Kijana Amiri Mtoi mhanga wa bomu la Arusha amezikwa leo Mkuzi - Lushoto.

Dec 11, 2010
3,321
6,328
Ndugu zangu.

Kijana Amiri Mtoi ambaye ni mtoto wa kaka yetu Mtoi Kolowa Daffa (mtoto wa baba yetu mkubwa) amezikwa leo majira ya saa 5 kijijini kwetu Mkuzi wilayani Lushoto.

Marehemu Amiri ni miongoni mwa wahanga wa tukio la bomu kule Arusha, amesafirishwa usiku kuamkia leo na amezikwa mapema asubuhi kufuatia imani ya dini yetu lakini pia ili kutoa fursa ya watu walio sindikiza mwili kutoka Arusha waianze safari yao mapema.

Amiri Mtoi amekatishwa masomo angali darasa la tatu, amiri hakuwahi kufikiri wala kuzadhani kuwa atakufa akiwa na tundu la risasi kwenye mwili wake, nimeangalia picha zake nimeumia sana, ametangulia mbele ya haki, walio rusha risasi nao watamfuata, Mwenyezi Mungu atawalipa, sio kwa dua mbaya za familia, lakini kwa mapenzi yake yeye (Mungu).

Watu wa Arusha kwa wingi na umoja wao wameonyesha ushirikiano wa kutosha.
Kwa niaba ya wana ukoo wa Mtoi tunawashukuru sana!

Tumuombee Amiri apumzike kwa amani baada ya kukatishwa uhai wake na watu wasio kuwa na huruma na wenye kujiona wao pekee ndio wenye mamlaka ya kuitawala Tanzania na kuamua nani aishi na nani atangulie mbele za Mungu.

Itoshe kusema.

Inauma sana, hasira zangu dhidi ya ccm hazita koma na wamefungua ukurasa mpya wa mapambano dhidi yao, sisi ni maskini na wanyonge hatuwezi kumiliki bunduki wala bastola zenye risasi lakini tunaweza kuuwa kwa kutumia sanduku la kura. Nitayaongoza mapambano

"All those that fight when oppressed incur no guilt, but Allah shall punish the
oppressor." Come the day.

Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums.
 
Oh that is very sad! poleni sana Mungu awafariji, ni jambo gumu na la kuhuzunisha sana ukizingitia mazingira yaliyopelekea, ni uonevu na ni damu hata isiyo na hatia, inatia uchungu kwa kweli. Pole sana kwako kwa familia
 
Pole rafiki Mohamedi Mtoi
Hakika Mwenyezi Mungu atalipia kwa kitendo hiki cha kinyama. Wanadhani wanatia watu hofu kumbe wanatoa sababu zaidi na ari ya kuundoa madhalimu haya.
Mungu yupo
 
Last edited by a moderator:
Mungu awajaze nguvu , naamini huyu Mungu bado yupo na hajazeeka kiasi cha kushindwa kuwahukumu waliotenda uovu huu.....fikiria wewe ndio mzazi na huyu ndio mwanao halafu anajitokeza Mjinga mmoja anatoa kauli kama za Nnape na Lukuvi.........
 
Poleni sana wafiwa. Kwa hakika ni msiba wetu wote.
Mabadiliko ni lazima kutokea na hasa kipindi ambacho watu wanataka mabadiliko.
 
Ndugu yangu Mtoi inauma sana.Na kila mwenye akili na akaamua kuzitumia anajua hili
 
Ndugu zangu.

Kijana Amiri Mtoi ambaye ni mtoto wa kaka yetu Mtoi Kolowa Daffa (mtoto wa baba yetu mkubwa) amezikwa leo majira ya saa 5 kijijini kwetu Mkuzi wilayani Lushoto.

Marehemu Amiri ni miongoni mwa wahanga wa tukio la bomu kule Arusha, amesafirishwa usiku kuamkia leo na amezikwa mapema asubuhi kufuatia imani ya dini yetu lakini pia ili kutoa fursa ya watu walio sindikiza mwili kutoka Arusha waianze safari yao mapema.

Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un

Poleni sana kwa msiba,hakuna mtu atakayeishi milele.bali ni kuwahurumia waliofanya vitendo vya mauaji bila kuangalia umri wa mtu....mtoto mdogo namna hiyo hata hajui nini anafuata pale,ANAULIWA...kwa kuwa tu wanajua watatetewa na hakuna wakuwafanya chochote kwani pia imekuwa ndiyo gear ya kupandishwa CHEO...yana mwisho tena haupo mbali huo mwisho,watafichuliwa hata wakiwa mapangoni au wakiwa wafu na wao kuhakiki DNA zao kama kweli nao wamekufa
 
Pole sana Mkuu mohamed mtoi kwa kumpoteza ndugu yako akiwa bado na ndoto nyingi za maisha yake akiwa na mawazo ya kufika mbali kwenye elimu yake akiwa bado anahitaji kuishi na kuyaona maisha yake na akijaliwa kutimiza malengo aliyojiwekea. Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake kwa amani japo ameondoka akiwa mdogo sana na bado akiwa anahitajika. Poleni sana wafiwa.
 
Last edited by a moderator:
inasikitisha sana na inaumiza mno !
hawa ni baadhi tu ya wapigania uhuru wa pili wa matanzania.poleni familia ya Mtoi na Mungu awape nguvu zaidi.
 
poleni sana kaka binafsi nimeumia sana na hivi ninavyo andika machozi yananitoka,naomba niishie hapo
 
Back
Top Bottom