa ili ufurahishe jamii
 
Ndoa haina gharama kubwa gharama yake ni kuandkisha kanisani na kulipia vyeti vya ndoa na ukishafunga kanisani ndoa imekamilika kinachofuata hapo ni harusi au sherehe ya ndoa ambayo unaweza kuifanya kulingana na uwezo ulionao au kama huna uwezo hata usipofanya hakuna dhambi kumbuka "fahali bila Mali ni mhali"
 
Nishaona sana ndoa zikifungwa kanisani katika misa za asubuhi (zile misa za katikati ya week) na ndugu/jamaa wachache, watu wakitoka hapo kila mmoja na mihangaiko yake.

Hivyo uchaguzi ni wako tu.
 
Ndoa ambazo hazina harusi ni nyingi sana kwanza kabisa kanisa katoliki linahimiza ndoa isiwe na gharama kubwa maana Jambo hili linawakwaza vijana kila wakifikiria harusi kubwa na hela hawana! Nenda kanisani kaandishe ndoa.

Nunua nguo yako ya kawaida siku ya ndoa ambatana na msimamizi wako na jamaa wachache wa karibu ndoa itafungwa vzr kama utaweka chakula kidogo kwa wageni wachache ni maamuzi yako kama utapanda bodaboda au bajaji na mkeo ni ww kama utaamua kwenda geto kwako ni ww tu! Ukitaka makuu au madogo ni maamuzi yako mwenyewe.

Haupo kuoa ili ufurahishe jamiias
 
Nishaona sana ndoa zikifungwa kanisani katika misa za asubuhi (zile misa za katikati ya week) na ndugu/jamaa wachache, watu wakitoka hapo kila mmoja na mihangaiko yake.

Hivyo ucdhaguzi ni wako tu.
Amen
 
Nimekwambia hata ya 15k zipo ila hapo ni wali mweupe tu hakuna matunda wala ndizi!
hahhaaaaaaaaaa uwiiiii mbona hizo za 15k zina maatunda , soup, biriani, wali na pilau haizzzzzinaga mbwembwe sana ila cha kufanya yy ajipange kwa bajeti yake ilivyo
 
unataka NDOA au HARUSI (sherehe)......ila ktk yote wanawake ndio shiiiida....ndoa bila sherehe ya harusi hakuelewi....japo wapo waelewa wachache....kama wako muelewa ishu very simpo blaza....
 
Wakuu wanajukwaa wasalaam,

Msaada, kwa kijana anayeanza maisha na anataka kufunga ndoa ya kikristo bila kutumia gharama kidogo za harusi.

Au afanyeje ili kuepukana na gharama za harusi, je umewahi kushuhudia ndoa/ harusi ya bei rahisi? Je likuwaje?

Je umewahi kuhudhuria ndoa isiyo na harusi? Je ilikuwaje na ilitafsiriwaje na jamii?

Naomba tupeane ujuzi wakuu!

Kupunguza gharama afanye moja kati ya hapo..

1.asianze maisha kwanza badala yake jambo la mwanzo aoe hapo atapunguza gaharama.

2.Asioe kwanza badala yake aanze maisha kwanza kisha atakuja kuoa baadae mambo yakikaa sawa.
 
Back
Top Bottom