Kijana anakunywa maji lita 100 kwa saa mbili, tangu apigwe na radi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875

Mkazi wa kijiji cha Maguu wilayani Mbinga mkoani Ruvuma Erick Msuha ayesumbuliwa na matatizo mbalimbali ya kiafya yanayomsababishia kunywa lita mia moja za maji kwa saa mbili ili aendelee kuishi anaomba msaada aweze kutibiwa.

Mgonjwa huyo anasema matatizo yake yamemuanza baada ya kupigwa na radi mwaka 1993 lakini katika miaka ya hivi karibuni hali imekuwa mbaya zaidi ambapo amekuwa akitumia lita 100 za maji ambayo huyatoa kwa njia kutapika na njia ya haja ndogo huku akicheua.

Baba wa mgonjwa huyo Bw. January Msuha anasema mwanae anateseka sana na hawezi kulala kutokana na yanayomsibu na wao wameuza kila walichonacho kumsaidia bila mafanikio na hivyo wanawaomba wasamaria wema kuwasaidia.
 
Ukipigwa na radi au umeme.. Unaungua hii hupekekea kupungukiwa maji mwilini,,,, kwa sababu ngozi ilipongua itashindwa kufanya kazi ya kuzuia maji yasipotee..
Hii hutikoea muda huo huo.. Siyo kitu cha kudumu..
Sidhani kama kuna link ya Maji na kupigwa radi... Huenda ana Hydrophilia tu.
Habari ingekamilika vizuri kama tungejua hospital wamesemaje?
 
Mkazi wa kijiji cha Maguu wilayani Mbinga mkoani Ruvuma Erick Msuha ayesumbuliwa na matatizo mbalimbali ya kiafya yanayomsababishia kunywa lita mia moja za maji kwa saa mbili ili aendelee kuishi anaomba msaada aweze kutibiwa.

Mgonjwa huyo anasema matatizo yake yamemuanza baada ya kupigwa na radi mwaka 1993 lakini katika miaka ya hivi karibuni hali imekuwa mbaya zaidi ambapo amekuwa akitumia lita 100 za maji ambayo huyatoa kwa njia kutapika na njia ya haja ndogo huku akicheua.

Baba wa mgonjwa huyo Bw. January Msuha anasema mwanae anateseka sana na hawezi kulala kutokana na yanayomsibu na wao wameuza kila walichonacho kumsaidia bila mafanikio na hivyo wanawaomba wasamaria wema kuwasaidia.
Mapepo hayo akaombewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wekeni hapa namba yake ya sim, tuweze kumchangia na wakiwepo wataalamu wa afya watatupa ushauri kitaalam zaidi, Mungu ni muwezaji wa yote, tunamuombea mgonjwa, unaposikia watu wana matatizo ndiyo haya sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom