Kijana aliyeripoti nyufa hostel za Magufuli (Kumbusho Kagine) adai amenusurika kutekwa na watu wasiojulikana

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
USALAMA WANGU UPO MASHAKANI.

Kumbusho Dawson Kagine

"Toka Mwaka jana mwezi wa 12 baada ya mimi kupiga picha katika mojawapo ya Hostel za Dr. John Pombe Magufuli iliyokuwa ikionyesha nyufa kumekuwa na watu ambao wamekuwa wakinifuatilia mara kwa mara kila mahali ninapoenda, (Siwezi kusema kupiga picha za nyufa ndio sababu ya kunifuatilia kwangu au la), awali nilidhani labda wanashughuli zao lakini kilichonishangaza ni kuwa kila siku zinavyoidi kwenda nikikaa sehemu watu hawa nao walikuwa wanakaa umbali kidogo nilipo mimi, nami nikianza kuondoka nikigeuka nyumba nabaini kuwa wananifuatilia.... Siku zinavyozidi kwenda nimebaini watu wale walikuwa na nia mbaya kwangu.

Wiki jana, siku ya Alhamisi nikiwa natoka Mlimani City nilianza kutembea kurudi zangu hosteli nikipita ile njia ya Service road mbele yangu niliona gari aina ya Noah imepaki na mlango ukiwa wazi (Mbele kidogo ya geti la Mlimani City) nilivyofika kwenye ile gari watu wale walinitaka niingie kwenye gari huku wakiwa ndani ya gari lile! Mimi niliwajibu, "Mnanifahamu??.... Mnajua ninakoenda??...... Wakati nikiwauliza haya maswali walianza kushuka kwenye gari huku wakiniambia sio lazima kutujua sisi ni akina nani...... " Ingia kwenye gari haraka" waliniambia kwa ukali.

Namshukuru Mungu kulikuwa na watu jirani wakiwemo wakiwemo waendesha bajaji waliokuwa wamepaki nyuma kidogo, hivyo nilipiga kelele kuwaeleza kuwa wanataka kuniteka.

Baada ya mimi kupiga kelele watu wale waliokuwa wanashuka kunitaka kunilazimisha niingie kwenye gari waliingia haraka na kuliondosha gari lile.... Kipekee niwashukuru waendesha bajaji kwa msaada wenu, hakika msingekuwepo nyinyi pale leo tungekuwa tunazungumza mengine.

Baada ya tukio lile niliripoti kwenye vyombo tofauti vya ulinzi ikiwa ni pamoja na Polisi wasaidizi (Auxiliary Police) na Polisi wenyewe na kuandikiwa RB yenye kumbukumbu namba UD /RB/344/2018...... Polisi waliniomba endapo nitaziona sura zile mahali popote zikinifuatilia nitoe taarifa huku wakiniomba nisitembee peke yangu kila sehemu ninapoenda na kunieleza kuwa nitakapoona inafaa nijilinde.

Hali kadhalika suala hili niliripoti kwa walezi wangu wanaonilea kwa maana ya Ofisi ya Mshauri wa Wanafunzi hapa chuoni kwangu.

Rai yangu kwa nyie vipele mnaonifuatilia waambieni hao wanao watuma wauache utoto....... Mlimpa nini Kumbusho Dawson mpaka mnamfatilia hivi??? kama mnanidai njooni nitawalipa.
 
Tukileta thread za kuonya mods mnafuta

Eleweni hawa watu wako desperate kufanya lolote na mjue hawana aibu wala haya.

Mnalodhani haliwezekani,wao kwao linawezekana.

Tuko katika zama ambazo hazijawahi kutokea huko nyuma na pengine hazitatkuja kutokea tena huko baadae.

Kosa la bwana Kumbusho na hao madereva wa Bajaji ni kuto-note namba za hiyo gari.

Kutaja namba kungesaidia habari hii isionekane ni uzushi au ni propaganda tu.
 
Hakikisha unatembea na kiberiti, na ukiwaona piga kelele ili wachomwe moto. Hakuna haja ya kupelekana nao popote ni kupoteza muda. Hilo gari kama unalikumbuka namba pia iweke huku mitandaoni, popotwe itakapoonekana kiberiti kilihusu. Hakikisha ukimshuku mtu yoyote kukufuatilia mpigie kelele ya mtekaji huku ukijitambulisha wewe ndio uliyepiga picha majengo ya UDSM na hivyo wanataka kukuteka na kukuumiza kama Lissu. Nakuhakikishia haitachukua dakika 5 yoyote anayekufuatilia lazima ataaga dunia.
 
Pole yake Kijana, nyakati hizi hazifanani na Nyakati zile.

Amepewa ushauri nini cha kufanya naomba auzingatie.

Pia naomba nimuongezee ushauri mwingine tafadhali mfikishieni na auzingatie
"ASIMUAMINI MTU YEYOTE MAHALI POPOTE NA WAKATI WOWOTE"
 
Itakuwa ni washkaji wa mtaani mchizi aliwaibia demu au anaona maruweruwe, mshaurini aachane na siasa bado ni kijana mdogo, asishangae matokeo yake baada ya kumaliza chuo yasionekane wala jina lake lisionekane kwenye darabase.... Aachane na hii serikali anajiharibia future tu..
 
Polee sana Mkuu.jitaidi kutotembea pekee yako..Jitaidi pia kuwashilikisha watu katika kila ufanyacho..kila wakati fanya baadhi ya watu wajue ulipo..!
.....
Kile ulichofanya sio kidogo..umegusa maslahi ya watu wengi sanaa pale
 
Back
Top Bottom