Kijana aliyepata ajali amtafuta mpenzi wake wafungue kesi

GIB

JF-Expert Member
Mar 2, 2012
336
92
MKAZI wa Tungi Kigamboni, Dar es Salaam, Nicolaus Maganga(21) aliyevunjika mguu takribani miezi miwili iliyopita kutokana na ajali yapikipiki amefika katika ofisi za gazeti hili, jijini Dar es Salaam akimtafutarafiki yake wa kike wasaidiane kufungua kesi ya madai dhidi ya mtualiyesababisha ajali hiyo.

Maganga alifika katika ofisi za gazeti hili jana na kumtaja kwa jina mojamsichana anayemsaka kuwa ni Rehema ambaye katika ajali iliyotokana na kugongwana gari Januari 16 mwaka huu, alikuwa amempakia.

Kwa mujibu wa Maganga, baada ya ajali hiyo, alipoteza fahamu lakini msichanahuyo ambaye alikuwa naye kwa muda alimsaidia kwa kumpeleka katika Hospitali yaKigamboni kwa matibabu kisha kumfikisha Hospitali ya Wilaya ya Temeke kabla yakuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Maganga alisema baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Muhimbili aligundulikakuwa amevunjika mguu wa kulia katika sehemu ya paja na hivyo kuwekewa vyumaambavyo anatembea navyo hadi sasa.

Alisema kuwa baada ya kuruhusiwa kurudi nyumbani aliendelea kuishi na mpenziwake lakini baadaye aliondoka kwa hasira kutokana na kutoelewana jambo ambalolimekuwa likimuumiza.

“Mimi nilichokuja kuomba hapa ni mnisaidie kuniandikia habari ili nimpatempenzi wangu aje tusaidiane kufungua kesi ya madai dhidi ya aliyenigonga kwakuwa mpenzi wangu ndiye aliyeona gari na mtu aliyehusika maana yeye hakuumialakini mimi nilipoteza fahamu kwa hiyo sikuelewa chochote” alisema.

Kulingana na maelezo ya Maganga, hafahamu nyumbani kwa msichana huyo wala nduguzake kwa kuwa walikutana mtaani na kuamua kuishi pamoja kwa takribani mwezimmoja kabla ya ajali.

Alisema kuwa kwa sasa anaishi na bibi yake baada ya kukosa mtu wa kumsaidiahivyo mpenzi wake atakaporudi watasaidiana kufungua kesi na kutimiza ahadiwaliyowekeana ya kufunga ndoa kwa kuwa hapo awali walikuwa wakiishi kinyumbabila ndoa.

Nawasilisha

Tafakari

 
Mnh tatizo awakuwahi kuapa,wataudumiana katika shida na raha,...
 
lakini utaishije na msichana au mvulana bilakujua ndugu zake? au ndiyo yale yakukutana club ,mkielewana mnaenda kulianzisha??
Kazi kweli kweli.
 
Duh..vijana wetu wana[otea kwa kukosa maarifa.

Inawezekanaje mtu kusishi na mwenzio ambae hujui hata kwao? wala asili yake?
Viana UKIMWI utattumaliza!!
 
Kwanza huu ni utovu wa nidhamu, uneweza kuishi kweli na mtu mwezi hujui anatoka wapi kama wangekufa kwenye ajali ingekuaje. Vijana kuweni makini//
 
tume kutana kimjini mjini tunaa achana kimjini mjinii..yametimiaaaaaaaaa.
 
Kijana tulia huyo rehema kakukimbia coz unaumwa,achana nae hana mapenzi ya kweli,jikaze tafuta msaada kwa ndugu zako wakutibie upone haraka then tafuta hela atakuja tena hapo ndio umtoe nduki ya kufa mtu.
 
lakini utaishije na msichana au mvulana bilakujua ndugu zake? au ndiyo yale yakukutana club ,mkielewana mnaenda kulianzisha??
Kazi kweli kweli.
hii ni wazi tume-adopt umoja uliopitiliza, kwa swali hili la bwana Maganga kuna haja ya kuaanza ku-impose vi-element vya ukabila ili kuwa na uwezo angalau wa kuhoji kuwa "wewe ni nani", "unatokea wapi" nk
 
Labda aliyekugonga alikuwa mpenzi wa rehema awali na wewe ukamnyang'anya....
 
Back
Top Bottom