Kijana aliyetuma picha za Nyufa za Hosteli za Magufuli UDSM akamatwa na Polisi, anyimwa dhamana

king Davidson

JF-Expert Member
Feb 9, 2017
252
1,063
Kijana Kumbusho Dawson Kagine Amekamatwa kwa kosa la kutuma PICHA za hosteli za Magufuli za UDSM. Yupo kituo cha Polisi UDSM na anapelekwa Central!


======

UPATES:

Amenyimwa dhamana

Dar es Salaam. Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Kumbusho Dawson anashikiliwa na polisi akituhumiwa kusambaza picha kuonyesha nyufa kwenye majengo ya hosteli.

Dawson ambaye ni mbunge wa serikali ya wanafunzi (Daruso) ameshikiliwa leo Jumatatu Desemba 4,2017 mchana.

Akizungumza na MCL Digital Makamu wa Rais wa Daruso, Anastazia Anthony amethibitisha kukamatwa kwa mbunge huyo saa saba mchana.

"Ni kweli Kumbusho amekamatwa na kupelekwa kituo cha polisi cha Chuo Kikuu kwa ajili ya kuhojiwa lakini ilipofika saa tisa alasiri polisi wamesema hawana uwezo wa kumuhoji hapa hivyo watampeleka Oysterbay," amesema Anastazia.

Alipotafutwa kwa simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Murilo Jumanne hakupatikana kuzungumzia kukamatwa kwa mwanafunzi huyo.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alipotafutwa amesema hana taarifa kuhusu tukio hilo.

Amesema anasubiri atakapofikishiwa taarifa atazitoa kwa umma.

Moshi Moshi, mwanafunzi wa UDSM akizungumzia kukamatwa kwa Dawson, amesema ameshughulikia dhamana yake katika Kituo cha Polisi Oysterbay lakini polisi wamesema hawezi kupewa.

Chanzo: Mwananchi

UPDATE:

Mwanafunzi aliyesambaza Picha za Nyufa Hostel UDSM Aachiwa kwa Dhamana Usiku


Post Zake kijana huyo kwenye mtandao wake wa Facebook hizi hapa

Andiko la kwanza kabisa

"Nimetoka New Hostel (Magufuli Hostel), Hosteli ambazo rais wetu amepigania mpaka zikajengwa kwa Shilingi Bilioni 10 tu za Kitanzania.

Ni Ajabu sana, Huenda hizi zikawa ni hosteli zilizojengwa kwa kiwango cha chini kuliko hosteli zote barani Afrika.... Nitawaletea picha hapa siku ya kesho au ikiwezakana baadaye...... Mtatoa machozi.

Hatupo Salama...... Naomba msinipige risasi mpaka nitoe ushahidi.

NB:
Hosteli hizi zimejengwa kwa Bilioni 10 tu"

[HASHTAG]#Bilioni10Tu[/HASHTAG].



"#JOHN_POMBE_MAGUFULI_HOSTEL.

Ikiwa ni takriban ya Wiki nne tu toka hosteli hizi kuanza kukaliwa na Wanafunzi hatimaye Nyufa kubwa na za kushangaza zimenza kujitokeza kwenye mojawapo ya
Majengo haya alimaarufu kama JOHN POMBE MAGUFULI HOSTEL.

Hosteli hizi zilizinduliwa na Mh. Rais mwanzoni mwa mwaka huu na zimeanza kukaliwa Mwezi wa 11 mwaka huu.

Ajabu ni kuwa nyufa zimezidi kuota kwenye mojawapo ya majengo haya. Hosteli hizi zimebeba takribani ya Wanafunzi 3840.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli alidai kuwa majengo haya yalijengwa kwa bilioni 10 tu za kitanzania ingawa takwimu za Mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali yaani CAG waliweza kubaini kuwa majengo haya yalijengwa kwa Sh. Bilioni 54 ... Majengo haya kujengwa kwake yametumia miezi Sita tu kukamilika kwake.. Taarifa za awali zinadai kuwa hosteli hizi huenda zikawa ni mojawapo ya Hosteli zilizojengwa kwa kiwango cha chini kuliko Hostel zozote Barani Afrika.

Pichani ni MAGUFULI HOSTEL.
Andika [HASHTAG]#Bilioni10[/HASHTAG] Kwa kilugha chako..... Twende kazi."


Andiko la Pili


MAJIBU YANGU KWA TBA.

Masaa matatu yaliyopita nilichapisha andiko langu hapa kwenye ukarasa wa Facebook nikielezea Jengo la Hostel lililojengwa kwa hisani ya Rais wetu mpendwa John Pombe Magufuli nikielezea kuwa yamepata nyufa.

Ofisa Mtendaji mkuu wa TBA bwana Elias Mwakalinga ameliambia Mwananchi kuwa anajiandaa kwenda kuangalia kama ni kweli, akaenda mbele zaidi na kusema kuwa huenda kuwa hosteli hizo ni za majengo mengine zimehusishwa na majengo mengine.

Nimuombe Mkurugenzi wa TBA Mh. Elias Mwakalinga kuwa sijafananisha na majengo mengine na picha hizo ni za kweli na nimepiga mwenyewe.

Nendeni Hostel Block A, nitafuteni niwasadie kuwaonyesha nyufa zilipo.

Naomba niongezee kuwa tatizo sio hilo tu, tutafutane tuwaambie na matatizo mengine.

Tunawakoa ili kuwasaidia, msituone maadui na kutafuta visingizio vingine eti majengo yatakuwa sio yenyewe....

http://www.mwananchi.co.tz/…/1597578-4213244-7p1…/index.html

© Kumbusho Dawson



Andiko la Tatu

"SIO TU NYUFA BALI TBA TOLEEÑI UFAFANUZI WA MIUNDO MBINU YA MAJI MACHAFU NA BAADHI YA MAKABATI.

Jana baada ya kuchapisha Chapisho langu kupitia ukurasa wangu wa Facebook ukielezea Nyufa zilizopo kwenye mojawapo ya jengo ambalo ni Block A, TBA walifunga safari kuja kuthibitisha kama kuna nyufa kweli New Hostel.

Sio tu Nyufa bali TBA wakubali kuwa majengo haya waliyejenga Chini ya kiwangi likiwemo Block A ambalo limeanza kutoa nyufa.

Zaidi ya Nyufa lazima tukubali kuwa bado majengo haya baadhi ya miundo mbinu ni mibovu ikiwemo maji machaf hasa Mabafuni. Mabafuni hali ni mbaya sana wanafunzi wachache tu wakioga maji yanatuama na kupelekea maji machafu kuanza kutembea korodoni.

Lengo la machapisho yangu haya ni kuwasaidia TBA kuboresha na kufanya ufanisi zaidi siku za mbeleni huko watakapo pewa kazi nyingine. Hebu tuachanane na suala la miundo mbinu ya maji machafu.

Suala lingine ni hili (Ingawa sina uhakika kama hii ni kazi ya TBA au kuna mtu meingine alipangiwa kazi hii) Kuhusu makabati yaliyotlekezwa takribani ya wiki 3 sasa bila kufikisiwa ukutani. Ni nini hasa chanzo ? Je mafundi wamepangiwa kazi nyingine ama?? Au ni tatizo la kifedha??. (Nendeni block

Nategemea TBA baadaye na hili watalifanyia kazi. Lakini suala la msingi niwapongeze TBA baada ya kuona machapisho yangu kupitia ukurasa wangu jana saaa usiku 3 usiku walifunga safari kuja Magufuli Hosteli kuangalia nyufa hizo. (Hakika mmeonyesha kuwa mnawajali wanafunzi) Heko kwenu.

Nategemea mtafanya marekebisho kwenye miundo mbinu ya maji pia kwani ni mibovu.
(Tembeleeni block A, na Block B)

Tukosoe kusaidia, tukusoe kwa manufaa ya Taifa.

Change ni mimi, ni wewe ni sisi..... TWAWEZA.

1f637.png
Pichani ni baadhi ya maji machafu yaliyotuama Kwenye korodi na baada ya kujaa bafuni.

1f637.png
Picha ya pili ikionyesha Makabati yaliyotelekezwa bila kufiksiwa ukutani

Cc. Lucy Magereli
John Heche
Hawaa Mwaifunga Bananga
Ally Bananga
Patrick Ole Sosopi
Iringa DC
Aisha Luja
Neema Godfrey Tz
Hilda Newton Chadema
Kenani Kihongosi

©Kumbusho Dawson"

Habari zaidi soma=>TBA yakiri kubomoka kwa mabweni ya UDSM, yatoa sababu zake

Jeshi la Polisi, Dar es Salaam limesema halina taarifa ya kukamatwa kwa Kijana aliyetuma picha za Nyufa za Hosteli
 
Sheria ya huduma za habari imeanza kung'ata, kama hana cheti cha uandishi wa habari kazi anayo.
Mbona YEYE hafuatishi sheria.. Ngoja yaanguke! Badala ya kumkamata mjenzi mnakamata Raia mwema aliyeonyesha tatizo? Mbona Tanesco wanasemaga MTU akiona nguzo au waya iko chini atoe taarifa.

Hii ni nchi yetu sote, wao kua viongozi haina maana kua wao wanaakili kubwa kutuzidi sisi wengine zaidi ya 50mil.
 
Back
Top Bottom